Wednesday, June 29, 2016





HOFU NA WOGA WA USICHOKIJUA ( THE FEAR OF UNKNOWN)

Nilipokuwa mdogo nilikuwa mwoga sana wa fimbo. Mwalimu alikuwa akitaka kunichapa ningeweza kurudi hata nyumbani au kwenda kumwomba anisamehe baadae au kumwomba mwalimu rafiki yangu aniombee msamaha kwa mwalimu mwenzake. Shida ilikuwa ninapokuwa sijaenda shule na mwalimu akaahidi kutoa adhabu kwa watoro. Nilikuwa nakutana na rafiki yangu anasema “Mwalimu atakuua”. Hofu hii ilininyima raha kuliko viboko vyenyewe. Cha ajabu, mwalimu angenisamehe lakini niliadhibiwa kisakolojia sana na woga wa adhabu nisiyoijua itakuwaje!

Watu wengi hawajaribu mambo kadhaa maishani mwao kwa kuogopa kushindwa, na hata kama hawajui kwa kina “risk” watakazokabiliana nazo.

Hujajaribu biashara kwa hofu ya kushindwa, hujanunua kiwanja kwa hofu ya kukosa hela ya kujenga, hujampeleka mwanao shule nzuri kwa hofu ya kukosa ada, hujaanzisha huduma na chochote kwa kuogopa uliona wengine wakishindwa!  

Watu wana ndoto zao mioyoni, wanaogopa kuacha kazi kuzitimiza kwa kuogopa kisichojulikana – the fear of unknown!

Ninatamani leo nikutie moyo, uache woga uiendee ndoto yako. Stop fearing what you even don’t know! Usiogope kivuli chako.

Mwandishi John Mason anasema “paths without obstacles don’t lead anywhere important” akimaanisha  “njia isiyokuwa na vizuizi haikupeleki popote penye maana” itakiwa inaenda sehemu ya ovyo! Ili uipate dhahabu utachimba na kuchimbua sana!

Fil 4:13 “Nayeweza yote katika yeye anitiaye nguvu” Mwamini Mungu akutiaye nguvu na utavuka!

By Remigius Kyaruzi,

Monday, June 27, 2016




KUISHI KWENYE ENEO LA KUJIFARIJI (COMFORT ZONE)

Uf 21:7 " Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili".
Biblia hatwambii kwamba hatutakumbana na changamoto za kiimani, za maisha, za kifamilia, za kazi nk. Hata wanafunzi wa Yesu aliwajulisha kwamba wangeuawa, wangetengwa, wangekataliwa - he assured them about disappointment!

Lakini anasema, majaribu hayo yakija, LAZIMA MUYASHINDE!
Tunaishi maisha ambayo yamejaa vitu vya kututia woga na hofu, kukataliwa, kukatishwa tamaa, kutishwa, kuumizwa. Lakini mwandishi wa kitabu kiitwacho "The impossible is Possible, Doing what other say can't be done" {Yasiyowezekana Yanawezekana, kufanya ambayo wengine huseme hayawezi kufanyika} anasema mtu ambaye hajapitia hayo, HAJAWAHI KUJARIBU CHOCHOTE MAISHANI!

Katika maisha tunahitaji kukabiliana na mambo yote kwa kujiamini. Watu wengi deep inside (ndani sana ya mioyo yetu) tunaishi katika ndoto za kufanikiwa, lakini hatukuwahi kujaribu kuziendea hizo ndoto!

Ondoka katika eneo la kujifariji (comfort zone). Watu wengi utawasikia wanaongelea, ooh nilipokuwa bado nasoma nilikuwa mzuri kimasomo, ooh nilipokuwa bado msichana, mara hivi na hivi,! Tunataka uache kujifariji kwa yaliyopita, pambana sasa! Utishe kwenye eneo la biashara, kazi, ujasiriamali nk.

Ukiona unaishi kwa kusema Enzi zangu hivi na vile, jua kuna kitu kimekushinda unahitaji kujipanga upya! Kill your Goalith please!


 

Saturday, June 25, 2016

SOMO :-

UHUSIANO WA JINA NA MAISHA YA MTU

                 NA

YAFAHAM MAJINA HAYA KATIKA BIBLIA NA KUYAEPUKA!!!

****************************

Ndugu yangu mpendwa msomaji. Karibu tujifunze kitu muhimu sana yaani JINA

Biblia inasema katika MITHALI 22:-1:-" HERI KUCHAGUA JINA JEMA kuliko Mali nyingi ; Na neema kuliko fedha na dhahabu ".

Neno" HERI" maana yake ni baraka, mafanikio, utukufu, uzuri.

Neno la Mungu linatuambia hapo HERI KUCHAGUA JINA JEMA kuliko Mali nyingi........!!!  Maana yake baraka, mafanikio uzuri na utukufu huambatana ndani ya jina la mtu aliyechagua kuitwa JINA JEMA .

JINA ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya mtu.

Kila mtu ana jina lake na jina hilo limebeba kitu kikubwa sana ndani ya maisha ya mtu.


