Thursday, February 15, 2018


UWEZA WA MUNGU.KATIKA MAISHA YA WAAMINI.

"Sauti ya mtu aliaye Nyikani,Itengenezeni njia ya Bwana,Yanyosheni Mapito yake.

Kila Bonde litajazwa na kila Mlima na kilima kitashushwa,palipo potoka patakuwa pamenyoka.

Na palipoparuza patalainishwa. Na wote wenye Mwili watauona Wokovu wa Mungu"

 ( Luka 3:4-6).

Mpenzi Rafiki Wa Mungu,Nakutakia Neema,Amani,Upendo Viwe Juu yako.

Nimatumain yangu na imani Yangu kwako kwamba Mungu ameendelea kujifunua na kujidhihirisha katika Maisha Yako. Nakuombea Ujazwe na Roho Mtakatifu. Ubadilishwe nia yako. Na matanio Yako kwa Mungu akujibu.

Naomba Roho Mtakatifu Akufundishe,Akushauuei na akuongoze Njia. Na akupe Nguvu. Kadiri Unavyozidi kuusoma ujumbe Moto Wa Roho Mtakatifu uwake ndani Yako. Usawazishe milima,Usawazishe Mabonde,Uondoe Na kuteketeza hila za ibilisi Maishan mwako. Amina.

Sasa turudi kwenye Somo. Letu. Somo La Leo Mwinjilist Yohana,Mbatizaji anatueleza uwezo Na nguvu za Mungu. Upitao Fahamu na akili za Wanadamu.

Mungu anaweza kutenda yasiyo wezekana kwa Wanadamu,Yasiyo elezeka kwa akili za Wanadamu.

Akili za Mwanadamu zinapoishia kufikiri,Zinapoishia kuwaza,Nguvu za Mwanadamu zinapoishia Ndipo Mungu Anapoanza Kufanya kazi. Ukisurender yote kwa Mungu ndipo utakapo uona ukuu wa Mungu maishani Mwako.

Mwinjilist huyu Wa KimataifaYohana Mbatizaji ,Anatuambia Ili Mungu aweze Kuporomosha milima Yetu. Lazima Tufanye kazi na kufuata kanuni na Sheria za Kiroho. Ambazo ni.

A. Kutengeneza Mapito Yetu. Ni kutengeneza Njia Ya Bwana.

Mfano Rais hawezi kwenda na msafara wake sehemu ambayo hakuna maandalizi,hakuna njia hakuna Usafiri. Au kunausafiri lakini maeneo hayo hayana usafi, Rais hawezi kuketisehemu hizo.

Ndivyo ilivyo Kwa Mungu wetu Yesu Kristo. Hawezi kupita sehemu Chagu,Sehemu isiyo na Maandalizi. Lazima Tutengeze uhusiano Wetu na Mungu,Lazima tutubu ,Tuache Njia zetu mbaya. Tumrudie Mungu kwa Toba na kuamini Uwepo Wake Mungu. Ndipo Miujiza itakapo tujia. Na kutufuata milele.

Baada ya kunwalika Yesu Kristo Maishani Mwetu. Uwepo Wa Mungu unaanza kututengeneza Sisi. Utaona hamu ya Dhambi inaondoka,Ufahamu unakujia,Uwepo wake Unakufunika,Uwepo Wake unakujaza nankukupa amani Ya ajabu. Palipo Mungu ,Palipo Roho Mtakatifu pana Uhuru maana hakutakuwa na milima,Hakuta kuwa na magonjwa,Shoda na mashaka. Hata kama utapiyia hayo utakuwa na amani ,furaha na mafanikio tele.

Hapa ndipo Penye Shida sana,Wengi tunapenda kuona Milima ,shida ,mateso,umaskini Ukiongezeka,magonjwa yakiondoka lakini Hatupendi Kufuata kanuni,hatupendi kulipa Gharama za kuondoa hiyo miujiza. Wengi tunapenda kuishi kwa Imani,Ila hatupendi kulipia gharama za Maisha hayo ya Imani. Ni kujikana,kufunga ,kuomba,kutoa sana tena kwa Wingi na kwa imani,Kukesha katika kusoma na kutafakari Neno la Mungu. Haya hatupendi kuyafuata.

Na Ndio Maana Tunafuatana Na kujaa katika Makanisa na.kwa manabii wa pokea ,pokea pokea kwa jina la yesu. Amka Acha Uvivu Muda wa Kulala umeisha

Mwisho Mwinjilist huyu Yohane Mbatizaji Anatuambia Na Wote Wenye Mwili hatauona Wokovu Wa Mungu.

