GHARAMA YA KULIPA ILI UTEMBEE NA MUNGU (Somo Na Mwl M, Mwambeso)
🔹Watu
wengi sana wanapenda kutembea na Mungu katika maisha yao, na hicho ni kitu
kizuri sana, lakini ni watu wachache sana ambao wanaelewa gharama wanayotakiwa
kulipa ili wafanikiwe katika jambo hilo.
🔸Mungu
anapenda kuona watu wake wanatembea pamoja nae kama walivyofanya wakina Henoko,
Ibrahimu, Daudi n.k, lakini ana kanuni zake ambazo watu wake wanatakiwa
kutembea nazo kila wakati.
🔹Kanuni
kubwa ni kufanya mapenzi ya yake (yaani mapenzi ya Mungu) katika maisha yako.
Yesu alisema kwamba Baba yake alikuwa pamoja nae siku zote na wala hakumuacha
kwasababu tu alikuwa anafanya yampendezayo (mapenzi ya Baba yake), Yohana 8:29
🔹Unapotaka
kufanya mapenzi ya Mungu na kutembea pamoja nae katika maisha yako, unatakiwa
kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo;
*1. LAZIMA
UKUBALI KUMPA MUNGU NAFASI YA KWANZA KATIKA MAISHA YAKO.*
➡Unatakiwa kumpa nafasi ya kwanza katika kila eneo la maisha
yako.
➡Nafasi ya kwanza kwenye moyo wako,nafasi ya kwanza kwenye
uchumi wako, wokovu wako, utumishi wako, ndoa yako, nafasi ya kwanza kwenye
muda wako, nafasi ya kwanza kwenye mipango yako n.k.
*2. LAZIMA
UWE NA UTAYARI WA KUFANYA CHOCHOTE NA KWA MUDA WOWOTE.*
➡Tarajia kwamba wakati mwingine Mungu atakutaka ufanye vitu
ambavyo havikuweko kwenye ratiba yako.
➡Anaweza akakuambia ingia kwenye maombi ya kufunga wakati
wewe haukupanga, anaweza akakuamsha usiku kumuombea mtu wakati wewe ulitaka
kulala, n.k. Unahitaji utayari wa wa hali ya juu sana vinginevyo utashindwa
kutembea nae. (2Timotheo 4:2)
*3. LAZIMA
UKUBALI KWENDA KINYUME NA MILA NA TAMADUNI AMBAZO ZIKO KINYUME NA NENO LAKE.*
➡Huwezi kutembea na Mungu wakati mila na tamaduni zingine
unazozing’angania haziendani na neno lake, mfano ibada za wafu, matambiko n.k.
➡Vitu ambavyo viko kwenye jamii yako na yeye havipendi lazima
ukubali kuviacha. (1Wakorintho 10:23)
*4. LAZIMA
UWE TAYARI KUTEMBEA KWENYE MAJIRA YAKE.*
➡Hili sio jambo jepesi, na linawafanya watu wengi wapishane
na muda wao wa kuinuliwa na Bwana/muda wa kujiliwa na Bwana/Appointed time.
➡Yanaweza yakawa ni majira ya kuoa au kuolewa, majira ya
kuanza utumishi n.k.
➡Shida kubwa inayokuja hapa ni kwamba sio rahisi sana
wanadamu wakakuelewa, kwa hiyo unazungukwa na hofu, na kuogopwa kutengwa.
*5. LAZIMA
UTAFUTE KIWANGO KIKUBWA CHA IMANI.*
➡Kutembea na Mungu kunahitaji Imani zaidi, kwasababu wakati
mwingine hutajua anakupeleka wapi.
➡ Angalia mfano huu, halafu utaelewa kiwango cha imani
ambacho kilikuwa kinahitajika, _Mwanzo 12:1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe
katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi
nitakayokuonyesha._
➡Huo ulikuwa ni mtihani mgumu saa kwa Ibrahimu ingawa
alifaulu.
➡Sijui ukiambiwa neno kama hilo na Mungu utajiuliza maswali
mangapi moyoni mwako! Na utachukua uamuzi gani!
➡Pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6).
➡Hata kwenye maisha ni vigumu sana kuambatana na mtu kama
humwamini.
*6.
UNAHITAJI UNYENYEKEVU.*
➡Unyenyekevu ni wa muhimu sana ili uweze kutembea na Mungu
katika maisha yako.
➡ Mungu mwenyewe asema kwamba anaketi pamoja na mtu aliyetubu
na kunyenyekea (Isaya 57:15).
➡Yakobo 4:6 … Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema
wanyenyekevu.
*7.