     MAANA YA JINA

Chimbuko la neno "Jina"  linatokana na neno la kigiriki liitwalo "SUM"

Neno hili "Sum" Maana yake ni :-" Ukumbusho au kumbukumbu au utambulisho   ".

KUTOKA 17:14:-" BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe Ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua ; ya kuwa nitaufuta UKUMBUSHO wa Amalek kabisa, usiwe tena chini ya mbingu ".

Ukumbusho au Sum kama ilivyoandikwa katika Biblia ya kigiriki. Inamainisha JINA.

Kwa sababu hiyo Jina /Sum ni alama ya pekee ambayo mtu anapewa ili kumtofautisha na mwingine.

Vigezo vya kumpatia mtu JINA hutofautiana. Kuna Majina mengi huwakilisha Uwezo na HESHIMA YA PEKEE ya jina muhusika . Kwa mfano Biblia inasema katika WAFILIPI 2 :9-11:-" Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lile lipitalo kila jina; ili Kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi ; Na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, Kwa utukufu wa Mungu Baba ".

Ameen.

Unaweza kuona hili jina la YESU ndani yake limebeba uwezo, nguvu, Mamlaka, utukufu na heshima ya kipekee. Hili ni jina kubwa na zito lipitalo majina yote.


Majina mengine huwakilisha sifa ya huyo anayepewa hilo jina. Mfano:-  RAIS wa nchi jina la sifa au cheo ambalo anapewa muhusika.

MAJINA MENGINE ni kuonyesha Mamlaka ndani yake . Mfano :-  Jemadari,  kaptain, Askari N. K. Ni jina linaloonyesha Mamlaka fulani ndani yake.


KWA SABABU YA TABIA FULANI FULANI BAADHI YA MAJINA HUTOKEA ,

Mfano mwingine JEHOHAV SHALOM. Maana yake Mungu ni Amani yetu ". Yeye anaitwa ni MUNGU WA AMANI au MFALME WA AMANI (Isaya 9:6-7).

Hili ni jina jema ambalo linatokana na sifa na tabia ya Mungu mwenyewe katika kuleta Amani Kwa Watu wake.

Unaweza kuona Mpaka hapo.


Mfano mwingine PAKA amepewa jina hilo NYAU Kwa sababu tu ya kulia nyauuuuuu!!

Kuna mtu anaitwa CHAUSIKU na jina hili alipewa baada ya kuzaliwa tu usiku.

Mimi sijui wewe unaitwa nani na jina lako linatokana na nini. Maana majina yanabeba jambo kubwa sana Kwa muhusika, katika ulimwengu wa roho.

Mfano mtu MCHAFU anaweza kupewa jina hilo kutokana na tabia yake ya uchafu wake na jina hilo likamshika na kushika maisha ya mtu huyo.
Hata MPOLE anaweza kupewa jina hilo Kwa sababu tu ya tabia ya upole wake.

Mfano kuna Watu Kayaiba au mwizi hayo ni majina yanayotokana na tabia ya mtu.


Je, jina lako ni nani?  Je, jina lako linatokana na kitu chema au kibaya??   JINA LAKO LIMEBEBA BARAKA AU LAANA ??  Jina lako limebeba nini??
Limebeba baraka au lina maagano na Shetani.


AINA KUU MBILI ZA MAJINA.

(1) JINA ambalo mtu anapewa na wazazi wake au jina la Asili.


(2) JINA kutoka nje ya familia kutokana na sifa za mtu huyo (majina ya kizungu).

Je jina lako ni nani??  Tafakari jina lako umelipataje.
Je, jina lako linatokana na nini??
Ni muhimu sana kujua maana ya jina lako na chanzo chake. Maana ya JINA LINAWEZA KUBEBA LAANA AU BARAKA ndani yake.


KUNA MAJINA HUTOKANA NA UKOO au kabila. Haya ni majina ya kuwa nayo makini sana, maana koo zetu nyingi hawajaokokoka hivyo ni rahisi sana kupewa jina ambalo lina maagano na mizimu na kukupelekea kuwa ni mtu wakupata majanga ya hapa na pale ndani ya maisha yako. Kumbe kiini cha tatizo ni jina lako

LUKA 1:13-17, 59-61:-" Lakini yule malaika akamwambia, USIOGOPE, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto mwanaume, na JINA LAKE UTAMUITA YOHANA. Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watafurahia kuzaliwa kwake. Kwa sababu Atakuwa mkuu mbele za BWANA ; hatakunywa divai wala kileo ; Naye atajwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa Mamaye. Na wengi katika Israeli atawarejeza Kwa BWANA Mungu wao...................... Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria. Mamaye akajibu la sivyo ; bali ataitwa Yohana. Wakamwambia, hapana mtu katika jamaa zako (ukoo wako) aitwaye jina hilo ".

Kwenye hilo Andiko hapo juu. Unaweza kujiuliza Kwanini Mungu aliamua kutoa jina la YOHANA aliyekuwa Yohana mbatizaji??  Huku ndugu zake wakitaka jina la ukoo?

MUNGU alijua kabisa kwamba jina hilo la ukoo lisingeweza kuitimiza kusudi lake kuu. Bali Mungu akampa jina la mtoto huyo aitwe " YOHANA".  Na jina hilo Yohana, maana yake ni " Yahweh is gracious or graced by Yahweh".  Maana yake :-" BWANA ni mwenye neema au Aliyepewa neema na BWANA ".

