SOMO :-
UHUSIANO WA JINA NA MAISHA YA MTU
NA
YAFAHAM MAJINA HAYA KATIKA BIBLIA NA KUYAEPUKA!!!
****************************
Ndugu yangu mpendwa msomaji. Karibu tujifunze kitu muhimu sana yaani JINA
Biblia inasema katika MITHALI 22:-1:-" HERI KUCHAGUA JINA JEMA kuliko Mali nyingi ; Na neema kuliko fedha na dhahabu ".
Neno" HERI" maana yake ni baraka, mafanikio, utukufu, uzuri.
Neno la Mungu linatuambia hapo HERI KUCHAGUA JINA JEMA kuliko Mali nyingi........!!! Maana yake baraka, mafanikio uzuri na utukufu huambatana ndani ya jina la mtu aliyechagua kuitwa JINA JEMA .
JINA ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya mtu.
Kila mtu ana jina lake na jina hilo limebeba kitu kikubwa sana ndani ya maisha ya mtu.
MAANA YA JINA
Chimbuko la neno "Jina" linatokana na neno la kigiriki liitwalo "SUM"
Neno hili "Sum" Maana yake ni :-" Ukumbusho au kumbukumbu au utambulisho ".
KUTOKA 17:14:-" BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe Ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua ; ya kuwa nitaufuta UKUMBUSHO wa Amalek kabisa, usiwe tena chini ya mbingu ".
Ukumbusho au Sum kama ilivyoandikwa katika Biblia ya kigiriki. Inamainisha JINA.
Kwa sababu hiyo Jina /Sum ni alama ya pekee ambayo mtu anapewa ili kumtofautisha na mwingine.
Vigezo vya kumpatia mtu JINA hutofautiana. Kuna Majina mengi huwakilisha Uwezo na HESHIMA YA PEKEE ya jina muhusika . Kwa mfano Biblia inasema katika WAFILIPI 2 :9-11:-" Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lile lipitalo kila jina; ili Kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi ; Na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, Kwa utukufu wa Mungu Baba ".
Ameen.
Unaweza kuona hili jina la YESU ndani yake limebeba uwezo, nguvu, Mamlaka, utukufu na heshima ya kipekee. Hili ni jina kubwa na zito lipitalo majina yote.
Majina mengine huwakilisha sifa ya huyo anayepewa hilo jina. Mfano:- RAIS wa nchi jina la sifa au cheo ambalo anapewa muhusika.
MAJINA MENGINE ni kuonyesha Mamlaka ndani yake . Mfano :- Jemadari, kaptain, Askari N. K. Ni jina linaloonyesha Mamlaka fulani ndani yake.
KWA SABABU YA TABIA FULANI FULANI BAADHI YA MAJINA HUTOKEA ,
Mfano mwingine JEHOHAV SHALOM. Maana yake Mungu ni Amani yetu ". Yeye anaitwa ni MUNGU WA AMANI au MFALME WA AMANI (Isaya 9:6-7).
Hili ni jina jema ambalo linatokana na sifa na tabia ya Mungu mwenyewe katika kuleta Amani Kwa Watu wake.
Unaweza kuona Mpaka hapo.
Mfano mwingine PAKA amepewa jina hilo NYAU Kwa sababu tu ya kulia nyauuuuuu!!
Kuna mtu anaitwa CHAUSIKU na jina hili alipewa baada ya kuzaliwa tu usiku.
Mimi sijui wewe unaitwa nani na jina lako linatokana na nini. Maana majina yanabeba jambo kubwa sana Kwa muhusika, katika ulimwengu wa roho.
Mfano mtu MCHAFU anaweza kupewa jina hilo kutokana na tabia yake ya uchafu wake na jina hilo likamshika na kushika maisha ya mtu huyo.
Hata MPOLE anaweza kupewa jina hilo Kwa sababu tu ya tabia ya upole wake.
Mfano kuna Watu Kayaiba au mwizi hayo ni majina yanayotokana na tabia ya mtu.
Je, jina lako ni nani? Je, jina lako linatokana na kitu chema au kibaya?? JINA LAKO LIMEBEBA BARAKA AU LAANA ?? Jina lako limebeba nini??
