Saturday, February 24, 2018

SEHEMU YA PILI
TAFSIRI KUHUSU WANA WA MUNGU
NA BINTI ZA WANADAMU (MW.6:1-4)

UTANGULIZI

Katika sehemu ya kwanza, nilitambulisha kambi mbili kuu za nadharia zinazokinzana kuhusu “wana wa Mungu” walioatajwa katika Mw.6:1-4 ni akina nani. Kambi moja inafundisha ni “malaika wa Mungu” walioasi kwa kuoana na binadamu na kuzaa watoto wa kinefili. Kambi ya pili inafundisha “wana wa Mungu” ni uzao wa Sethi” ambao walikengeuka na kuoana na binti za wanadamu wa “ukoo wa Kaini.”

Katika uchambuzi wa awali nilipingana na “nadharia ya malaika kuoana na binadamu”. Leo nawasilisha uchambuzi wa unaoangukia katika tafsiri ya pili inayofundisha kwamba “wana wa Mungu” sio malaika bali ni binadamu. Nitaanza kwa kuelezea chimbuko la historia ya ukoo wa uzao wa nyoka; pili chimbuko la historia ya ukoo wa “wana wa Mungu”, na tatu nitachambua kuhusu Mkengeuko Wa Maadili Ya Ndoa Kwa “Wana Wa Mungu” Kuoana Na Wasioamini. Karibuni:

1. Chimbuko La Historia Ya Ukoo Wa “Uzao Wa Nyoka”

Katika Mw.3:15 tunasoma ya kuwa Mungu mwenyewe ndiye alitabiri aina 2 tofauti za uzao pale alipotaja kuhusu “uadui” kati ya Uzao wa nyoka" na "uzao wa Mwanamke" (MW.3:15) Kutokana na “tamko la uadui” likawa ndilo chimbuko la “wana wa Mungu” na “binti za wanadamu” katika Mw.6:1-4.

Tukisoma katika Mwanzo Sura za 4 na 5 tunakuta ushahidi wa kihistoria ya watoto wa kwanza  kiume wa Adamu, Kaini na Habili. Humo tunashuhudia jinsi ambavyo: “BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; lakini Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.” (Mw.4:4b-5) Baadaye tunamsoma Kaini anamwua Habili mdogo wake na kulaaniwa na Mungu: “Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;…” (Mw.4:11) Kuanzia hapo Kaini akawa ndio mwasisi wa “uzao wa nyoka”!

Kwa kupitia uzao wa Kaini tupata orodha ya watoto wake kuanzia Henoko, Iradi, Mehuyaeli, Methushaeli ambaye alimzaa Lameki. (Mw.17-18) Ni kwenye “ukoo wa uzao wa nyoka (Kaini) tunamkuta Lameki akianzisha utaratibu wa “ndoa za wake wengi”, kinyume cha maadili ya ndoa ya mke mmoja tangu Adamu na Hawa. (Mw.4:19)

Ushahidi mwingine unaothibitisha ya kuwa Kaini ndio “uzao wa nyoka uliolaaniwa”, ni pale mjukuu wake Lameki alipotoa kiapo hasi cha kuendeleza visasi vya mauaji kama babu yake: “ ….enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; kijana kwa kunichubua; kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba, hakika Lameki atalipiwa kisasi mara sabini na saba.” (Mw.4:23-24)

2. Chimbuko La Historia Ya Ukoo Wa “Wana Wa Mungu”

Baada ya ukoo wa “uzao wa nyoka” kupitia Kaini kuongezeka, tunamkuta Adamu amepata mtoto mwingine wa kiume akamwita jina lake Sethi. Sethi naye akamzaa Enoshi ambapo tusoma ya kuwa ndipo watu walipoanza kuliitia jina la BWANA.” (Mw.4:25-26)

Kwa mantiki hii, Sethi akawa ndiye baba wa ukoo wa “wana wa Mungu”! Ukoo wenyewe umeanishwa kwa kirefu katika Mwanzo 5:5-32 ukianzia kwa Sethi, Enoshi, Kenani, Mahalaleli, Yaredi, Henoko, Methusela, Lameki (si yule wa Kaini).

Ushahidi mwingine unaothibitisha ya kuwa “wana wa Mungu” ni “uzao wa Sethi” ni Nuhu ambaye ndiye aliyeonekana mtu wa haki wa kuendeleza ukoo safi wa wana wa Mungu baada ya hukumu ya Gharika: “Nuhu akapata neema machoni pa BWANA….Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.”(Mw.6:8-9)

3. Mkengeuko Wa Maadili Ya Ndoa Kwa “Wana Wa Mungu” Kuoana Na Wasioamini

Sasa tuje kwenye kiini cha mjadala wa kisa cha Mw.6:1-4. Ushahidi wa kimaandiko katika kisa hiki unaonesha chimbuko la uharibifu sio “ndoa za malaika na binadamu” kama ilivyo kwa mtazamo wa nadharia husika.

Kiini cha mgogoro hapa ni “mkengeuko wa maadili ya ndoa” uliosababishwa na “Ukoo wa Sethi” ambao ndio “wana wa Mungu’ kuoana na binti za ukoo wa Kaini ambao hawakupaswa kuchangamana kifamilia. Mungu alikasirishwa na ukengeufu huu wa wana wa Sethi kuamua “kujitwalia wake waliowataka” kutoka ukoo wa Kaini na kuzaa nao watoto. Lakini sio hilo tu bali walivuka mipaka kwa kuacha utaratibu ndoa ya mke mmoja kwenda ndoa za wake wengi: “wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.” (Mw.6:2)

Msamiati wa neno “kujitwalia wake" kwa kiebrania ni laqah ukimaanisha “muungano wa kindoa” au “kujipatia mke”. Msamiati huo huo umetumika pia kwa “kujitwalia wake” kwa njia ya kuvunja maadili ya kimungu ya ndoa ya mke mmoja(Mw.2:23-24;MT.19:4-5) kwenda “ndoa za wake wengi” kama alivyofanya mjukuu wa Kaini:

“Lameki akajitwalia wake wawili, jina la kwa kwanza ni Ada, na jina la pili ni Sila.” (Mw.4:19) Hii ndiyo iliyomkasirisha Mungu kiasi cha kufupisha “kiwango cha ukomo wa kuishi”(Mw.6:3) duniani; na kisha kufutilia mbali kizazi chote cha binadamu na viumbe hai wote dunia nzima. (Mw.6:5-7)

Mpango wa Mungu tangu mwanzo ni kutunza ukoo safi wa uzao wa mwanamke ambao ungemzaa Yesu Kristo awe mkombozi wa ulimwengu. Ibilisi akamponda “adamu kisigino cha uasi” kwa kumwingia mzaliwa wa kwanza Kaini akalaaniwa. Ukoo wa Sethi ndio uliotegemewa  kumleta mkombozi lakini nao pia ukaingiliwa na kukengeuka. Kwa neema akapatikana Nuhu na uzao wake.

Hata baada ya gharika tunaona Mungu aliendeleza msimamo wake mkali kwa “wana wa Mungu” wa kutokuingiliana kindoa na mataifa yenye kuamini miungu mingine: “Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita ukaila sadaka yake. Ukawaoza wana wako binti zao, na binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.” (Kut.34:15-16)

“…..usifanye agano nao, wala kuwahurumia, wala usioane nao; binti yako usimpe mwanawe mume, na wala usimtwalie mwano mume binti yake. Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya BWANA juu yenu, naye atakuangamiza upesi..” (Kumb.7:2-4)

UFAFANUZI WA NYONGEZA KUHUSU
NDOA ZA MALAIKA NA BINADAMU

Kwenye makala iliyopita, baadhi ya wasomaji ninaowaheshimu sana waliuliza maswali kuhusu uhalali wa maelezo yangu ya kutokukubaliana na nadharia ya “wana wa Mungu” kuwa sio malaika. Walitaka kujua msamiati wa kiebrania wa “wana wa Mungu” unasemaje kama hauna maana ya malaika wa Mungu kuwa ndio wana wa Mungu. Na wengine wametaka kujua chimbuko la wanefili.