Na ndivyo ilivyokuwa Kwa huyo mtoto katika maisha yake. Ama kweli Mungu alimuinua na kumtumia kipekee sana ( MATHAYO 11:7-11).

Ndugu zake walitaka Apewe jina la ukoo. Lakini Mungu alikataa, Kwa maana alijua jina lao hilo la ukoo, lisingeweza kuitimiza kusudi lake.

Kumbe kuna majina ambayo hayawezi kutimiza makusudi ya Mungu juu ya maisha ya mtu. Ndiomana kuna kuokoka, pia ndiomana kuna ubatizo ili kuzika utu wa kale na maagano ya ukoo na mizimu na MAJINA YA KIKABILA ambayo mengine hutokana na maagano ya kishetani.


NB :-
Wazazi na wale ambao mtakuwa wazazi baadaye. Nawaombeni muangalie sana jambo hili yaani JINA ambalo mtampa mtoto wenu.



UMUHIMU WA JINA KATIKA MIPANGO WA MUNGU.

Jina la mtu ni Alama muhimu sana katika ulimwengu wa roho juu ya mpango wa Mungu au wa Shetani kwenye maisha ya mtu muhusika.

Kwa mfano. Jina YESU maana yake ni " Mwenye kuokoa au mwokozi"  ( MATHAYO 1:21).

Jina hili lilikuwa na kusudi maalumu katika mpango wa Mungu juu ya kazi yake ya kutaka kuwaokoa wanadamu ( Luka 19:9-10; Yohana 3:16-17).


Si hilo tu. Lakini Biblia inatuambia pia katika MWANZO 17:4-6,15-16:-" Mimi, Agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, wala jina lako hutaitwa tena Abramu, LAKINI JINA LAKO LITAKUWA IBRAHIM, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.

Mungu akamwambia Ibrahim, sarai mkeo, hutamwita jina lake sarai, Kwa kuwa JINA LAKE LITAKUWA SARA. Nami nitambariki, nami nitakupa Mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa Mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za Watu watatoka kwake ".

Tumeona hapo Ibrahim kabla hajaitwa hivyo, mara ya Kwanza aliitwa Abram.
Jina hili Abramu maana yake :-"  High Father /Height Father / Exalted Father.  Maana yake :- " Baba mtukufu".

Jina Ibrahim. Maana " Father of Multitude". Maana yake :- Baba wa mataifa mengi.

MUNGU aliona jina hilo Abramu haliwezi kutimiza kusudi lake ndiomana alimbadilisha jina hapo na kumwita Ibrahim. Hata mkewe Sara hapo Mwanzo aliitwa Sarai. Lakini Mungu wa mbinguni akambadilisha hilo jina la Sarai na kumwita SARA. Jina la Sara maana yake ni " Binti
mfalme".


Pia katika MWANZO 32:24-28:-" Yakobo akakaa pekee yake ; Na mtu mmoja akashindanaye mweleka hata Alfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake ; Ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema, niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, SIKUACHI, USIPONIBARIKI. Akamwuliza, jina lako ni nani?  Akasema Yakobo. Akamwambia, jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda ".

Jina Yakobo maana yake ni"  Mshikilia kisigino au mchukua nafasi ".

Lakini jina Israeli maana yake "  GOD STRIVES OR GOD PREVAILS ".  Maana yake Mungu mpiganaji wangu au Mungu ushindi wangu".


Ukisoma neno la Mungu pia katika MWANZO 41:45. Hapa Farao alimpa jina jipya Yusufu lakini jina lake hilo jipya halikufanya kazi na likafutika. Maana jina la YUSUFU ndilo liliokuwa linatimiza kusudi la mpango wa Mungu.


Pia katika katika kitabu cha HESABU 13:16 Biblia inasema :-" Hayo ndiyo majina ya hao waliotumwa na Musa waende kuilepeleza nchi. Na huyo Hoshea Mwana wa Nuni, Musa AKAMWITA JINA LAKE YOSHUA ".

Hapa jina la Hoshea hakikuwa linatimiza kusudi la Mungu ndiomana akambadilisha jina lake la zamani na kumwita jina jipya la YOSHUA. Ambalo maana yake ni" Mkombozi ".


Ndugu mpendwa msomaji. JE UNAONA UMUHIMU WA JINA??   Una maana kubwa katika mpango wa Mungu. Na sio kitu cha kukipuuzia bali ni jambo la kuwa nalo makini sana.

Kwa maana wako watu wengi sana kutokana na majina yao, mpango wa Mungu uliokusudiwa kwao wa wa kuwainua na kuwabariki, umeshindwa kutimia kwao.  JINA LAKO ni mlango wa kuachilia baraka za Mungu au kuzuia baraka za Mungu juu ya maisha yako.


UHUSIANO WA JINA NA MAISHA YA MTU MWENYEWE.

Biblia inasema juu ya hilo katika kitabu kile cha 1 SAMWELI 25:25:-"  " Nakusihi, bwana wangu, wewe usimuangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali ; Kwa maana KAMA LILIVYO JINA LAKE NDIVYO ALIVYO YEYE ; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao ; lakini mimi mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu uliowatuma".