Limebeba baraka au lina maagano na Shetani.
AINA KUU MBILI ZA MAJINA.
(1) JINA ambalo mtu anapewa na wazazi wake au jina la Asili.
(2) JINA kutoka nje ya familia kutokana na sifa za mtu huyo (majina ya kizungu).
Je jina lako ni nani?? Tafakari jina lako umelipataje.
Je, jina lako linatokana na nini??
Ni muhimu sana kujua maana ya jina lako na chanzo chake. Maana ya JINA LINAWEZA KUBEBA LAANA AU BARAKA ndani yake.
KUNA MAJINA HUTOKANA NA UKOO au kabila. Haya ni majina ya kuwa nayo makini sana, maana koo zetu nyingi hawajaokokoka hivyo ni rahisi sana kupewa jina ambalo lina maagano na mizimu na kukupelekea kuwa ni mtu wakupata majanga ya hapa na pale ndani ya maisha yako. Kumbe kiini cha tatizo ni jina lako
LUKA 1:13-17, 59-61:-" Lakini yule malaika akamwambia, USIOGOPE, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto mwanaume, na JINA LAKE UTAMUITA YOHANA. Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watafurahia kuzaliwa kwake. Kwa sababu Atakuwa mkuu mbele za BWANA ; hatakunywa divai wala kileo ; Naye atajwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa Mamaye. Na wengi katika Israeli atawarejeza Kwa BWANA Mungu wao...................... Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria. Mamaye akajibu la sivyo ; bali ataitwa Yohana. Wakamwambia, hapana mtu katika jamaa zako (ukoo wako) aitwaye jina hilo ".
Kwenye hilo Andiko hapo juu. Unaweza kujiuliza Kwanini Mungu aliamua kutoa jina la YOHANA aliyekuwa Yohana mbatizaji?? Huku ndugu zake wakitaka jina la ukoo?
MUNGU alijua kabisa kwamba jina hilo la ukoo lisingeweza kuitimiza kusudi lake kuu. Bali Mungu akampa jina la mtoto huyo aitwe " YOHANA". Na jina hilo Yohana, maana yake ni " Yahweh is gracious or graced by Yahweh". Maana yake :-" BWANA ni mwenye neema au Aliyepewa neema na BWANA ".
Na ndivyo ilivyokuwa Kwa huyo mtoto katika maisha yake. Ama kweli Mungu alimuinua na kumtumia kipekee sana ( MATHAYO 11:7-11).
Ndugu zake walitaka Apewe jina la ukoo. Lakini Mungu alikataa, Kwa maana alijua jina lao hilo la ukoo, lisingeweza kuitimiza kusudi lake.
Kumbe kuna majina ambayo hayawezi kutimiza makusudi ya Mungu juu ya maisha ya mtu. Ndiomana kuna kuokoka, pia ndiomana kuna ubatizo ili kuzika utu wa kale na maagano ya ukoo na mizimu na MAJINA YA KIKABILA ambayo mengine hutokana na maagano ya kishetani.
NB :-
Wazazi na wale ambao mtakuwa wazazi baadaye. Nawaombeni muangalie sana jambo hili yaani JINA ambalo mtampa mtoto wenu.
UMUHIMU WA JINA KATIKA MIPANGO WA MUNGU.
Jina la mtu ni Alama muhimu sana katika ulimwengu wa roho juu ya mpango wa Mungu au wa Shetani kwenye maisha ya mtu muhusika.
Kwa mfano. Jina YESU maana yake ni " Mwenye kuokoa au mwokozi" ( MATHAYO 1:21).
Jina hili lilikuwa na kusudi maalumu katika mpango wa Mungu juu ya kazi yake ya kutaka kuwaokoa wanadamu ( Luka 19:9-10; Yohana 3:16-17).
Si hilo tu. Lakini Biblia inatuambia pia katika MWANZO 17:4-6,15-16:-" Mimi, Agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, wala jina lako hutaitwa tena Abramu, LAKINI JINA LAKO LITAKUWA IBRAHIM, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.