Naomba kuongeza ufafanuzi wa nyongeza katika kujibu maswali yaliyokwisha kuulizwa kama ifuatavyo: Tafsiri ya kiebrania ya “wana wa Mungu” ni bene ha'elohim. Katika Agano la Kale msamiati huu unapatikana sehemu kuu mbili kwenye Agano la kale. Ayu 6:1 na Ayub 2:1. Kwenye Ayu38:7 neno “ha” halipo. Katika sehemu hizo mbili tafsiri ya bene ha’elohim (wana wa Mungu) lilitumika kwa kwa malaika na mahali pengine kwa binadamu pia. (Hos.2:1; Kumb.14:1)

Lakini ukiuchunguza kwa makini muktadha wa maandiko ya kitabu cha Mwanzo utakuta hakuna mahali popote ambapo nadharia hii ya “wana wa Mungu” kuwa ni “malaika wa Mungu” imetajwa. Iwe ni katika Mwanzo au katika vitabu vyote vya Musa vya Kutoka, Hesabu, Walawi, na  Kumbukumbu la Torati. Kwa maelezo mengine hii ni tafsiri ya kuazima kutoka kwenye vyanzo vingine ambavyo matumizi ya misamiati yake nayo haina uhusiano na tukio la ndoa zinazodaiwa kuwa za malaika na binadamu katika Mw.6:1-4)

Kana kwamba hii haikutosha, kuna uthibitisho wa kitafiti kwamba nadharia ya “malaika kuoana na binadamu” ilipata nguvu zaidi kutoka chanzo kingine cha taarifa cha “Kitabu cha Henoko” ambacho ndicho kimesimulia habari za ndoa za malaika kuacha enzi yao na kujitwalia wake za kibinandamu na kuzalisha watoto wa kinefili. Kitabu hicho kilitumiwa sana na baadhi ya wakristo maarufu wa karne za kwanza waliovutwa na taarifa zake wakiwemo akina Tertullian, Irenaeus, Origen, na Clement wa Alexandria.

Lakini baadaye Kitabu cha Henoko kilikataliwa kuingizwa kwenye orodha ya maandiko matakatifu ya Agano la Kale. Mojawapo ya sababu za kukataliwa ni paamoja na ukweli kwamba kitabu cha Henoko hakikuandikwa na Henoko mwenyewe. Hata hivyo baadhi ya wanazuoni wa tafsiri ya maandiko ya Kale waliendelea kutumia nukuu za kitabu hicho katika kutafsiri maandiko matakatifu.

CHUMBUKO LA WANEFILI

Watu wengi wameuliza maswali kuhusu wanefili ni akina nani na walitokea wapi! Katika sehemu ya kwanza nilijibu kwa sehemu ya kwamba, wanefili sio uzao wa kinachodaiwa ni mwingiliano wa kingono kati ya malaika na binadamu.

Jina la “wanefili” hali maana moja ya “majitu”. Pia kuna maneno tofauti ya kiebrania yenye tafsiri ya Wanefili.  Kuna neno “naphal” likimaanisha “kuwashukia wengine” au “wenye kushambulia wengine” katika Yos 11:7; Ayu.1:15 na Yer.46:16.  Neno la pili ni “palah” likiwa na maana “watu wasio wa kawaida” (extraordinary) Hii inamtaja mfalme mwenye nguvu nyingi mno za kuharibu kiasi cha kustaajabisha watu…(Dan.8:23-24)

Lakini pia wanefili lilitumika kwa binadamu wenye maumbile makubwa kama Goliati (1 Sa.17:4; 21:19-20) Sehemu nyingine ambapo tunasoma habari za wanefili ni wana wa Anaki katika Hes.13:22,28,33).

Jambo  la kuzingatia hapa ni kuwa chimbuko la wanefili sio uzao wa ndoa za malaika na binadamu.  Ni jamii ya watu waliotokana na uzao wa binadamu. Sasa kama hawa wanefili wa Wana wa Anaki walizaliwa na binadamu aliyeitwa Anaki, hali kadhalika na wanefili wa Mw 6:4. Nao walizaliwa na wana wa ukoo wa Kaini, na hasa kwa tabia yao ya ukatili wa kushambulia binadamu wengine katika jamii za wakati huo.

Pia kuna tofauti kati ya “wanefili” na “wana wa waliozaliwa kutokana na ndoa haramu za kibinadamu ambao wanaitwa “watu waliokuwa hodari na wenye sifa.”

Najua ya kwamba uchambuzi huu ni mgumu kwa baadhi. Nitakuwa tayari kujibu maswali yoyote yatakayoulizwa kutoka na uchambuzi wangu. Nitafurahi pia kupata maoni yako. Ubarikiwe sana.

Na askofu Sylvester Gamanywa

Thursday, February 15, 2018

Somo: UPONYAJI WA NAFSI ILIYOUMIZWA.

Mnenaji: Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila.

Tukio: Semina Maalum ya Wadada

Tarehe: 14/02/2016

Utangulizi

⚡Nafsi imegawanyika katika sehem kuu tatu.
1)Hisia (Emotions & Feelings)
2)Maamuzi na machaguo (choices and decisions)
3)Akili (Intellect part)

Na katika somo hili tunajifunza kuhusu hisia.

1)HISIA
Hisia zipo ndani ya mtu tayari na zinaamka zikipata reaction kutoka nje.
Kuna aina mbili za hisia
a) Positive feelings
mfano: furaha, amani, kushangilia nk
b) Negative feelings
mfano: kulia, huzuni, uchungu nk

Vyote hivi vipo ndani ya mtu tayari lakini hadi vipate reaction kutoka nje ndio vitaonekana.

Hisia zinatokana na taarifa kutoka kwenye milango mitano ya ufahamu.

Yaani: Hata Mungu aliyetuumba sisi kwa sura na mfano wake ana hisia hizi za aina mbili:
i)Hasi
Mfano: "Hasira ya Bwana ikawaka"
Au "Mimi ni Mungu mwenye wivu"
Ama
"Wala msimhuzunishe Roho mtakatifu"
Hizi hisia hata Baba yetu anazo lakini anajua namna ya kuzicontrol!

ii) Chanya
"Mungu ni pendo"
Au
"Furaha ya Bwana ni nguvu yetu" ikiwa na maana anafurahi pia.

Lakini anajua namna ya kuzitawala hisia zake.

Hivyo basi, si tatizo kuwa na hisia chanya.
Bali hisia hasi usipojua namna ya kuzitawala na kuzimilki zitakuharibia maisha na watu wengine wanaokuzunguka.

Kumbuka: Hauwezi kuomba ili hasira isiweko kabisa ndani yako, ila unaweza kuomba "hasira isikutawale" (Waefeso 4:26).
Na ni wajibu wako kumnyima nafasi Ibilisi kukulisha taarifa mbaya na kukujeruhi ili kuamsha "hisia hasi" ndani yako ili ufanye dhambi na matukio mabaya!

Jambo jingine la muhimu kujua:

Vichocheo vinavyoamsha hisia hasi (hasira, uchungu, majeraha ya nafsi, visasi) yanakuja kupitia MILANGO MITANO YA FAHAMU.
Unachoona
Unachosikia
Unachogusa/hisi
Unachonusa
Unacholamba
Kama si kizuri, HISIA HASI zitaamka ndani yako na unaweza kufanya mambo ya ajabu.
Jiandae, uko duniani, utaona mengi mabaya ya kuumiza, utasikia taarifa mbaya, utahisi, utagusa na hata kunusa vitu vinavyokera na kuboa.
Mwitikio wako ndio utakaoamua nini utafanya na nini kitajengeka ndani yako.
Ili kushinda hisia mbaya, na majeraha ya nafsi tunapaswa tujue kanuni za Kibiblia za kutawala milango yetu mitano ya fahamu na kila kinachoingia ndani yetu kupitia hiyo!

kwahyo ili tuweze kujicontrol kwenye negative feelings zisituaffect maisha yetu na kuona hatuna sababu yoyote ya kuishi kwasababu ya tarifa uliyosikia au kuona ikaaamsha hisia zako tunapaswa kuwa na taarifa nyingi za neno la Mungu ili ziweze kubadilisha mazingira ya nje.
Hasira, Wivu, huzuni, uchungu vyote hivi vinapaswa viwe controlled na neno la Mungu.
Mungu akusaidie kutembea juu ya kila changamoto kutokana na wingi wa neno lililojaa ndani yako na lenye uvuvio wa Roho Mtakatifu..