Ni muhimu kufaham katika Andiko hilo, neno la Mungu linatufundisha juu ya uhusiano wa jina na maisha ya mtu.  Jina lako ndilo litakalo yafanya maisha yako kuwa jinsi yalivyo Leo. Maana yake jina lako likiwa baya au lenye maana mbaya na maisha yako yatakuwa ni Mabaya hapo mbeleni.

Ukiitwa Mateso. Maisha yako yatakuwa ni ya mateso kweli.
Ukiitwa Shida au Taabu. Maisha yako yatakuwa ni ya mahangaiko kweli.

Ukiitwa wewe Mjinga, utakuwa na maisha ya ujinga kweli.

Ukiitwa Mawazo. Maisha yako utakuwa ni mtu uliyejaa msononeko wa mawazo tuu.


Kuna Watu ambao wamerithi au wamepewa majina fulani na majina hayo yanawatesa sana.

Wapo watu waliorithi majina ya bibi zao au babu zao waliokuwa wanasumbuliwa na magonjwa fulani, lakini licha ya kupita miaka mingi Kwa sasa, wajukuu zao waliorithi majina yao kutoka kwao, wanasumbuliwa na magonjwa yale yale yaliyowatesa hadi kuwaua bibi zao.

WEWE MZAZI NAKUSIHI MPE MWANAO JINA ZURI LINALOMTUKUZA MUNGU.


Biblia inasema katika MITHALI 18 :21:-" Mauti na uzima huwa katika UWEZO WA ULIMI ; Na wale waupendao watakula matunda yake ".

Hata Mungu aliumba Kwa kutamka iwe, ikawa hivyo. Kuna nguvu katika kutamka. Hivyo wewe unayeitwa sura mbaya, hao watu wanaokuita hivyo wanakuumbia sura mbaya, hivyo unakuwa sura mbaya kweli na hakuna mtu atakaye taka kukuoa sura mbaya.

Tafuta maana ya jina lako. Itawezekana jina lako linatengeneza Baraka au Laana ndani ya maisha yako.

Na Kama jina lako lina maagano ya kiukoo au kikabila, au jina lako limekusababia Mabaya na matatizo kwenye maisha yako. Dawa yake ni KUOKOKA TU halafu badilisha hilo jina. Biblia inasema katika 2 WAKORINTO 5:17.


Kuna Watu wengine wanafilisika Kwa sababu tu ya majina yao yanawafilisi. Biblia inasema katika MITHALI 22:1:-" Heri kuchagua jina jema kuliko Mali nyingi ; Na neema kuliko fedha na dhahabu ".

Usikubali kuitwa jina lilo na maagano ya mababu wala Usikubali jina lenye ushetani ndani yake.

Wewe mzazi ni vizuri ukiaangalia jina zuri kwenye Biblia ili kumpa mtoto Wako. MWITE MTOTO WAKO JINA LINALOLETA UTUKUFU KWA MUNGU.

Jina la mtu ndilo litakalo yafanya maisha ya mtu kuwa jinsi yaliyo hapo baadaye. Majina Mabaya au majina yenye maana mbaya yanazuia kabisa baraka za Mungu juu ya maisha ya mtu. Naomba ufaham hilo mpendwa.


YAFAHAM MAJINA HAYA KATIKA BIBLIA NA KUYAEPUKA KUMUITA MTOTO WAKO.

Siyo kila jina lilotamkwa au kuandikwa katika Biblia lina maana nzuri. Hapana. Kuna baadhi ya majina mengine yako ndani ya Biblia lakini hayampi Mungu utukufu.

Kwa sababu hiyo tunapochagua jina katika Biblia na kuamua kuwatia watoto wetu. Ni muhimu Kwanza Asili ya hilo jina na maana yake ni nini hasa, kabla ya kulichukua jina hilo.

Kwa sababu hiyo Kwa mfano nyakati za Leo kuna Watu wengi ambao watapenda kuitwa majina haya MESHAKI, SHEDRAKI na ABELNEGO

NI muhimu tuyaangalie majina hayo ambayo watu wengi wakristo watayachukua majina hayo katika Biblia na kuitwa wewe Meshaki, yule Shedraki N. K.

Ni muhimu kufaham majina hayo Shedraki, Meshaki na Abelnego siyo majina kabisa yanayomtukuza Mungu wala kumpa utukufu.

Jina Belteshaza alipewa Daniel.
Jina Meshaki alipewa Mishaeli.
Jina Shadrack alipewa Hanania
Na Abelnego alipewa Azaria.
( SOMA :- DANIELI 1:6-7).

Hayo ni majina mapya waliyopewa na kuitwa na watu wakadayo waliokuwa ni waabudu miungu. Waliwabadilisha majina yao ya Mwanzo yaliyokuwa yanamtukuza Mungu wao YEHOVA na wakawaita majina yao mapya yaljyokuwa yanaitukuza hiyo miungu yao ya kibabeli.

(1) Jina HANANIAH. Maana yake " Yahweh is gracious".  " BWANA/ YEHOVA ni mwenye neema".