Mara Nyingi Katika Shida pasipo Imani Huwezi kuuona thamni Ya Wokovu. Huwezi kujua raha ya kumtumaini Mungu. Huwezi Kuamini Kama Kumtegemea Yesu Kuna Raha sana. Ila Baada ya kuanza Kutumia imani Yako. Unaamuru Mvua Inasimama. Na wewe unapita ukifika Nyumbani Unaiamuru inyeshe na inanyesha.

Unanjaa nyumbani unaamuru Mungu akuletee unga maraa paap unaona Watu wanakuletea Pasipo kuwalazimisha. Hapo ndipo utakapo Msifu Mungu,utakapo muabudu Mungu. Ndipo utakapo pata Kulithibitisha neno La Nitakulisha Daima na kukushibisha kwa Miaka mingi.( Zab91:14-15)

Ushauri Wa Bure Naomba nikushauri Jambo Jifunze kutembea kwa Imani Yako binafsi,Jenga Mazoea ya Kujiombea ,na Kuwaombea Wengine daima. Weka ratiba za kulisoma neno kwa Mfululizo ,Soma vitabu Vingi vya kiroho na Vya kimaisha ili Kupata ufahamu Mpya,mawazo Mapya. Hakika hautakuwa vile ulivyo kuwa.

Mungu Akubariki,Mungu akuinue zaidi Na zaidi. Unapotumia Muda mwingi Katika Kumwadhimisha Yeye Aliye mtakatifu sana,Atukuzwe Mungu Baba,Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu Milele Na Milele.

Nakuomba Ombea Nchi Ya Tanzania,Ombea Watumishi Wa Mungu Duniani kote,Ombea Wachungaji,Wainjilist,Ombea Manabii,Mitume,Waimbaji wote.

Naomba kwa unyenyekevu Ombea Uchaguzi Wa Tanzania Wa Mwaka 2019/2020. Ombea Amani Iwepo,Ufahamu ukawafunike kw akila Mtanzania. Ombea Mungu Atuonyesha Kiongozi Anayestahili,sio Anaye stahili kwa Chama fulani.

Wenu Katika Utumishi wa Yesu Kristo.

Punda Wa Yesu Kristo.

Wednesday, February 14, 2018


GHARAMA YA KULIPA ILI UTEMBEE NA MUNGU (Somo Na Mwl M, Mwambeso)
🔹Watu wengi sana wanapenda kutembea na Mungu katika maisha yao, na hicho ni kitu kizuri sana, lakini ni watu wachache sana ambao wanaelewa gharama wanayotakiwa kulipa ili wafanikiwe katika jambo hilo.

🔸Mungu anapenda kuona watu wake wanatembea pamoja nae kama walivyofanya wakina Henoko, Ibrahimu, Daudi n.k, lakini ana kanuni zake ambazo watu wake wanatakiwa kutembea nazo kila wakati.

🔹Kanuni kubwa ni kufanya mapenzi ya yake (yaani mapenzi ya Mungu) katika maisha yako. Yesu alisema kwamba Baba yake alikuwa pamoja nae siku zote na wala hakumuacha kwasababu tu alikuwa anafanya yampendezayo (mapenzi ya Baba yake), Yohana 8:29

🔹Unapotaka kufanya mapenzi ya Mungu na kutembea pamoja nae katika maisha yako, unatakiwa kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo;

*1. LAZIMA UKUBALI KUMPA MUNGU NAFASI YA KWANZA KATIKA MAISHA YAKO.*

Unatakiwa kumpa nafasi ya kwanza katika kila eneo la maisha yako.
Nafasi ya kwanza kwenye moyo wako,nafasi ya kwanza kwenye uchumi wako, wokovu wako, utumishi wako, ndoa yako, nafasi ya kwanza kwenye muda wako, nafasi ya kwanza kwenye mipango yako n.k.

*2. LAZIMA UWE NA UTAYARI WA KUFANYA CHOCHOTE NA KWA MUDA WOWOTE.*

Tarajia kwamba wakati mwingine Mungu atakutaka ufanye vitu ambavyo havikuweko kwenye ratiba yako.

Anaweza akakuambia ingia kwenye maombi ya kufunga wakati wewe haukupanga, anaweza akakuamsha usiku kumuombea mtu wakati wewe ulitaka kulala, n.k. Unahitaji utayari wa wa hali ya juu sana vinginevyo utashindwa kutembea nae. (2Timotheo 4:2)

*3. LAZIMA UKUBALI KWENDA KINYUME NA MILA NA TAMADUNI AMBAZO ZIKO KINYUME NA NENO LAKE.*

Huwezi kutembea na Mungu wakati mila na tamaduni zingine unazozing’angania haziendani na neno lake, mfano ibada za wafu, matambiko n.k.
Vitu ambavyo viko kwenye jamii yako na yeye havipendi lazima ukubali kuviacha. (1Wakorintho 10:23)

*4. LAZIMA UWE TAYARI KUTEMBEA KWENYE MAJIRA YAKE.*

Hili sio jambo jepesi, na linawafanya watu wengi wapishane na muda wao wa kuinuliwa na Bwana/muda wa kujiliwa na Bwana/Appointed time.