❤❤ vitu viwili vinavyokaa karibu na moyo wa mtu
a) Yesu (neno)
Ufunuo 3:20 msaada ambao upo muda wowote.
ukimkataa Shetani then umemkubali Yesu

b) Dhambi
Mwanzo 4:7
ukimkubali shetani then umemkataa Yesu.

Yesu yuko karibu na moyo wako kwa mujibu wa Ufunuo 3:20, akisubiri umpe nafasi akusaidie.

Lakini pia dhambi iko mlangoni kwa moyo wako ikisubiri uliache Neno na agizo la Mungu iingie ndani yako.
Kama ilivyokuwa kwa Kaini (Mwanzo 4:7-8)

Ni wajibu wako kuruhusu nini kiingie na kipi kisiingie MOYONI MWAKO hasa UNAPOPATA TAARIFA MBAYA kutoka kwenye mazingira yako, watu wako, ndugu, mme, mke, watoto, biashara yako nakadhalika.

Ayubu alipopata TAARIFA MBAYA kuhusu wanae, mifugo, mali zake na hata afya yake, HAKUTENDA DHAMBI WALA KUMUWAZIA MUNGU KWA UPUMBAVU (Ayubu 1:22).

Alijua namna ya KUKABILI TAARIFA KUTOKA NJE.

Biblia inasema alichofanya ni "KUMSIFU MUNGU" akisema "JINA LA BWANA LIBARIKIWE"

Ni wajibu wako kujipanga kwa Neno, kwa kumuomba Mungu, na kupata nguvu ya kukabili kila HABARI MBAYA.

"Mwenye haki HATAOGOPA HABARI MBAYA, MOYO WAKE UIMARA UKIMTUMAINI BWANA"
(Zaburi 112:6-7).
Kadri ambavyo UNAKABIDHI MOYO WAKO KWA BWANA... UNA UHAKIKA WA KUTOTETEREKA HABARI MBAYA NA MABAYA YAKITOKEA.

Lakini kadri unavyokuwa unaombea vitu na maisha yako (unavikabidhi kwa Bwana kama Ayubu alivyokuwa akifanya ibada kwa ajili ya wanae na kuwatolea sadaka), unajikuta UNAJUA MUNGU YUKO KAZINI, BILA KUJALI NINI KINAKUTOKEA!

Waebrania 5:7 " Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule,awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu."
hapa tunaona Yesu pia alilia.
wanawake na mabinti wengi huwa tukiumia ni wepesi sana kulia...
Yaan haijalishi umeumizwa kiasi gani usiseme siwezi kuomba nooooo nenda mbele za Mungu kwa machozi na kulia Mungu anasikia aisee.
Stephano pia alilia.

1 Peter 5:7
" huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
⚡Mungu anajishughulisha sana kwa mambo yetu sio mambo yake ni yetu kwahyo kazi yetu ni kumtika yeye fadhaa zetu zote
Fadhaa ni chochote cha huzuni, kusikitisha, kinachochukua amani yako, kinachokufanya usifurahiw maisha na kisichokupa raha nafsini mwako.
Mwambie Mungu fulani (mtaje jina) amekuwa mwiba kwangu.
ongea na Mungu mwambie fadhaa zako zote

Mathayo 11:28
kuna vitu vwili ambavyo vipo hapo
a) Mungu hataki mtu asumbuke yaani unapaswa uishi maisha ya raha, luxurious life
b) Mungu hataki ulemewe. Mwambie hilo linalokulemea kwamba umejaribu peke yako umeshindwa.

Yakobo 5:12 inasema, "Je mtu wa kwenu amepatwa na mabaya? AOMBE. Ana moyo wa kuchangamka na AIMBE ZABURI"

Hii ina maana siku unazokutana na taarifa mbaya au matukio mabaya... BREKI YA KWANZA NI KWA BWANA KUMUELEZA KWA UWAZI NA BILA KIFICHO... UNAVYOJISIKIA... ULIVYOUMIA... KAMA NI KULIA LIA KWELI... KAMA NI KUSHTAKI SHTAKI SANA TU... Lakini hakikisha unatumia TAARIFA MBAYA KAMA MWALIKO WA KUOMBA... Ibilisi hatakuumiza kamwe wala kukuua kama wengine.
Unapoomba, kusali na kushukuru, AMANI YA MUNGU ITAKUFUNIKA NA KUPONYA "MOYO WAKO NA NAFSI YAKO (NIA YAKO)" (Wafilipi 4:6-7).
Na moyo na nafsi zetu kumbe zinaponywa na KUOMBA, KUSALI NA KUMSHUKURU MUNGU badala ya kumlaumu au kulaumu watu au matukio.

Kama tukio limetokea na bado HALIJAKUATHIRI SANA NA KUKUONDOLEA UCHANGAMFU... Huo ni muda mzuri wa KUIMBA ZABURI (Kuanza kumsifu na kumuabudu Mungu)!
Kuna nguvu katika kuabudu na kumsifu Mungu katikati ya jaribu na changamoto.
Paulo na Sila gerezani walisifu na kumuabudu Mungu MILANGO YA GEREZA IKAFUNGUKA KWA UPAKO ULIOSHUKA JUU YAO.
Nakuona ukimsifu na kumuabudu Mungu badala ya kulia na kuomboleza kila hali na taarifa mbaya zijapo na ninamuona Mungu akikuvusha kwenye kila jaribu, pito na gereza katika jina la Yesu!

⚡2 Wakorintho 4:18" tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana, kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele."

chochote kile ambacho kinaonekana au kimeshaokea kwenye mazingira ya nje tayari ni cha muda maadam tu kinaonekana basi ni cha muda tu sio cha kudumu.
Hivyo haijalishi umefanyiwa kitu gani kikaamsha negative hisia ndani yako( uchungu, huzuni, masikitiko, kukosa amani) maadam tu kinaonekana basi ni cha muda tu yaani lazima kitaondoka.
Hapa Biblia inasema tusitazame vinavyoonekana bali tutazame visivyoonekana.
Na visivyo oonekana vinahitaji imani yaani unaangalia vitu jinsi ambavyo neno la Mungu linasema.

🔒Yote yaliyosikiwa au yaliyoonekana haijalishi yamebeba ujumbe gani mbaya kiasi gani hayo ni ya muda tu kwasababu yameshaonekana.

🎄unapopata zuri lolote kwenye maisha yako ni muda wa weww kutoa muda wako mwingi sana kukiatamia kwenye maombi.
Next levels New devils.
kwa kadiri unavyopata mafanikio na mazuri ndivyo ambavyo na shetani anazidi kukukarbia ili apate nafasi,  na mara nyingi  sana tunajisahau tunapopata yale tuliyoyategemea.
💊 ukiona kitu kizuri kimetokea kwenye maisha yako ndio muda wa kuomba kuliko kawaida.
" Udhanipo kuna amani ndipo uharibifu huja"

1 wakorintho 16:9 " kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wapo wengi wanipingao"

kwahyo jua kwamba kwenye kila mlango mkubwa uliofunguliwa kwako wapo wengi(hawana idadi) wakupingao.
Ufunuo 12:13-16
Ufunuo 12:4b "na yule joka akasimama mbele za yule mwanamke aliye tayari kuzaaa,ili azaapo amle mtoto wake"

unaona huyu mwanamke anategemea kupata mtoto yaani taarifa njema, lakini yule joka anasubiri azae tu ili amle mtoto wake.