Lakini walimbadilisha hilo jina wakamwita SHADRACK.  Linatokana na neno >>>>" Shudur - Aku "

Na jina hilo jina maana yake   " Command of Aku". Maana yake Amri ya Aku.
Huyu Aku alikuwa ni mungu wa kibabeli, ambaye alikuwa ni mungu mwezi waliyemwabudu wapangani wa kibabeli.


Leo mtu anayeitwa Shadrack hilo ni jina baya linaloitukuza miungu badala ya Mungu Aliye hai.


(2) Jina AZARIA. Maana yake ni " Yahweh has helped". " BWANA/YEHOVAH amesaidia au Mungu ni msaada wangu "

Lakini Hao wapangani wa kibabeli walimbadilisha hilo jina na kumuita jina lao jipya ABEDNEGO.

Na hilo jina Abelnego linatokana na neno" Abednergal ".

Ambalo maana yake ni "  Servant of god Nebo/Nab ; Nergal ". Mtumishi wa mungu Nebo (miungu).


(3) Jina DANIELI maana yake"  God is my Judge ".  Mungu ni Hakimu wangu.


Lakini Hao wapangani walimbadilisha jina na kumuita Kwa jina la miungu yao Belteshaza.


(4) Jina la MISHAELI. Maana yake ni " Who is like God ".  Nani kama Mungu Yehovah".


Lakini Hao wapangani wa kibabeli walimbadilisha jina hilo na kumpa jina lao MESHAKI.

Jina Meshaki linatokana na neno >>>>" " Misha - Aku".  Ambalo ni   "Who is as Aku is".

Maana yake " Nani aliye kama mungu Aku".

Huyu Aku ni jina la miungu ya kibabeli, mungu mwezi aliyeabudiwa na wapangani wa kibabeli katika nchi ya Babeli.


👉 Kwa hiyo Leo mtu mkristo anayeitwa MESHAKI maskini hajui tu hilo ni jina la miungu. Ni jina linalomtukuza miungu badala ya Mungu Aliye hai YEHOVA


Biblia inatuonya kama wakristo tuliokolewa Kwa damu ya YESU. Majina yetu yawe na maana zuri ya kumpa Mungu wetu utukufu na sio miungu ya aina yoyote iwe ni mizimu ya kiukoo, kikabila N. K. Tusiitwe Kwa majina yao hayo.

Biblia inasema katika 📖 KUTOKA 23:13:-" Yaangalieni hayo yote niliyowaambia asema BWANA ; wala MSITAJE KABISA MAJINA YA MIUNGU MINGINE, wala yasisikizwe kutoka kinywani mwako. "

Amen.

Kama Wewe unaitwa shadrack au Meshaki na umeokoka. Ni muhimu ubadilishe hilo jina lako, liache.

Kama Wewe umepewa jina la kiukoo na jina hilo linamaana ya kuisifia miungu hiyo ya kikabila N. K.
Kama Wewe umeokoka liachee kulitumia jina hilo kabisa na ulikatae kwenye ulimwengu wa roho. Maana majina kama hayo yanakufanya jina lako lisiandikwe mbinguni hata kama umeokoka. YESU hawezi kulikiri jina lako hilo mbinguni (UFUNUO 3:4-5; UFUNUO 21 :27).

Na Kwa sababu hiyo Badilisha jina lako sasa mpendwa . Na Chagua JINA JIPYA lenye maana ya kumpa Mungu utukufu. Kama ilivyoandikwa   UFUNUO 2:17:-" Yeye aliye na sikio na Alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya Ile Mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo LIMEANDIKWA JINA JIPYA asilolijua mtu ila yeye anayelipokea ".