Mungu akamwambia Ibrahim, sarai mkeo, hutamwita jina lake sarai, Kwa kuwa JINA LAKE LITAKUWA SARA. Nami nitambariki, nami nitakupa Mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa Mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za Watu watatoka kwake ".
Tumeona hapo Ibrahim kabla hajaitwa hivyo, mara ya Kwanza aliitwa Abram.
Jina hili Abramu maana yake :-" High Father /Height Father / Exalted Father. Maana yake :- " Baba mtukufu".
Jina Ibrahim. Maana " Father of Multitude". Maana yake :- Baba wa mataifa mengi.
MUNGU aliona jina hilo Abramu haliwezi kutimiza kusudi lake ndiomana alimbadilisha jina hapo na kumwita Ibrahim. Hata mkewe Sara hapo Mwanzo aliitwa Sarai. Lakini Mungu wa mbinguni akambadilisha hilo jina la Sarai na kumwita SARA. Jina la Sara maana yake ni " Binti
mfalme".
Pia katika MWANZO 32:24-28:-" Yakobo akakaa pekee yake ; Na mtu mmoja akashindanaye mweleka hata Alfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake ; Ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema, niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, SIKUACHI, USIPONIBARIKI. Akamwuliza, jina lako ni nani? Akasema Yakobo. Akamwambia, jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda ".
Jina Yakobo maana yake ni" Mshikilia kisigino au mchukua nafasi ".
Lakini jina Israeli maana yake " GOD STRIVES OR GOD PREVAILS ". Maana yake Mungu mpiganaji wangu au Mungu ushindi wangu".
Ukisoma neno la Mungu pia katika MWANZO 41:45. Hapa Farao alimpa jina jipya Yusufu lakini jina lake hilo jipya halikufanya kazi na likafutika. Maana jina la YUSUFU ndilo liliokuwa linatimiza kusudi la mpango wa Mungu.
Pia katika katika kitabu cha HESABU 13:16 Biblia inasema :-" Hayo ndiyo majina ya hao waliotumwa na Musa waende kuilepeleza nchi. Na huyo Hoshea Mwana wa Nuni, Musa AKAMWITA JINA LAKE YOSHUA ".
Hapa jina la Hoshea hakikuwa linatimiza kusudi la Mungu ndiomana akambadilisha jina lake la zamani na kumwita jina jipya la YOSHUA. Ambalo maana yake ni" Mkombozi ".
Ndugu mpendwa msomaji. JE UNAONA UMUHIMU WA JINA?? Una maana kubwa katika mpango wa Mungu. Na sio kitu cha kukipuuzia bali ni jambo la kuwa nalo makini sana.
Kwa maana wako watu wengi sana kutokana na majina yao, mpango wa Mungu uliokusudiwa kwao wa wa kuwainua na kuwabariki, umeshindwa kutimia kwao. JINA LAKO ni mlango wa kuachilia baraka za Mungu au kuzuia baraka za Mungu juu ya maisha yako.
UHUSIANO WA JINA NA MAISHA YA MTU MWENYEWE.
Biblia inasema juu ya hilo katika kitabu kile cha 1 SAMWELI 25:25:-" " Nakusihi, bwana wangu, wewe usimuangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali ; Kwa maana KAMA LILIVYO JINA LAKE NDIVYO ALIVYO YEYE ; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao ; lakini mimi mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu uliowatuma".
Ni muhimu kufaham katika Andiko hilo, neno la Mungu linatufundisha juu ya uhusiano wa jina na maisha ya mtu. Jina lako ndilo litakalo yafanya maisha yako kuwa jinsi yalivyo Leo. Maana yake jina lako likiwa baya au lenye maana mbaya na maisha yako yatakuwa ni Mabaya hapo mbeleni.
Ukiitwa Mateso. Maisha yako yatakuwa ni ya mateso kweli.
Ukiitwa Shida au Taabu. Maisha yako yatakuwa ni ya mahangaiko kweli.
Ukiitwa wewe Mjinga, utakuwa na maisha ya ujinga kweli.
Ukiitwa Mawazo. Maisha yako utakuwa ni mtu uliyejaa msononeko wa mawazo tuu.