Chochote ambacho unatamani kukizaa kiatamie kwenye maombi ili shetani asikile kwenye elimu yako, kazi yako, ndoa yako, huduma yako, biashara yako nakadhalika.

Ufunuo 12:4 inasema "Ibilisi (joka) alikuwa amesimama mbele ya mwanamke mwenye mimba anayetaka kuzaa ili amle mwanae akimzaa"
Hii ina maana kuna vita kati yako na Ibilisi isiyokoma.
Unapoomba muujiza usifikiri Shetani anakuchekea, anasubiri uje huo muujiza auharibu kabla hujaufaidi!
Angalia "mwanamke anafurahia kuwa anakwenda kuzaa mtoto" asijue Ibilisi yuko hapo karibu anasubiri kuumeza huo muujiza.
Ndio maana watu wanaomba wanapata waume, halafu ndoa (mtoto aliyezaliwa) inakuwa mbovu na inavunjika.
Mtu anaomba kazi, akifika kazini kazi inakuwa uwanja wa vita na anaweza kuamua kuacha (mtoto ameliwa na joka)!
Daka hii:
"Kila muujiza unaotaka kuuzaa Ibilisi anausubiria ili aule"
Ndio maana WATU WANAANZISHA VITU VINAKUFA.
Biashara unaanza vizuri na una uhakika unakwenda kutoka, INALIWA NA JOKA.
Hii ni sababu ya kukufanya UDUMU KUOMBA MPAKA YESU ANARUDI.
HAKUNA BREKI YA MAOMBI RAFIKI YANGU kama unataka vitu vizaliwe!

1Wakorintho 16:9 inasema "Nimefunguliwa mlango mkubwa na wa kufaa sana lakini wako wengi wazuiao/ wanipingao"

Hii ina maana kila ukiona mpenyo, kitu fulani kimetokea, umepata mme, mke, baraka, huduma imekua, umepata mtoto... JIANDAE, KUZIMU NZIMA ITAAMKA KUJARIBU KUUA HUO MLANGO MZURI WA KUFAA.
Ni wajibu wako KUKESHA UKIOMBA ILI MWIZI AJAPO ASIINGIE KWAKO!
UAMUZI NI WAKO.

Unawajibika kuamua ni aina gani ya mawazo uyaruhusu yatawale maisha yako either positively au negatively.
2 Wakorintho 10:3-5
Jinsi ya mwili ni kuangalia vitu vinavyoonekana au taarifa zinasemaje. Yatupasa tuamue kutoka ndani sawasawa na neno lililopo moyoni ili tuwrxe kureact na taarifa mbaya ambazo tunaziona nje
Ni wajibu wako kutiisha kila wazo lako.
Matendo 5:1-11
Waefeso 4:26-27
Yakobo 5:13  -- upatwapo na baya lolote cha kwanza kufanya ***OMBA***
Wafilipi 4:6-7.

cha mwisho pima mawazo yako.
Zaburi 19:14

na ukisoma Wafilipi 4:8 inatufundisha yapi ya kutafakari
1)Yaliyo ya kweli
2)Yaliyo ya staha/ sitirika, bila uchafu
3)Yaliyo ya haki
4)Yaliyo safi
5) Yenye kupendeza
6)Yenye sifa njema
7) Yenye wema wowote
8)Yenye sifa yoyote nzuri
Chochote utakachokitafakari nje ya hzi point nane basi  achana nalo lisikuumize kichwa.

Waza na kutafakari aina hizi tu za mawazo.
Mengine nje ya hapo yaangushe na kuyapangua kwa jina la Yesu!

Mwisho kabisa, ni mapenzi ya Mungu tuwe na furaha kila saa ,sekunde, dakika na kila wakati.

Isaya 12:3
"Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu"

Mungu anahitaji furaha yako ili umwabudu.

Isaya 55:12
 "Maana mtatoka kwa furaha, mtaongozwa kwa amani ....mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo (hali ngumu zinazozuia wengine kwenu zitakuwa fursa), na miti ya kondeni (wanadamu) itawapigia makofi (watawacelebrate)"

Yohana 16:23-24
 "....... hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu iwe timilifu"

Kusudi la Mungu kukujibu maombi yako ni ili ufurahi.

Yesu anawajibika na furaha yako yaani yupo comitted kuhakikisha kila muda unafurahi (Wafilipi 4:4).
Ndiyo maana hakufia dhambi tu msalabani bali pia "HAKIKA AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU, AMEJITWIKA HUZUNI ZETU" (Isaya 53:4).

Kwa hiyo maombi ni opportunity ya kukufanya ufurahi.

Hesabu 23:19
"Mungu si mtu , aseme uongo.....
so ikiwa Mungu amesena na umeona kwenye neno lake lazima atimize"

Nikutakie uanafunzi mzuri.
Urudie na kurudia na kurudia na kisha UYATENDE MOJA BAADA YA JINGINE, mpaka utakapokuwa MASTER WA HISIA ZAKO!
Mwl D.C.K
www.yesunibwana.org
(Tembelea hii website kila mara kukua kiroho)!

KWANINI MIMI NINAABUDU SIKU YA JUMAPILI?

Baada ya kusoma majadiliano mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malumbano ya siku gani ni halali ya kusali katika Biblia, kwamba ni Jumapili au Jumamosi; Kwa faida ya wasomaji wangu katika ukurasa huu ambao wamekuwa wakiomba nitoe maoni kuhusu ipi siku ni halali, leo nimeona kujibu maombi yao kwa kuwasilisha makala haya huku nikitoa sababu zangu 5 kama hizi zifuatazo:

I.YESU KRISTO ALIFUFUKA SIKU YA JUMAPILI

Katika historia ya kibiblia; tendo la Yesu kufufuka siku ya Jumapili lilifungua ukurasa mpya wa Agano Jipya. Maandiko ya Injili yanathibitisha ya kwamba Yesu alifufuka siku ya kwanza ya juma, ambayo ni Jumapili. (Mk 16:9; Lk 24:1,13,21)

Pamoja na kwamba kifo cha Yesu ndicho kilitengeneza wokovu wetu, lakini kufufuka kwa Yesu ndiko kunakotupa nguvu za kushangilia na kuabudu kwa shangwe. Ibada iliyo hai imejengwa juu ya kufufuka kwa Yesu Kristo.

II.YESU ALIWASILISHA MBINGUNI DHABIHU YA DAMU YAKE SIKU YA JUMAPILI

Tukio jingine la kihistoria ambalo lilibadilisha mfumo mzima wa kiibada ni pale ambapo Yesu alisema anapaa kwenda kwa Baba na Mungu wake.

Yesu alipomtaja Baba kwa jina la Mungu alisema hivyo akiwa ndiye Kuhani mkuu mpya wa Agano Jipya ambaye alitakiwa kupeleka damu yake mwenyewe kwenye Kiti cha Rehema mbinguni ili kukamilisha dhabihu ya Agano jipya.

