Tuesday, April 5, 2016

SEMINA YA SIKU 8 AGAPE CHRISTIAN FELLOWSHIP, KITUNDA DSM 03-10/aPRIL 2016

SEMINA YA NENO LA MUNGU INAYOENDELEA AGAPE cHRISTIAN FELLOWSHIP, KITUNDA KIBEBERU CHINI YA MWL KATUNZI KUTOKA EAGT TEMEKE
(iPO KILA SIKU HADI TAR 10/04/2016 SAA KUMI JIONI)
DAY 1: SISI NI WATUMWA
Tulipitia maandiko Rum 1:1, Fil 1:1, Yak 1:1
Hayo yote yanamwonyesha Paulo akijiita MTUMWA! Tulifundishwa kanisa la kwanza, walijitambua kuwa wao ni watumwa. Utumwa ni kupoteza HAKI YAKO MWENYEWE; na kuishi sawa na mapenzi ya BWANA wako. Rum 10:8-10 (Ukimkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako , unaokoka)
Wakati wa biashara ya utumwa; mtumwa hata akiugua, aliogopa kumwambia bwana wake maana hakika angeuawa. Sisi tunaishi na kuenenda kwa Mungu kama MABOSS! Sisi mafua tu hatwendi kanisani, lakini mwenye mafua anapika, anaenda sokoni na kufanya shopping!
Tumechagua siku ya kwenda kwenye ibada ni Jpili tu! Mungu hufanya kazi na watumwa, watu waliomwamini na wanaomtetemekea yeye peke. Sasa unatetemeshwa na mkuu wako wa kazi kuliko Mungu mwenyewe. Biashara yako inakutawala huna muda na Mungu.
Ukijitambua kwamba wewe ni mtumwa ndipo Mungu anafanya kazi na wewe. Tumekuwa watu wa kujiinua. Tukifanikiwa kidogo basi kiburi kinapanda.
Yoh 3:30
“Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua”. Yohana mbatizaji alishuhudia na kufurahi yeye kushuka, kuwa si kitu ili Yesu atawale. Mwisho wake alikatwa kichwa gerezani!
Watumishi wa sasa ni wa kujitukuza, akitenda muujiza kidogo basi Tanzania yote itajua. Lakini neno
Lk 17:10
|” Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mlioyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya”
Yesu anatufundisha kutimiza wajibu bila kujisifu, kujiinua na kujiona wa maana. Anawafundisha unyenyekevu. Kwa nini tunapoteza unyenyekevu katika maisha yetu. Petro alikuwa na UPAKA kuliko wanaojiita wazee wa upako kwa sasa. Kivuli chake alikopita kilifufua wafu, na wagonjwa walipona. Lakini hawakujiinua.
Tulifundishwa juu ya Eliya kuzuia mvua miaka 3 na nusu, na akajificha kwa mama wa Serepta asionekane! Kama leo mtu angefufua maiti au aneamuru mvua isinyeshe angetamani CNN na BBC ndiyo wamtangaze!
Yesu anawauliza wanafunzi; kwa nini mnaniita Bwana , Bwana, lakini hamtendi nisemayo? Lk 6:46
Ukiwa mtumwa utafanya Bwana wako anachokuamuru! Jifunze kunyenyekea 2Nyak 7:14
Mungu akubariki ukiweza kufika agape Kujifunza. Usifungwe na dini, naombea roho za udhehebu zikuache maana wewe ni mtumwa wa Kristo! Tupigie Mch Kyaruzi 0713386315,

No comments:

Post a Comment