Ameen


MUNGU AWABARIKI WOTE Kwa neno la ujumbe huu. Mbarikiwe

Ni miye ,

Mtumishi wa Mungu,  Mwalimu Odrick   (0759 386 988 ; 0717 591 466). 📚➕📖


******************************

Thursday, June 23, 2016



*BWANA akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele. (MWA. 13:14-15 SUV).*
Kama vile Bwana alivyoongea na Abramu akamwambia ainue macho yake kutoka hapo alipo atazame kutoka hapo alipo upande wa kaskazini, na wa kusini, na wa mashariki na wa magharibi maana nchi yote aionayo atampa yeye n...a uzao wake hata milele, ni dhahiri tunaiona kanuni ya ajabu sana ya Mungu hapa.
Ibrahimu alikuwa amesimama katika nchi ya ahadi.
Akaambiwa ainue macho yake atazame pande zote.
Ni sehemu tu ya ile nchi ambayo aliweza kuiona ndiyo angepewa.
Bibilia ni kama nchi ya ahadi kwetu maana ndani yake kumejaa ahadi za Mungu kwa ajili yetu lakini haziwi zetu kwa sababu zimeandikwa bali zinakuwa zetu kwa sababu tunajua kuwa zimeandikwa na tunaachilia imani zetu kuzipokea.
Usipokuwa msomaji wa neno huwezi kujua nini kimeandikwa na usipojua nini kimeandikwa huwezi kumwamini Mungu kwa hiyo ahadi na usipomwamini hutaiona hiyo ahadi ikitimia maishani mwako.
Naamini kaskazini ni kitabu cha Mwanzo, kusini ni kitabu cha Malaki, mashariki ni kitabu cha Mathayo na magharibi ni kitabu cha Ufunuo.
Soma bibilia Mwanzo hadi Malaki, Mathayo hadi Ufunuo, kila ahadi utakayoiona Mungu atakupa wewe na uzao wako.
Utakachofanikiwa kukiona kwa habari ya ahadi za Mungu humo kwenye maandiko ndo hicho Mungu atakupa katika maisha yako maana ahadi za Mungu zinarithiwa kwa imani na uvumilivu sasa huwezi kumwamini Mungu kwa kitu ambacho hata hujui kama kipo.
Bibilia ni kitabu cha ahadi na maagizo.
Wengi tunaishi chini ya kiwango kwa sababu hatujui.
Hatujaona.
Na hatujaona kwa kuwa hatujaamua kuinua macho yetu kusoma.
Soma bibilia hapo ulipo uzijue ahadi za Mungu maana Mungu analiangalia neno Lake apate kulitimiza.
Haliangalii lililoandikwa alitimize bali lile lililoandikwa ambalo wewe unalijua alitimize maana ukishalijua ni rahisi kumwamini Mungu kwa ajili ya hilo.
Acha uvivu.
Soma.
Mungu amezikuza ahadi Zake juu ya Jina Lake lote.
Soma ujue ahadi za Mungu maana ni zile tu unazojua ndizo zinamfanya Mungu azitimize.
Imani yako itasababisha Mungu kutimiza ahadi Yake maishani mwako.

Saturday, June 11, 2016

Mkono wa Bwana Haukutupungukia.....!

"Tazama, mkono wa Bwana haukupungua, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia, lakini maovu yenu yamewafarikisha na ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia." Isaya 59:1-2

Huu ni ushahidi kwamba Mungu hutuwazia mema wakati wote. Anasema yeye hawezi kukosa kusikia, hawezi kutuacha tuangamie. Lakini anatuonesha tatizo liko kwetu, nalo ni MAOVU YETU!

Tukitubu na kuacha njia mbaya na kumgeukia atatusikia na atatuokoa!




Friday, June 10, 2016



 KUUKOMBOA WAKATI

Ef 5:15-16 "Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu"!

WEWE NI NANI ?
Umeshawahi kujiuliza wewe ninani?
Je unafaham umetoka wapi?
Na je' unajua unaenda wapi?...
Je umewahi kuwaza au kujiuliza kama hapo ulipo ndipo unapotakiwa kuwepo?
Je' toka upewe nafasi yakuwepo ulipo umeshafanya unacho takiwakufanya?
Je' ulishawahi kujiuliza kwanini haikua jana? Kwanini imekua leo?
Je' unafaham kua umeaminiwa kuwepo ulipo? Kama bado ulikuahujafaham, basi lifaham hilo, ili usimame kwenye nafasi uliyopewa. Acha manung'uniko unapoteza nguvukazi, chamsingi komboa wakati jitahidi kumaliza sehemuyako vyema kwa umakini mkubwa na ubunifu mkubwa.
UMEAMINIWA-Miriam Mauki

Thursday, June 9, 2016




Kanisa la Agape Christian Fellowship, Kimuli Karagwe! Kanisa hili linaongozwa na Mch Paul Maulid na lina waumini wanaozidi 250! Bwana anazidi kuonekana. Kila kazi itapimwa!

Kazi Yako Itapimwa
1 Kor 3:10
"Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake".
Kazi yako mpendwa ni ya muhimu iwe kwa kanisa au huduma uliyopewa na Mungu popote. Itapimwa na utalipwa. Hakikisha unalijua kusudi la Mungu kukuweka mahali ulipo na unalitimiza, ndipo uingoje taji yako!
Mungu akubariki na kukulinda

Tuesday, June 7, 2016

 Mama Judy Lamborn alikuwa ni Mmishenari aliyeipigania Injili toka New Zealand !
Alifika kanisani kwetu Agape Christian Fellowship na akatuasa sana juu ya kumtumikia Mungu bila kuzitelekeza familia zetu. Hii ilikuwa 07 Juni 2015.

Hata hivyo, ilikuwa safari yake ya mwisho na alifika Tanzania, akiwa Karagwe na alizikwa Karagwe Kayanga kwa kadiri ya wosia wake kwamba azikwe popote atakapoitiwa na Bwana.
Leo nikikumbuka mwaka mmoja tangu amekuja kutuhudumia, nafarijika na neno  1Thesolonike 4:13-18 " Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.."
Tunalo tumaini katika Kristo, atamfufua siku ile!


 Mbeba maono, Mwanzilishi wa makanisa ya Agape Christian Fellowship, C.N. Lucas akihudumu kama mkalimani, wakati Mmishenari Tony Lamborn toka New Zealand akitufundisha. Ujumbe wake ulikuwa THE POWER OF VISION (NGUVU YA MAONO). Neno katika Mithali 29:18 "Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria"
Maono hutupa sababu ya kuendelea kuishi, hutupa sababu ya kusonga mbele kwa sababu tunayo dira ya tunakoelekea.