Yesu alisema maneno haya baada ya kumkatalia Mariamu asimguse kwanza mpaka atimilize zoezi ya kuwasilisha dhahibu ya damu yake mbele za Mungu Baba yake:

“Yesu akamwambia, usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawambie ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, na Mungu wangu naye ni Mungu wenu.” (YH.20:17)

Sasa siku ambayo Yesu aliifanya kazi hii ilikuwa ni Jumapili baada ya kufufuka kutoka katika wafu. Najuaje kwamba aliwasilisha dhahibu mbinguni siku ya Jumapili? Ushahidi wangu ni pale ambapo maandiko yenyewe yamekiri ya kwamba Yesu alipaa mbinguni siku ile ile kwenda mbinguni; na kwamba  alishuka dunia ile ile jumapili; na kuwatokea wanafunzi siku ile ile ya kwanza ya juma:

“Ikawa jioni, siku ile ya siku ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa sababu ya hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia amani iwe kwenu.” (YH.20:19)

III.ROHO MTAKATIFU ALISHUKA DUNIANI JUMAPILI

Tukio la tatu la kihistoria katika mambo ya kiibada kwa mujibu wa Agabno Jipya ni ujio wa Roho Mtakatifu duniani. Kutimia kwa ahadi ya Roho Mtakatifu siku ya Jumapili kuliifungua siku hiyo  kuwa ibada ya kwanza ya kuabudu Mungu katika roho na kweli kama Yesu alivyomtabiria mwanamke Msamaria kisimani (MDO.2:1-4)

“Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.” (YH.4:23)

Unaona? Huu ulikuwa ni mjadala wa mahali panapostahili kuabudia kama ni Hekaluni Yerusalemu au juu ya mlima wa Samaria. Yesu akatabiri za kuja kwa mabadiliko ya mtindo wa kuabudu, mazingira ya kuabudia na siku ya kuabudu. Siku ya ujio wa Roho Mtakatifu ambayo ni Jumapili ndipo mabadiliko ya kiibada yalifanyika kwa mara ya kwanza.

IV. KANISA LA KRISTO LILIZALIWA SIKU YA JUMAPILI

Huko nyuma mwanza wa huduma za Yesu aliwahi kutabiri akimwambia Petro ya kwamba:

“Nami nakwambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; na milango ya kuzimu haitalishinda.” (MT.16:18)

Kibiblia tunafahamu ya kwamba kanisa hili lilizaliwa siku ya Pentekoste kwa sababu injili ya kwanza ya mitume ilianza rasmi baada ya kumpokea Roho Mtakatifu kama Yesu alivyokuwa ameagiza.

Ni baada ya mitume na wakristo wengine jumla ya watu 120 walipojazwa Roho Mtakatifu na kusema kwa lugha nyingine Petro alihubiri na wakatubu na kubatizwa waamini wapya 3000. Hawa ndio mavuno ya kwanza yaliyozaa kanisa la kwanza.

Na mavuno haya yalipatikana siku ya Jumapili. Kwa maana imeandikwa na: Na siku ile…… ipi? Siku aliposhuka Roho Mtakatifu…. Siku gani? Jumapili!

V. KANISA LA KRISTO LILIKUTANA KIIBADA SIKU YA JUMAPILI

Kama ilivyo desturi, ibada yo yote inayo mambo au matendo ya kiibada ambayo huitambulisha kuwa hiyo kweli ni ibada. 

Kuna matendo mawili ya kiibada ambayo tunasoma kanisa lilifanya siku ya Jumapili. Tendo la kwanza ni Meza ya Bwana inaitwa siku ya kumega mkate (Mdo. 20:7)

 Na tendo la pili ni matoleo ya changizo na sadaka. Hakuna ubishi ya kwamba mojawapo ya tukio maarufu la kiibada ni utoaji.  Tunasoma ya kwamba kanisa la kwanza likikutana kiibada na kufanya matoleo (1 Kor.16:1-2

Kwangu miye, haya mambo makubwa, mazito ya kihistoria na kiibada ndiyo yananishawishi niamini na kujua ya kwamba Ibada za Agano Jipya ni siku ya kwanza ya Juma ambayo ndiyo jumapili.

Ndugu msomaji wangu. Ukurasa huu ni kwa ajili ya kuelimishana na si mahali pa malumbano na matusi.

Katika makala haya sitarajii kufanya malumbano ya wapinzani wa siku ya jumapili. Ila naomxa kutahadharisha mapema ya kwamba kama ukifanyika uchokozi wa aina yoyote mabishano au matusi, safari Hii nitalazimika kujibu majibu ya ukweli mzito na makali na hapo nisije kulaumiwa.

Kama umesoma post hii na imekubariki basi nijulishe kwa ku-like na pia warushie marafiki zako pia.


Silvester Gamanywa


ACHA KUKIMBIZANA NA"MANABII" ILI KUPATA "NENO KUTOKA KWA MUNGU" ANZA KUKIMBIZANA NA NENO THABITI ZAIDI LA KINABII.
Wapenzi nimesikia hili wazo likidondoka ndani yangu nilipokuwa najiandaa kulala na mara lilipodondoka nikaanza kutafakari jinsi watu wanavyokimbia huko huko ili eti "Kusikia neno toka kwa Bwana kwa ajili yao kupitia manabii."
Mimi binafsi nakubali kabisa kuwa manabii wapo hata leo ila nisichokubaliana nacho ni kwamba manabii wa Agano Jipya ni sawa na manabii wa Agano la Kale.

Katika Agano Jipya nabii ni mmojawapo kati ya zile huduma tano teule za Waefeso 4:11 na ni mojawapo ya huduma ongozi ndani ya kanisa sawa na na I Kor. 12: 28 na Matendo 13: 1 na pia mojawapo kati ya huduma mbili ziwekazo msingi wa kanisa sawasawa na Efeso 2: 20.
Nabii ni mfunuaji na mtafsiri wa siri na mafumbo ya Mungu kupitia kuhubiri na kufundisha kulikovuviwa.
Nabii huleta kwetu siri ya Ufunuo wa Kristo kupitia mahubiri na mafundisho.
Nabii anatuthibitisha katika kumjua Kristo kupitia mahubiri na mafundisho.
Huduma hii inavyofanya kazi katika Agano Jipya ni tofauti kabisa na ilivyokuwa inafanya kazi katika Agano la Kale.
Sababu kubwa ikiwa ni kwenye Agano Jipya kila amwaminiye ana uwezo wa kuisikia sauti Yake maana imeandikwa kondoo wangu waisikia sauti Yangu. Tena imeandikwa sehemu nyingine "hao rafiki Zako huisikia sauti yako" na Yesu anatuita sisi marafiki na sio watumwa kwa hiyo sote twaisikia sauti ya Mungu.

Pia Roho Mtakatifu anaifunua kwetu sauti ya Mungu maana anayatwaa yaliyo Yake na kuyafunua kwetu so mwamini hahitaji "Nabii" hapo anamhitaji Roho Mtakatifu.
Wakati kwenye Agano la Kale Bwana Mungu alikuwa hafanyi lolote pasipo kwanza kuwafunulia watumishi Wake manabii siri Zake katika Agano Jipya atakapokuja huyo Roho wa Kweli atatuongoza na kututia katika kweli yote na atatupasha moja kwa moja habari za mambo yajayo.
Agano la Kale Roho Mtakatifu alikuwa juu ya manabii, makuhani na Wafalme katika Agano Jipya yupo juu na ndani ya kila amwaminiye.

Nabii katika Agano Jipya ni mojawapo ya huduma tano teule ambaye hufanya kazi kwa kushirikiana na hizo huduma zingine ili kuukamilisha Mwili wa Kristo hata kazi ya huduma itendeke. Kwa mujibu wa Agano Jipya hamna kitu kama nabii aliye peke yake asiyeshirikiana na wenzake na ambaye badala ya kujenga Mwili wa Kristo anajenga jina lake na ufalme wake.

Nabii anahitaji kushirikiana na mitume, wainjilisti, wachunagaji na waalimu kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke na mwili wa Kristo Ujengwe. Huku akishirikiana na hizo huduma zingine atahakikisha sote tunafikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu na sio yeye nabii. Nabii wa kweli huliinua Jina la Yesu na sio la kwake. Humhubiri Kristo na sio yeye. Huutafuta Utukufu wa Kristo na sio wake.

Watoto wa Mungu wanahitaji kujua kuwa Mungu anatamani kujifunua kwao na kuzungumza nao kupitia neno Lake. Maana Mungu na Neno Lake ni Wamoja.
Mungu anataka tulisome neno Lake ili alifunue kwetu na tusikie sauti Yake na sio kukimbizana na manabi, matokeo yake tukaparamiana na manabii wa uwongo wanautupa maunabii ya uwongo na kututoza kila aina ya sadaka hatarishi kwa kazi ya Msalaba wa Yesu.
Mtu wa Mungu embu tubadilike na tuanze kuwa na kiu ya kweli na sio mbwembwe.
Tafakari niliyoandika na Bwana akakupe ufahamu katika mambo yote.