UNAHITAJI UTII*.
➡Jambo la utii wa mtu ni la muhimu sana kwa Mungu kuliko
sadaka zake(1Samweli 15:22)
➡Mungu anaupa utii nafasi kubwa sana kuliko sadaka.
➡Utii ni mlango mkubwa sana sana wa mtu kufanikishwa na Bwana
(Isaya 1:19, Kumbukumbu la Torati 28: 1-13).
➡Kukosekana kwa utii huleta laana (Kumbukumbu la Torati 28:
15-68).
➡ Kwahiyo ukitaka kutembea pamoja na Mungu, unahitaji roho ya
utii wa hali ya juu na kutambua kuwa yeye ni boss na hivyo unatakiwa kumtii
badala ya kusimamia misimamo yako. Tii anachokuambia kila wakati, ndio mtaenda
pamoja.
*8. LAZIMA
USHUGHULIKIE ROHO YA MAZOEA KWA MUNGU WAKO.*
➡Hiki ni kitu muhimu sana sana, kwasababu kadri unavyozidi
kuwa karibu nae ni rahisi ukaanza kumzoea.
➡Hata kwenye maisha ya kawaida, kadri unavyozidi kuwa karibu
zaidi na mtu ni rahisi ukajikuta heshima yako kwake inapungua, na unaanza
kumuona ni wa kawaida sana.Hili jambo lilimgarimu Nabii Musa.
➡ Angalia watu wengi ambao wameokoka, kadri wanavyozidi kukaa
kwenye wokovu, wanajikuta wameanza kutembea kwenye wokovu kwa mazoea.
➡ Pia angalia watumishi wengi (waimbaji, Wahubiri n.k,
utagundua kuwa kadri wanavyozidi kutumika ndipo wanapoanza kutumika kwa mazoea
na kutumia uzoefu wao badala ya kumtegea Roho Mtakatifu.
*9. LAZIMA
UAMUE KUICHUKIA DUNIA NA MAMBO YAKE MAOVU.*
➡Ukitaka kuambatana na Mungu kwenye maisha yako ni lazima
uamue kuyachukia mambo maovu ya dunia hii (Yakobo 4:4).
➡Mungu anachukia sana sana dhambi, ndio maana pamoja na
kwamba Daudi alimpenda sana na alikuwa rafiki yake, lakini alipofanya zinaa na
mke wa mtu alimkasirikia sana na hakumuacha bila adhabu.
*10.
LAZIMA UWE TAYARI KUBEBA LAWAMA KUTOKA KWA WANADAMU NA KUKATALIWA NA
KUDHARAULIWA WAKATI MWINGINE.*
➡Ukitaka kumpendeza Mungu na kutembea pamoja nae, ni lazima
utambue kuwa muda mwingi wanadamu watakupinga sana, na utakataliwa na watu
ambao wakati mwingine haukuwategemea.
➡ Ndio maana watu wengine wakiokoka wanatengwa na ndugu zao,
wengine wanaacha kusaidiwa na ndugu zao.
➡Unaweza ukakataliwa na kusemwa vibaya na wazazi wako,
mke/mume wako, rafiki zako, watumishi wenzako, wafanyakazi wenzako n.k.
Yesu
mwenyewe alipokuja duniani kufanya mapenzi ya Baba yake, alikataliwa na ndugu
zake kabisa (Yohana 1:11).
➡Kwahiyo maeneo mengine ukikataliwa na kusemwa vibaya,
usikasirike sana na kuharibu uhusiano wako na Mungu, kwasababu hata Mwokozi
wetu Yesu alifanyiwa hivyo. Mtume Paulo alikataliwa, Daudi alikataliwa, Yusufu
alikataliwa n.k
➡Jambo la muhimu kwako, ni kuendelea kusimama pamoja na Mungu
wako na Imani yako. Shetani huwa anatumia watu ili kuharibu uhusiano wako na
Mungu wako.
Bwana Yesu
akubariki na azidi kukuongoza katika maisha yako,na ninaamini hili somo
litakupa hatua mpya.
*ZINGATIA*:
Ni vigumu sana ukayaweza mambo yote hayo kwa wakati mmoja,hivyo anza taratibu,
jambo moja baada ya jingine. Mtegemee zaidi Roho Mtakatifu ili akusaidie
kutembea kwenye hizo kanuni. Tamani sana awe rafiki yako na mshauri wako wa
karibu.
🔹Washirikishe
watu wengine mafundisho haya.
*Na Mwl M,
Mwambeso*
0752
197065, 0784 136 816
Email:
mwambeso80@gmail.com
No comments:
Post a Comment