Kuna Watu ambao wamerithi au wamepewa majina fulani na majina hayo yanawatesa sana.
Wapo watu waliorithi majina ya bibi zao au babu zao waliokuwa wanasumbuliwa na magonjwa fulani, lakini licha ya kupita miaka mingi Kwa sasa, wajukuu zao waliorithi majina yao kutoka kwao, wanasumbuliwa na magonjwa yale yale yaliyowatesa hadi kuwaua bibi zao.
WEWE MZAZI NAKUSIHI MPE MWANAO JINA ZURI LINALOMTUKUZA MUNGU.
Biblia inasema katika MITHALI 18 :21:-" Mauti na uzima huwa katika UWEZO WA ULIMI ; Na wale waupendao watakula matunda yake ".
Hata Mungu aliumba Kwa kutamka iwe, ikawa hivyo. Kuna nguvu katika kutamka. Hivyo wewe unayeitwa sura mbaya, hao watu wanaokuita hivyo wanakuumbia sura mbaya, hivyo unakuwa sura mbaya kweli na hakuna mtu atakaye taka kukuoa sura mbaya.
Tafuta maana ya jina lako. Itawezekana jina lako linatengeneza Baraka au Laana ndani ya maisha yako.
Na Kama jina lako lina maagano ya kiukoo au kikabila, au jina lako limekusababia Mabaya na matatizo kwenye maisha yako. Dawa yake ni KUOKOKA TU halafu badilisha hilo jina. Biblia inasema katika 2 WAKORINTO 5:17.
Kuna Watu wengine wanafilisika Kwa sababu tu ya majina yao yanawafilisi. Biblia inasema katika MITHALI 22:1:-" Heri kuchagua jina jema kuliko Mali nyingi ; Na neema kuliko fedha na dhahabu ".
Usikubali kuitwa jina lilo na maagano ya mababu wala Usikubali jina lenye ushetani ndani yake.
Wewe mzazi ni vizuri ukiaangalia jina zuri kwenye Biblia ili kumpa mtoto Wako. MWITE MTOTO WAKO JINA LINALOLETA UTUKUFU KWA MUNGU.
Jina la mtu ndilo litakalo yafanya maisha ya mtu kuwa jinsi yaliyo hapo baadaye. Majina Mabaya au majina yenye maana mbaya yanazuia kabisa baraka za Mungu juu ya maisha ya mtu. Naomba ufaham hilo mpendwa.
YAFAHAM MAJINA HAYA KATIKA BIBLIA NA KUYAEPUKA KUMUITA MTOTO WAKO.
Siyo kila jina lilotamkwa au kuandikwa katika Biblia lina maana nzuri. Hapana. Kuna baadhi ya majina mengine yako ndani ya Biblia lakini hayampi Mungu utukufu.
Kwa sababu hiyo tunapochagua jina katika Biblia na kuamua kuwatia watoto wetu. Ni muhimu Kwanza Asili ya hilo jina na maana yake ni nini hasa, kabla ya kulichukua jina hilo.
Kwa sababu hiyo Kwa mfano nyakati za Leo kuna Watu wengi ambao watapenda kuitwa majina haya MESHAKI, SHEDRAKI na ABELNEGO
NI muhimu tuyaangalie majina hayo ambayo watu wengi wakristo watayachukua majina hayo katika Biblia na kuitwa wewe Meshaki, yule Shedraki N. K.
Ni muhimu kufaham majina hayo Shedraki, Meshaki na Abelnego siyo majina kabisa yanayomtukuza Mungu wala kumpa utukufu.
Jina Belteshaza alipewa Daniel.
Jina Meshaki alipewa Mishaeli.
Jina Shadrack alipewa Hanania
Na Abelnego alipewa Azaria.
( SOMA :- DANIELI 1:6-7).
Hayo ni majina mapya waliyopewa na kuitwa na watu wakadayo waliokuwa ni waabudu miungu. Waliwabadilisha majina yao ya Mwanzo yaliyokuwa yanamtukuza Mungu wao YEHOVA na wakawaita majina yao mapya yaljyokuwa yanaitukuza hiyo miungu yao ya kibabeli.