*WOKOVU UMETOLEWA KWA WOTE LAKINI JUHUDI YA KUMTAFTA MUNGU NI MTU BINAFSI*

Mwanzo 19 : 17 - Ikawa walipomtoa nje, *mmoja alisema, Jiponye nafsi yako* usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea.

Kama umeamua kuokoka amua kama wewe na nafsi yako ukiaza kutazama wa kanisani kwako wanasemaje watakupoteza maana  wengi makanisani ni wazugaji tu  wokovu ni safari ya wokovu inakuhusu wewe

Ukiangalia  wakati Lutu na familia yake walipataneema ya wokovu kama tulivopata Mimi na wewe  walikuwa wamepata Neema walikuwa *wanne* llakini malaika walipokuwa wakiwaokoa walisema neno la ajabu saana ambalo mama Lutu hakuelewa
Watu walikuwa wanne *lakini wao wakasema jiponye nafsi yako*

Walitumia umoja ili kuonyesha kuwa safari ya wokovu ni juhudi ya mtu binafsi

 Na walitambua kuwa yupo mwenyemoyo mgumu


Mwanzo 19:26 Pamoja na tahadhari yote lakini mkewe Lutu aligeuga nyuma akapotea kwa kugeuka kuwa nguzo ya chuvi

Mungu anapomuokoa mwadamu anamuokoa kwa kumhurumia na jehanamu ya moto wa milele ndivo alivowaokoa Lutu na familia yake

Mwazo 19:16 *Akakawiakawia nao wale watu wakamshika mkono na Mkono mkewe na mkono wa binti zake wawali ,kwa jinsi Bwana alivyowahurumia wakamtoa nje ya mji*

Angalia maneno hayo jinsi Mungu alivo wapenda Lutu na mkewe

Lakini mama Lutu  wakati akiwa njiani alipokumbuka mali alizozicha milio ya wanyama wake akageuka nyuma

Ndivo ilivo katika kanisa la leo watu hawapo tayari kuacha mali zisizo halali mtu ameokoka lakini anatoa ruswa ya Pesa au zinaa ili apate Kazi 

Watu wanacheza na dhambi kanisani 

WOKOVU NI KUJIKANA

WOKOVU NI KUKUBARI KUPITA ALIMOPITA YESU

WOKOVU NI MAPAMBANO


KAMA UMESHINDWA BAKI PEMBENI MAANA UTAITWA MLOKOLE LAKINI MBINGUNI HUINGII
😪😪😪



Mtumwa remmy mdesa


HATUNA UDHURU KATIKA KUSAMEHE

Mathayo 18:23-35
26 Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.
28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho.
29 Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
30 Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu.

Bwana Yesu alitoa mfano mfalme na watumwa wake ili iwe fundisho kwetu

Tumesamehewa kwa gharama ya damu ya Yesu-dhambi zetu zote si kubwa wala ndogo zimesamehewa na ndio maana tunaishi hata sasa kwa neema, wewe na mimi ni nani hata tusisamehe.

haijalishi tunaowapenda wametuumizaje, haijalishi ndugu zetu wamefanya nini hata tukaumia kiasi kiasi cha kutaman kufa kwasababu ya Yesu kufa msalaban kwaajili ya makosa nadhambi zetu ndugu yangu tunapaswa kusamehe

tunafundishwa kwa habari ya mtumwa na Bwana wao, mmoja alikua akidaiwa maden makubwa akamwomba bwana wake amvumilie angemlipa lakini yule bwana alimsamehe ile deni yote. sasa aliekua amesamehewa deni nayeye akawa anamdai mtu aliombwa amvumilie angelipwa lakini alikataa -hakumsamehe, ndivyo tulivyo wanadamu Mungu anatusamehe makosa yetu lakini sisi hatuwasamehi wale wanaotukosea.

Kiwango cha mabaya uliyofanyiwa ni kidogo kulinganishwa na wewe uliyoyatenda mbele za Mungu hata ukasamehewa, hivyo hauna udhuru wa kusamehe.

Ukisoma mstari wa 21 Petro anamuuliza Yesu nisamehe mara ngapi? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

Maana yake kila unapotembea inatakiwa usamehe, kila kosa wewe ni lakusamehe tu hauna udhuru wowote

Sababu kubwa inayofanya tusisamehe ni kwamba tumechukulia vile tulivyofanyiwa ni vikubwa na havipwi kusamehewa na pia ndani yetu upendo wa Ki-Mungu umeondoka, kwani ndani yako kukijaa upendo kusamehe inakua ni kazi rahisi.

Hivyo omba upendo wa Ki-Mungu ujae ndani yako ukifurika ndipo utaona wepesi katika kusamehe

Watazame kwa jicho la pili wote wanaokukwaza, waone kama wametumwa na adui kukukwaza ili wakutoe katika uwepo wa Mungu, wakutoe kwenye ushirika na Mungu hivyo usiwatazame wao bali tazama kilicho ndani yao ambacho kinawasukuma wakukwaze, ndio maana pia wanaokuudhi badae wanakuja kujuta kwa vile walivyokufanyia sababu si wao yupo alie ndani yao anaewasukuma.

Wengine mmejaziwa maneno yauzushi kuwa fulani kafanya hivi kumbe ni uongo tu ili wakuchonganishe na muhusika, sikia iwe ni kweli au uwongo wewe samehe tu, kumbuka tumeagizwa tuwasamehe wote waliotukwaza.siku zote kumbuka amri kuu ya pili aliyotupa Bwana Yesu mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwaakili zako zote na mpende jirani yako kama nafsi yako

Ukiwapenda watu hutawachukia watu utasamehe siku zote.

Mungu akubariki.
Kama umebarikiwa na ujumbe huu share kwa ndugu jamaa na rafiki zako popote pale facebook na kwenye magroup ya Whatsup hutaachwa hivyo hivyo bali utabarikiwa kwa kuitangaza injili kwa kushare. Pia like Facebook Page yetu ya Nyumba ya Sala kwa Mataifa Yote kwa masomo mengi zaidi.

Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu kila siku kwa Whatsup tuma majina yako mawili inbox, whatsup kwa namba ya Tigo 0657 048393 kuomba kuunganishwa kupewa masomo kila siku na utatumiwa, pia kwa ushauri na maombi piga namba zilizopo hapo chini, na  Mungu wambinguni akubariki sana.

Merito Tagalile
~0657 048393


UWEZA WA MUNGU.KATIKA MAISHA YA WAAMINI.

"Sauti ya mtu aliaye Nyikani,Itengenezeni njia ya Bwana,Yanyosheni Mapito yake.

Kila Bonde litajazwa na kila Mlima na kilima kitashushwa,palipo potoka patakuwa pamenyoka.

Na palipoparuza patalainishwa. Na wote wenye Mwili watauona Wokovu wa Mungu"

 ( Luka 3:4-6).

Mpenzi Rafiki Wa Mungu,Nakutakia Neema,Amani,Upendo Viwe Juu yako.

Nimatumain yangu na imani Yangu kwako kwamba Mungu ameendelea kujifunua na kujidhihirisha katika Maisha Yako. Nakuombea Ujazwe na Roho Mtakatifu. Ubadilishwe nia yako. Na matanio Yako kwa Mungu akujibu.

Naomba Roho Mtakatifu Akufundishe,Akushauuei na akuongoze Njia. Na akupe Nguvu. Kadiri Unavyozidi kuusoma ujumbe Moto Wa Roho Mtakatifu uwake ndani Yako. Usawazishe milima,Usawazishe Mabonde,Uondoe Na kuteketeza hila za ibilisi Maishan mwako. Amina.

Sasa turudi kwenye Somo. Letu. Somo La Leo Mwinjilist Yohana,Mbatizaji anatueleza uwezo Na nguvu za Mungu. Upitao Fahamu na akili za Wanadamu.

