HOFU NA WOGA WA USICHOKIJUA ( THE FEAR OF
UNKNOWN)
Nilipokuwa mdogo nilikuwa mwoga sana
wa fimbo. Mwalimu alikuwa akitaka kunichapa ningeweza kurudi hata nyumbani au
kwenda kumwomba anisamehe baadae au kumwomba mwalimu rafiki yangu aniombee
msamaha kwa mwalimu mwenzake. Shida ilikuwa ninapokuwa sijaenda shule na
mwalimu akaahidi kutoa adhabu kwa watoro. Nilikuwa nakutana na rafiki yangu
anasema “Mwalimu atakuua”. Hofu hii ilininyima raha kuliko viboko vyenyewe. Cha
ajabu, mwalimu angenisamehe lakini niliadhibiwa kisakolojia sana na woga wa
adhabu nisiyoijua itakuwaje!
Watu wengi hawajaribu mambo kadhaa
maishani mwao kwa kuogopa kushindwa, na hata kama hawajui kwa kina “risk”
watakazokabiliana nazo.
Hujajaribu biashara kwa hofu ya
kushindwa, hujanunua kiwanja kwa hofu ya kukosa hela ya kujenga, hujampeleka
mwanao shule nzuri kwa hofu ya kukosa ada, hujaanzisha huduma na chochote kwa
kuogopa uliona wengine wakishindwa!
Watu wana ndoto zao mioyoni,
wanaogopa kuacha kazi kuzitimiza kwa kuogopa kisichojulikana – the fear of
unknown!
Ninatamani leo nikutie moyo, uache
woga uiendee ndoto yako. Stop fearing what you even don’t know! Usiogope kivuli
chako.
Mwandishi John Mason anasema “paths
without obstacles don’t lead anywhere important” akimaanisha “njia isiyokuwa na vizuizi haikupeleki popote
penye maana” itakiwa inaenda sehemu ya ovyo! Ili uipate dhahabu utachimba na
kuchimbua sana!
Fil 4:13 “Nayeweza yote katika yeye
anitiaye nguvu” Mwamini Mungu akutiaye nguvu na utavuka!
By Remigius Kyaruzi,
No comments:
Post a Comment