Jifunze kuandika njozi / maono yako, omba Mungu ayatimize. Kama kuna kosa kubwa maishani ni kuishi bila maono na kutojua kusudi la maisha yako!




Kutoka kulia: Mch C.N. Lucas, Mzee Lamborn, aliyetwaliwa Mama Judy na pastor Remigius Kyaruzi wakiwa kanisani Agape Christian Fellowship, Kitunda Kibeberu, Dar es salaam. Hapo ni 07 June 2015

Maneno Ya kutafakari

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako Nisije nikakutenda dhambi. Zaburi 119:11

Mwanangu Sikiliza na kuzipokea kauli zangu na Miaka ya maisha yako itakuwa mingi. Mithali 4:10

Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia zangu. Zaburi 119:105

Neno lako limesifika sana kwa hiyo mtumishi wako amelipenda. Zaburi 119:140

Ezekieli 3:1-3
 Akaniambia mwanadamu lisha tumbo lako ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo, Ndipo nikalila nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu kama utamu wa asali.

Maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Waebrania 4:12

Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na tenzi za rohoni huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16

Yafahamu sana haya nisemayo kwamaana Bwana atakupa akili katika mambo yote. 2Timo¬theo 2:7

Thursday, June 2, 2016

Mpingeni Shetani


1 Pet. 5:8-9
“Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.”

YAK. 4:7
“Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.”
--------
Mpinge Shetani, unaambiwa, na atakukimbia! Ni vizuri akukimbie, awe mbali nawe. Na hii ndio namna ya kumpinga;
1. Uwe na kiasi (self control). Hii ni moja ya silaha nzuri sana itakukuzuwia kutumbukia ktk mitego mingi ya Ibilisi anayekuzungukia kila wakati ili akunase.
2. Kesha. Usisinzie, kuwa makini, kuwa macho, dumu ktk Bwana, dumu ktk neno, dumu ktk imani! Huwezi kumpinga wakati upo legelege kiimani, haiwezekani. Imani hutupa ushindi.
3. Mtii Mungu. Ishi anavyotaka uishi, kamata anachotaka ukamate, acha asichokitaka!

Fanyia kazi maisha yako ya kiroho, tengeneza UTII, KIASI na KUKESHA ktk maisha yako.
BARIKIWA NA BWANA!!!!
By pastor Chikojo

Tuesday, May 17, 2016

Mwanzilishi na mbeba maona ya Agape Christian Fellowship, Mtumishi wa Mungu C. N. Lucas.
Mungu amekuwa akimtumia kama muhubiri wa kimataifa , akiifanya kazi ya Mungu kwa zaidi ya miaka 40!
Amewezesha kueneza Injili hasa vijijini ambako wengi hawafiki, na hakika Mungu anaonekana.

Tunamwombea Mungu azidi kumlinda na kumpigania, afikie mwisho mzuri wa utume wake

2 Timotheo 4 : 7-8 "Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, baili na wote pia waliopenda kufunuliwa kwake"


Monday, May 16, 2016

Mtumishi wa Mungu dada Anna Kiyungu akifundisha akina mama wa Agape Christian Fellowship Kitunda Dsm.
Semina yetu ilihusu MWANAMKE KAMA NGUZO YA KANISA NA FAMILIA.
Semina itakoyofuatia ni Ujasiriamali!

Thursday, April 7, 2016

DAY 2: PAULO ALIPOKUTANA NA YESU 
 
(Semina hii inaendelea Agape Christian Fellowship Kitunda Kibeberu hadi Jpili 10/04/2016 )

Katika siku yetu ya pili inayoongozwa na Mwl Katunzi; tulijifunza habari za Paulo wakati huo akiitwa Sauli kukutana na Yesu!
Somo letu lilijikita
Mdo 9:1-19
1 Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, 2akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. 3Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. 4Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? 5Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. 6Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. 7Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu. 8Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi. 10 Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. 11Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba; 12naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena. 13Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu; 14hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako. 15Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. 16Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu. 17Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. 18Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; 19akala chakula, na kupata nguvu.Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.
Katika habari maandiko haya; tunaona 
 