Mungu anaweza kutenda yasiyo wezekana kwa Wanadamu,Yasiyo elezeka kwa akili za Wanadamu.

Akili za Mwanadamu zinapoishia kufikiri,Zinapoishia kuwaza,Nguvu za Mwanadamu zinapoishia Ndipo Mungu Anapoanza Kufanya kazi. Ukisurender yote kwa Mungu ndipo utakapo uona ukuu wa Mungu maishani Mwako.

Mwinjilist huyu Wa KimataifaYohana Mbatizaji ,Anatuambia Ili Mungu aweze Kuporomosha milima Yetu. Lazima Tufanye kazi na kufuata kanuni na Sheria za Kiroho. Ambazo ni.

A. Kutengeneza Mapito Yetu. Ni kutengeneza Njia Ya Bwana.

Mfano Rais hawezi kwenda na msafara wake sehemu ambayo hakuna maandalizi,hakuna njia hakuna Usafiri. Au kunausafiri lakini maeneo hayo hayana usafi, Rais hawezi kuketisehemu hizo.

Ndivyo ilivyo Kwa Mungu wetu Yesu Kristo. Hawezi kupita sehemu Chagu,Sehemu isiyo na Maandalizi. Lazima Tutengeze uhusiano Wetu na Mungu,Lazima tutubu ,Tuache Njia zetu mbaya. Tumrudie Mungu kwa Toba na kuamini Uwepo Wake Mungu. Ndipo Miujiza itakapo tujia. Na kutufuata milele.

Baada ya kunwalika Yesu Kristo Maishani Mwetu. Uwepo Wa Mungu unaanza kututengeneza Sisi. Utaona hamu ya Dhambi inaondoka,Ufahamu unakujia,Uwepo wake Unakufunika,Uwepo Wake unakujaza nankukupa amani Ya ajabu. Palipo Mungu ,Palipo Roho Mtakatifu pana Uhuru maana hakutakuwa na milima,Hakuta kuwa na magonjwa,Shoda na mashaka. Hata kama utapiyia hayo utakuwa na amani ,furaha na mafanikio tele.

Hapa ndipo Penye Shida sana,Wengi tunapenda kuona Milima ,shida ,mateso,umaskini Ukiongezeka,magonjwa yakiondoka lakini Hatupendi Kufuata kanuni,hatupendi kulipa Gharama za kuondoa hiyo miujiza. Wengi tunapenda kuishi kwa Imani,Ila hatupendi kulipia gharama za Maisha hayo ya Imani. Ni kujikana,kufunga ,kuomba,kutoa sana tena kwa Wingi na kwa imani,Kukesha katika kusoma na kutafakari Neno la Mungu. Haya hatupendi kuyafuata.

Na Ndio Maana Tunafuatana Na kujaa katika Makanisa na.kwa manabii wa pokea ,pokea pokea kwa jina la yesu. Amka Acha Uvivu Muda wa Kulala umeisha

Mwisho Mwinjilist huyu Yohane Mbatizaji Anatuambia Na Wote Wenye Mwili hatauona Wokovu Wa Mungu.

Mara Nyingi Katika Shida pasipo Imani Huwezi kuuona thamni Ya Wokovu. Huwezi kujua raha ya kumtumaini Mungu. Huwezi Kuamini Kama Kumtegemea Yesu Kuna Raha sana. Ila Baada ya kuanza Kutumia imani Yako. Unaamuru Mvua Inasimama. Na wewe unapita ukifika Nyumbani Unaiamuru inyeshe na inanyesha.

Unanjaa nyumbani unaamuru Mungu akuletee unga maraa paap unaona Watu wanakuletea Pasipo kuwalazimisha. Hapo ndipo utakapo Msifu Mungu,utakapo muabudu Mungu. Ndipo utakapo pata Kulithibitisha neno La Nitakulisha Daima na kukushibisha kwa Miaka mingi.( Zab91:14-15)

Ushauri Wa Bure Naomba nikushauri Jambo Jifunze kutembea kwa Imani Yako binafsi,Jenga Mazoea ya Kujiombea ,na Kuwaombea Wengine daima. Weka ratiba za kulisoma neno kwa Mfululizo ,Soma vitabu Vingi vya kiroho na Vya kimaisha ili Kupata ufahamu Mpya,mawazo Mapya. Hakika hautakuwa vile ulivyo kuwa.

Mungu Akubariki,Mungu akuinue zaidi Na zaidi. Unapotumia Muda mwingi Katika Kumwadhimisha Yeye Aliye mtakatifu sana,Atukuzwe Mungu Baba,Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu Milele Na Milele.

Nakuomba Ombea Nchi Ya Tanzania,Ombea Watumishi Wa Mungu Duniani kote,Ombea Wachungaji,Wainjilist,Ombea Manabii,Mitume,Waimbaji wote.

Naomba kwa unyenyekevu Ombea Uchaguzi Wa Tanzania Wa Mwaka 2019/2020. Ombea Amani Iwepo,Ufahamu ukawafunike kw akila Mtanzania. Ombea Mungu Atuonyesha Kiongozi Anayestahili,sio Anaye stahili kwa Chama fulani.

Wenu Katika Utumishi wa Yesu Kristo.

Punda Wa Yesu Kristo.

Wednesday, February 14, 2018


GHARAMA YA KULIPA ILI UTEMBEE NA MUNGU (Somo Na Mwl M, Mwambeso)
🔹Watu wengi sana wanapenda kutembea na Mungu katika maisha yao, na hicho ni kitu kizuri sana, lakini ni watu wachache sana ambao wanaelewa gharama wanayotakiwa kulipa ili wafanikiwe katika jambo hilo.

🔸Mungu anapenda kuona watu wake wanatembea pamoja nae kama walivyofanya wakina Henoko, Ibrahimu, Daudi n.k, lakini ana kanuni zake ambazo watu wake wanatakiwa kutembea nazo kila wakati.

🔹Kanuni kubwa ni kufanya mapenzi ya yake (yaani mapenzi ya Mungu) katika maisha yako. Yesu alisema kwamba Baba yake alikuwa pamoja nae siku zote na wala hakumuacha kwasababu tu alikuwa anafanya yampendezayo (mapenzi ya Baba yake), Yohana 8:29

🔹Unapotaka kufanya mapenzi ya Mungu na kutembea pamoja nae katika maisha yako, unatakiwa kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo;

*1. LAZIMA UKUBALI KUMPA MUNGU NAFASI YA KWANZA KATIKA MAISHA YAKO.*

Unatakiwa kumpa nafasi ya kwanza katika kila eneo la maisha yako.
Nafasi ya kwanza kwenye moyo wako,nafasi ya kwanza kwenye uchumi wako, wokovu wako, utumishi wako, ndoa yako, nafasi ya kwanza kwenye muda wako, nafasi ya kwanza kwenye mipango yako n.k.

*2. LAZIMA UWE NA UTAYARI WA KUFANYA CHOCHOTE NA KWA MUDA WOWOTE.*

Tarajia kwamba wakati mwingine Mungu atakutaka ufanye vitu ambavyo havikuweko kwenye ratiba yako.

Anaweza akakuambia ingia kwenye maombi ya kufunga wakati wewe haukupanga, anaweza akakuamsha usiku kumuombea mtu wakati wewe ulitaka kulala, n.k. Unahitaji utayari wa wa hali ya juu sana vinginevyo utashindwa kutembea nae. (2Timotheo 4:2)

*3. LAZIMA UKUBALI KWENDA KINYUME NA MILA NA TAMADUNI AMBAZO ZIKO KINYUME NA NENO LAKE.*

Huwezi kutembea na Mungu wakati mila na tamaduni zingine unazozing’angania haziendani na neno lake, mfano ibada za wafu, matambiko n.k.
Vitu ambavyo viko kwenye jamii yako na yeye havipendi lazima ukubali kuviacha. (1Wakorintho 10:23)

*4. LAZIMA UWE TAYARI KUTEMBEA KWENYE MAJIRA YAKE.*

Hili sio jambo jepesi, na linawafanya watu wengi wapishane na muda wao wa kuinuliwa na Bwana/muda wa kujiliwa na Bwana/Appointed time.

