Mama Judy Lamborn alikuwa ni Mmishenari aliyeipigania Injili toka New Zealand !
Alifika kanisani kwetu Agape Christian Fellowship na akatuasa sana juu ya kumtumikia Mungu bila kuzitelekeza familia zetu. Hii ilikuwa 07 Juni 2015.
Hata hivyo, ilikuwa safari yake ya mwisho na alifika Tanzania, akiwa Karagwe na alizikwa Karagwe Kayanga kwa kadiri ya wosia wake kwamba azikwe popote atakapoitiwa na Bwana.
Leo nikikumbuka mwaka mmoja tangu amekuja kutuhudumia, nafarijika na neno 1Thesolonike 4:13-18 " Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.."
Tunalo tumaini katika Kristo, atamfufua siku ile!
Mbeba maono, Mwanzilishi wa makanisa ya Agape Christian Fellowship, C.N. Lucas akihudumu kama mkalimani, wakati Mmishenari Tony Lamborn toka New Zealand akitufundisha. Ujumbe wake ulikuwa THE POWER OF VISION (NGUVU YA MAONO). Neno katika Mithali 29:18 "Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria"
Maono hutupa sababu ya kuendelea kuishi, hutupa sababu ya kusonga mbele kwa sababu tunayo dira ya tunakoelekea.
Jifunze kuandika njozi / maono yako, omba Mungu ayatimize. Kama kuna kosa kubwa maishani ni kuishi bila maono na kutojua kusudi la maisha yako!
Kutoka kulia: Mch C.N. Lucas, Mzee Lamborn, aliyetwaliwa Mama Judy na pastor Remigius Kyaruzi wakiwa kanisani Agape Christian Fellowship, Kitunda Kibeberu, Dar es salaam. Hapo ni 07 June 2015

No comments:
Post a Comment