Mungu aweza kuamua kumtumia yeyote kwa kazi yake. 
Sauli aliriudhi kanisa na kuwaua watu wa Mungu. Lakini Kristo aliona amtumie kwa kazi yake. Kumbadilisha ilikuwa na juu ya Mungu mwenyewe. Wakati wa Bwana kukutumia ukifika anakutuma; haijalishi ukoje, upo mahali gani
Paulo anapoisikia sauti ya Yesu anamuuliza Nifanye nini Bwana? Ni vizuri ukijua kusudi la Mungu juu ya huduma yako. Msikilize Mungu akupe maelekezo
Pamoja na usomi wa Paulo, cheo chake kimamlaka nk anatumwa kwa mtu mdogo ANANIA! Anania akamwambia yampasayo kutenda. Akamwambia simama uingie Dameski.
Kama Paulo alingekubali kujishusha tusingemsikia, lakini alikubali kujifunza. Mchungaji na mjumbe wa Mungu anayekuletea neon la Mungu, ndiye Anania wako. Msikilize huyo, jifunze makusudi ya Mungu juu yako mpendwa. Watu wa sasa tunaangaika kutafuta miujiza, si kujifunza kusudi la Mungu. Neno la Mungu linasema “Ishara ni kwa wasioamini wapate kuamini
1 Kor 14:22
Ikiwa umemwamini Mungu, tafuta kujua kusudi lake kwako.
Katika habari za Paulo kukutana na Yesu , tuliona mtu unaweza kukosa faidi ya kuwa kanisani kwa kutotambua kusudi. Unahitaji kuuliza kama Paulo, Nifanye nini Bwana? Kumbe kuokoka ni kuitwa kufanya kazi.
1) Kwa nini Mungu amekuchagua? Kwa nini umeokolewa
2) Kwa nini upo mahali ulipo?
Anania alimwambia Paulo, Mungu wa Baba zetu amekuchagua! Wokovu wako hautakuwa na faida usipojua kusudi, utapoteza muda! Pia soma Mdo 22:6-16

Mungu akubariki na kukulinda!
Karibu Agape Christian Fellowship, Kitunda Kibeberu uwe mwanafunzi wa Yesu!
Waweza kutupigia simu: 0713386315/0753230205/0713453213

Tuesday, April 5, 2016

SEMINA YA SIKU 8 AGAPE CHRISTIAN FELLOWSHIP, KITUNDA DSM 03-10/aPRIL 2016

SEMINA YA NENO LA MUNGU INAYOENDELEA AGAPE cHRISTIAN FELLOWSHIP, KITUNDA KIBEBERU CHINI YA MWL KATUNZI KUTOKA EAGT TEMEKE
(iPO KILA SIKU HADI TAR 10/04/2016 SAA KUMI JIONI)
DAY 1: SISI NI WATUMWA
Tulipitia maandiko Rum 1:1, Fil 1:1, Yak 1:1
Hayo yote yanamwonyesha Paulo akijiita MTUMWA! Tulifundishwa kanisa la kwanza, walijitambua kuwa wao ni watumwa. Utumwa ni kupoteza HAKI YAKO MWENYEWE; na kuishi sawa na mapenzi ya BWANA wako. Rum 10:8-10 (Ukimkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako , unaokoka)
Wakati wa biashara ya utumwa; mtumwa hata akiugua, aliogopa kumwambia bwana wake maana hakika angeuawa. Sisi tunaishi na kuenenda kwa Mungu kama MABOSS! Sisi mafua tu hatwendi kanisani, lakini mwenye mafua anapika, anaenda sokoni na kufanya shopping!
Tumechagua siku ya kwenda kwenye ibada ni Jpili tu! Mungu hufanya kazi na watumwa, watu waliomwamini na wanaomtetemekea yeye peke. Sasa unatetemeshwa na mkuu wako wa kazi kuliko Mungu mwenyewe. Biashara yako inakutawala huna muda na Mungu.
Ukijitambua kwamba wewe ni mtumwa ndipo Mungu anafanya kazi na wewe. Tumekuwa watu wa kujiinua. Tukifanikiwa kidogo basi kiburi kinapanda.
Yoh 3:30
“Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua”. Yohana mbatizaji alishuhudia na kufurahi yeye kushuka, kuwa si kitu ili Yesu atawale. Mwisho wake alikatwa kichwa gerezani!
Watumishi wa sasa ni wa kujitukuza, akitenda muujiza kidogo basi Tanzania yote itajua. Lakini neno
Lk 17:10
|” Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mlioyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya”
Yesu anatufundisha kutimiza wajibu bila kujisifu, kujiinua na kujiona wa maana. Anawafundisha unyenyekevu. Kwa nini tunapoteza unyenyekevu katika maisha yetu. Petro alikuwa na UPAKA kuliko wanaojiita wazee wa upako kwa sasa. Kivuli chake alikopita kilifufua wafu, na wagonjwa walipona. Lakini hawakujiinua.
Tulifundishwa juu ya Eliya kuzuia mvua miaka 3 na nusu, na akajificha kwa mama wa Serepta asionekane! Kama leo mtu angefufua maiti au aneamuru mvua isinyeshe angetamani CNN na BBC ndiyo wamtangaze!
Yesu anawauliza wanafunzi; kwa nini mnaniita Bwana , Bwana, lakini hamtendi nisemayo? Lk 6:46
Ukiwa mtumwa utafanya Bwana wako anachokuamuru! Jifunze kunyenyekea 2Nyak 7:14
Mungu akubariki ukiweza kufika agape Kujifunza. Usifungwe na dini, naombea roho za udhehebu zikuache maana wewe ni mtumwa wa Kristo! Tupigie Mch Kyaruzi 0713386315,

Wednesday, January 20, 2016

Tunaamini ubatizo wa maji mengi!!
Hapa tumemaliza kubatiza waongofu wapya!



Pastor Remigius Kyaruzi, Agape Christian Fellowship, Dsm

03rd January, 2016 Praise and Worship!
Agape Praise Team organizes Praise and Worship events! Join as, at Agape Christian Fellowship , Kitunda Dar es Salaam.