Yanaweza yakawa ni majira ya kuoa au kuolewa, majira ya kuanza utumishi n.k.
Shida kubwa inayokuja hapa ni kwamba sio rahisi sana wanadamu wakakuelewa, kwa hiyo unazungukwa na hofu, na kuogopwa kutengwa.

*5. LAZIMA UTAFUTE KIWANGO KIKUBWA CHA IMANI.*

Kutembea na Mungu kunahitaji Imani zaidi, kwasababu wakati mwingine hutajua anakupeleka wapi.

Angalia mfano huu, halafu utaelewa kiwango cha imani ambacho kilikuwa kinahitajika, _Mwanzo 12:1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha._

Huo ulikuwa ni mtihani mgumu saa kwa Ibrahimu ingawa alifaulu.
Sijui ukiambiwa neno kama hilo na Mungu utajiuliza maswali mangapi moyoni mwako! Na utachukua uamuzi gani!

Pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6).

Hata kwenye maisha ni vigumu sana kuambatana na mtu kama humwamini.

*6. UNAHITAJI UNYENYEKEVU.*

Unyenyekevu ni wa muhimu sana ili uweze kutembea na Mungu katika maisha yako.

Mungu mwenyewe asema kwamba anaketi pamoja na mtu aliyetubu na kunyenyekea (Isaya 57:15).

Yakobo 4:6 … Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.

*7. UNAHITAJI UTII*.

Jambo la utii wa mtu ni la muhimu sana kwa Mungu kuliko sadaka zake(1Samweli 15:22)

Mungu anaupa utii nafasi kubwa sana kuliko sadaka.

Utii ni mlango mkubwa sana sana wa mtu kufanikishwa na Bwana (Isaya 1:19, Kumbukumbu la Torati 28: 1-13).

Kukosekana kwa utii huleta laana (Kumbukumbu la Torati 28: 15-68).

Kwahiyo ukitaka kutembea pamoja na Mungu, unahitaji roho ya utii wa hali ya juu na kutambua kuwa yeye ni boss na hivyo unatakiwa kumtii badala ya kusimamia misimamo yako. Tii anachokuambia kila wakati, ndio mtaenda pamoja.

*8. LAZIMA USHUGHULIKIE ROHO YA MAZOEA KWA MUNGU WAKO.*

Hiki ni kitu muhimu sana sana, kwasababu kadri unavyozidi kuwa karibu nae ni rahisi ukaanza kumzoea.

Hata kwenye maisha ya kawaida, kadri unavyozidi kuwa karibu zaidi na mtu ni rahisi ukajikuta heshima yako kwake inapungua, na unaanza kumuona ni wa kawaida sana.Hili jambo lilimgarimu Nabii Musa.

Angalia watu wengi ambao wameokoka, kadri wanavyozidi kukaa kwenye wokovu, wanajikuta wameanza kutembea kwenye wokovu kwa mazoea.

Pia angalia watumishi wengi (waimbaji, Wahubiri n.k, utagundua kuwa kadri wanavyozidi kutumika ndipo wanapoanza kutumika kwa mazoea na kutumia uzoefu wao badala ya kumtegea Roho Mtakatifu.

*9. LAZIMA UAMUE KUICHUKIA DUNIA NA MAMBO YAKE MAOVU.*

Ukitaka kuambatana na Mungu kwenye maisha yako ni lazima uamue kuyachukia mambo maovu ya dunia hii (Yakobo 4:4).

Mungu anachukia sana sana dhambi, ndio maana pamoja na kwamba Daudi alimpenda sana na alikuwa rafiki yake, lakini alipofanya zinaa na mke wa mtu alimkasirikia sana na hakumuacha bila adhabu.

*10. LAZIMA UWE TAYARI KUBEBA LAWAMA KUTOKA KWA WANADAMU NA KUKATALIWA NA KUDHARAULIWA WAKATI MWINGINE.*

Ukitaka kumpendeza Mungu na kutembea pamoja nae, ni lazima utambue kuwa muda mwingi wanadamu watakupinga sana, na utakataliwa na watu ambao wakati mwingine haukuwategemea.

Ndio maana watu wengine wakiokoka wanatengwa na ndugu zao, wengine wanaacha kusaidiwa na ndugu zao.

Unaweza ukakataliwa na kusemwa vibaya na wazazi wako, mke/mume wako, rafiki zako, watumishi wenzako, wafanyakazi wenzako n.k.
Yesu mwenyewe alipokuja duniani kufanya mapenzi ya Baba yake, alikataliwa na ndugu zake kabisa (Yohana 1:11).

Kwahiyo maeneo mengine ukikataliwa na kusemwa vibaya, usikasirike sana na kuharibu uhusiano wako na Mungu, kwasababu hata Mwokozi wetu Yesu alifanyiwa hivyo. Mtume Paulo alikataliwa, Daudi alikataliwa, Yusufu alikataliwa n.k

Jambo la muhimu kwako, ni kuendelea kusimama pamoja na Mungu wako na Imani yako. Shetani huwa anatumia watu ili kuharibu uhusiano wako na Mungu wako.

Bwana Yesu akubariki na azidi kukuongoza katika maisha yako,na ninaamini hili somo litakupa hatua mpya.

*ZINGATIA*: Ni vigumu sana ukayaweza mambo yote hayo kwa wakati mmoja,hivyo anza taratibu, jambo moja baada ya jingine. Mtegemee zaidi Roho Mtakatifu ili akusaidie kutembea kwenye hizo kanuni. Tamani sana awe rafiki yako na mshauri wako wa karibu.

🔹Washirikishe watu wengine mafundisho haya.

*Na Mwl M, Mwambeso*
0752 197065, 0784 136 816
Email: mwambeso80@gmail.com

Saturday, February 3, 2018

MEZA YA BWANA

MADA: "MEZA YA BWANA"

A. UTANGULIZI

"Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.

Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake." (Yohana 6:54,55&56)

B.LENGO/MAANA YA MEZA YA BWANA

Meza ya BWANA siyo msosi ama kinywaji tu; inayo maana na tafsiri ya kiroho:-

(i) Kuthibitisha USHIRIKA naye; yuko ndani yako nawe uko ndani Yake
(ii) Kutangaza mauti yake na kufufuka kwake, yeye ni UFUFUO
(iii) Kukiri kwamba WOKOVU unapatikana Kwake; yeye ni Njia,Kweli&Uzima

TAHADHARI: "Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana." (1 Wakorintho 11:27)


MTU AFANYEJE: "Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe." (1 Wakorintho 11:28)

USHIRIKI: Kula na kunywa tu kusikoendana na TAFAKARI ama MUKTADHA huo wa a MAANA ama LENGO la "Meza ya Bwana", huko ni sawa na kula na kunywa MKATE NA MVINYO kama viburudisho; ukifanya hivyo Kanisani unakuwa UNAKOSEA, wajitwalia HATIA, nenda ukafanyie KWENU ama MNAKOKUSANYIKIA kunywea na stori za hapa na pale

Paulo akahoji:
"Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya hili? La, hasha." (Wakorintho 11:22)

NB: Kuhusu kiwango mtu anywe ama kula, aina ya kinywaji ama mkate ubora wake, makanisa mengi yamedhibiti leo(mkate umachovywa tu ama kakipande kadogo na kamvinyo kadogo- wenzetu Wakorintho walilifanya KIHOLELA sana hadi hadi "MATABAKA" yalijidhihirisha,Paulo akahoji hivyo.

C. HITIMISHO

"Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu." (Luka 22:19&20)

Aliposema hayo hakumfukuza YUDA ingawaje aliijua nia yake baada ya kuingiwa na Shetani, akashiriki naye "meza ya BWANA".

Martin Kidenya (mwandishi)