(1) Jina HANANIAH. Maana yake " Yahweh is gracious". " BWANA/ YEHOVA ni mwenye neema".
Lakini walimbadilisha hilo jina wakamwita SHADRACK. Linatokana na neno >>>>" Shudur - Aku "
Na jina hilo jina maana yake " Command of Aku". Maana yake Amri ya Aku.
Huyu Aku alikuwa ni mungu wa kibabeli, ambaye alikuwa ni mungu mwezi waliyemwabudu wapangani wa kibabeli.
Leo mtu anayeitwa Shadrack hilo ni jina baya linaloitukuza miungu badala ya Mungu Aliye hai.
(2) Jina AZARIA. Maana yake ni " Yahweh has helped". " BWANA/YEHOVAH amesaidia au Mungu ni msaada wangu "
Lakini Hao wapangani wa kibabeli walimbadilisha hilo jina na kumuita jina lao jipya ABEDNEGO.
Na hilo jina Abelnego linatokana na neno" Abednergal ".
Ambalo maana yake ni " Servant of god Nebo/Nab ; Nergal ". Mtumishi wa mungu Nebo (miungu).
(3) Jina DANIELI maana yake" God is my Judge ". Mungu ni Hakimu wangu.
Lakini Hao wapangani walimbadilisha jina na kumuita Kwa jina la miungu yao Belteshaza.
(4) Jina la MISHAELI. Maana yake ni " Who is like God ". Nani kama Mungu Yehovah".
Lakini Hao wapangani wa kibabeli walimbadilisha jina hilo na kumpa jina lao MESHAKI.
Jina Meshaki linatokana na neno >>>>" " Misha - Aku". Ambalo ni "Who is as Aku is".
Maana yake " Nani aliye kama mungu Aku".
Huyu Aku ni jina la miungu ya kibabeli, mungu mwezi aliyeabudiwa na wapangani wa kibabeli katika nchi ya Babeli.
👉 Kwa hiyo Leo mtu mkristo anayeitwa MESHAKI maskini hajui tu hilo ni jina la miungu. Ni jina linalomtukuza miungu badala ya Mungu Aliye hai YEHOVA
Biblia inatuonya kama wakristo tuliokolewa Kwa damu ya YESU. Majina yetu yawe na maana zuri ya kumpa Mungu wetu utukufu na sio miungu ya aina yoyote iwe ni mizimu ya kiukoo, kikabila N. K. Tusiitwe Kwa majina yao hayo.
Biblia inasema katika 📖 KUTOKA 23:13:-" Yaangalieni hayo yote niliyowaambia asema BWANA ; wala MSITAJE KABISA MAJINA YA MIUNGU MINGINE, wala yasisikizwe kutoka kinywani mwako. "
Amen.
Kama Wewe unaitwa shadrack au Meshaki na umeokoka. Ni muhimu ubadilishe hilo jina lako, liache.
Kama Wewe umepewa jina la kiukoo na jina hilo linamaana ya kuisifia miungu hiyo ya kikabila N. K.
Kama Wewe umeokoka liachee kulitumia jina hilo kabisa na ulikatae kwenye ulimwengu wa roho. Maana majina kama hayo yanakufanya jina lako lisiandikwe mbinguni hata kama umeokoka. YESU hawezi kulikiri jina lako hilo mbinguni (UFUNUO 3:4-5; UFUNUO 21 :27).
Na Kwa sababu hiyo Badilisha jina lako sasa mpendwa . Na Chagua JINA JIPYA lenye maana ya kumpa Mungu utukufu. Kama ilivyoandikwa UFUNUO 2:17:-" Yeye aliye na sikio na Alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya Ile Mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo LIMEANDIKWA JINA JIPYA asilolijua mtu ila yeye anayelipokea ".
Ameen
MUNGU AWABARIKI WOTE Kwa neno la ujumbe huu. Mbarikiwe
Ni miye ,
Mtumishi wa Mungu, Mwalimu Odrick (0759 386 988 ; 0717 591 466). 📚➕📖
******************************