HATUNA UDHURU KATIKA KUSAMEHE
Mathayo
18:23-35
26 Basi
yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa
yote pia.
27 Bwana
wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.
28 Mtumwa
yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata,
akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho.
29 Basi
mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami
nitakulipa yote pia.
30 Lakini
hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.
Bwana Yesu
asifiwe mwana wa Mungu.
Bwana Yesu
alitoa mfano mfalme na watumwa wake ili iwe fundisho kwetu
Tumesamehewa
kwa gharama ya damu ya Yesu-dhambi zetu zote si kubwa wala ndogo zimesamehewa
na ndio maana tunaishi hata sasa kwa neema, wewe na mimi ni nani hata
tusisamehe.
haijalishi
tunaowapenda wametuumizaje, haijalishi ndugu zetu wamefanya nini hata tukaumia
kiasi kiasi cha kutaman kufa kwasababu ya Yesu kufa msalaban kwaajili ya makosa
nadhambi zetu ndugu yangu tunapaswa kusamehe
tunafundishwa
kwa habari ya mtumwa na Bwana wao, mmoja alikua akidaiwa maden makubwa
akamwomba bwana wake amvumilie angemlipa lakini yule bwana alimsamehe ile deni
yote. sasa aliekua amesamehewa deni nayeye akawa anamdai mtu aliombwa amvumilie
angelipwa lakini alikataa -hakumsamehe, ndivyo tulivyo wanadamu Mungu
anatusamehe makosa yetu lakini sisi hatuwasamehi wale wanaotukosea.
Kiwango
cha mabaya uliyofanyiwa ni kidogo kulinganishwa na wewe uliyoyatenda mbele za
Mungu hata ukasamehewa, hivyo hauna udhuru wa kusamehe.
Ukisoma
mstari wa 21 Petro anamuuliza Yesu nisamehe mara ngapi? Yesu akamwambia,
Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
Maana yake
kila unapotembea inatakiwa usamehe, kila kosa wewe ni lakusamehe tu hauna
udhuru wowote
Sababu
kubwa inayofanya tusisamehe ni kwamba tumechukulia vile tulivyofanyiwa ni
vikubwa na havipwi kusamehewa na pia ndani yetu upendo wa Ki-Mungu umeondoka,
kwani ndani yako kukijaa upendo kusamehe inakua ni kazi rahisi.
Hivyo omba
upendo wa Ki-Mungu ujae ndani yako ukifurika ndipo utaona wepesi katika kusamehe
Watazame
kwa jicho la pili wote wanaokukwaza, waone kama wametumwa na adui kukukwaza ili
wakutoe katika uwepo wa Mungu, wakutoe kwenye ushirika na Mungu hivyo
usiwatazame wao bali tazama kilicho ndani yao ambacho kinawasukuma wakukwaze,
ndio maana pia wanaokuudhi badae wanakuja kujuta kwa vile walivyokufanyia
sababu si wao yupo alie ndani yao anaewasukuma.
Wengine
mmejaziwa maneno yauzushi kuwa fulani kafanya hivi kumbe ni uongo tu ili
wakuchonganishe na muhusika, sikia iwe ni kweli au uwongo wewe samehe tu,
kumbuka tumeagizwa tuwasamehe wote waliotukwaza.siku zote kumbuka amri kuu ya
pili aliyotupa Bwana Yesu mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na
kwaakili zako zote na mpende jirani yako kama nafsi yako
Ukiwapenda
watu hutawachukia watu utasamehe siku zote.
Mungu
akubariki.
Kama
umebarikiwa na ujumbe huu share kwa ndugu jamaa na rafiki zako popote pale
facebook na kwenye magroup ya Whatsup hutaachwa hivyo hivyo bali utabarikiwa
kwa kuitangaza injili kwa kushare. Pia like Facebook Page yetu ya Nyumba ya
Sala kwa Mataifa Yote kwa masomo mengi zaidi.
Ukipenda
kutumiwa masomo ya Neno la Mungu kila siku kwa Whatsup tuma majina yako mawili
inbox, whatsup kwa namba ya Tigo 0657 048393 kuomba kuunganishwa kupewa masomo
kila siku na utatumiwa, pia kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo
chini, na Mungu wambinguni akubariki
sana.
Merito
Tagalile
~0657
048393
No comments:
Post a Comment