Yanaweza yakawa ni majira ya kuoa au kuolewa, majira ya kuanza utumishi n.k.
Shida kubwa inayokuja hapa ni kwamba sio rahisi sana wanadamu wakakuelewa, kwa hiyo unazungukwa na hofu, na kuogopwa kutengwa.

*5. LAZIMA UTAFUTE KIWANGO KIKUBWA CHA IMANI.*

Kutembea na Mungu kunahitaji Imani zaidi, kwasababu wakati mwingine hutajua anakupeleka wapi.

Angalia mfano huu, halafu utaelewa kiwango cha imani ambacho kilikuwa kinahitajika, _Mwanzo 12:1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha._

Huo ulikuwa ni mtihani mgumu saa kwa Ibrahimu ingawa alifaulu.
Sijui ukiambiwa neno kama hilo na Mungu utajiuliza maswali mangapi moyoni mwako! Na utachukua uamuzi gani!

Pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6).

Hata kwenye maisha ni vigumu sana kuambatana na mtu kama humwamini.

*6. UNAHITAJI UNYENYEKEVU.*

Unyenyekevu ni wa muhimu sana ili uweze kutembea na Mungu katika maisha yako.

Mungu mwenyewe asema kwamba anaketi pamoja na mtu aliyetubu na kunyenyekea (Isaya 57:15).

Yakobo 4:6 … Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.

*7. UNAHITAJI UTII*.

Jambo la utii wa mtu ni la muhimu sana kwa Mungu kuliko sadaka zake(1Samweli 15:22)

Mungu anaupa utii nafasi kubwa sana kuliko sadaka.

Utii ni mlango mkubwa sana sana wa mtu kufanikishwa na Bwana (Isaya 1:19, Kumbukumbu la Torati 28: 1-13).

Kukosekana kwa utii huleta laana (Kumbukumbu la Torati 28: 15-68).

Kwahiyo ukitaka kutembea pamoja na Mungu, unahitaji roho ya utii wa hali ya juu na kutambua kuwa yeye ni boss na hivyo unatakiwa kumtii badala ya kusimamia misimamo yako. Tii anachokuambia kila wakati, ndio mtaenda pamoja.

*8. LAZIMA USHUGHULIKIE ROHO YA MAZOEA KWA MUNGU WAKO.*

Hiki ni kitu muhimu sana sana, kwasababu kadri unavyozidi kuwa karibu nae ni rahisi ukaanza kumzoea.

Hata kwenye maisha ya kawaida, kadri unavyozidi kuwa karibu zaidi na mtu ni rahisi ukajikuta heshima yako kwake inapungua, na unaanza kumuona ni wa kawaida sana.Hili jambo lilimgarimu Nabii Musa.

Angalia watu wengi ambao wameokoka, kadri wanavyozidi kukaa kwenye wokovu, wanajikuta wameanza kutembea kwenye wokovu kwa mazoea.

Pia angalia watumishi wengi (waimbaji, Wahubiri n.k, utagundua kuwa kadri wanavyozidi kutumika ndipo wanapoanza kutumika kwa mazoea na kutumia uzoefu wao badala ya kumtegea Roho Mtakatifu.

*9. LAZIMA UAMUE KUICHUKIA DUNIA NA MAMBO YAKE MAOVU.*

Ukitaka kuambatana na Mungu kwenye maisha yako ni lazima uamue kuyachukia mambo maovu ya dunia hii (Yakobo 4:4).

Mungu anachukia sana sana dhambi, ndio maana pamoja na kwamba Daudi alimpenda sana na alikuwa rafiki yake, lakini alipofanya zinaa na mke wa mtu alimkasirikia sana na hakumuacha bila adhabu.

*10. LAZIMA UWE TAYARI KUBEBA LAWAMA KUTOKA KWA WANADAMU NA KUKATALIWA NA KUDHARAULIWA WAKATI MWINGINE.*

Ukitaka kumpendeza Mungu na kutembea pamoja nae, ni lazima utambue kuwa muda mwingi wanadamu watakupinga sana, na utakataliwa na watu ambao wakati mwingine haukuwategemea.

Ndio maana watu wengine wakiokoka wanatengwa na ndugu zao, wengine wanaacha kusaidiwa na ndugu zao.

Unaweza ukakataliwa na kusemwa vibaya na wazazi wako, mke/mume wako, rafiki zako, watumishi wenzako, wafanyakazi wenzako n.k.
Yesu mwenyewe alipokuja duniani kufanya mapenzi ya Baba yake, alikataliwa na ndugu zake kabisa (Yohana 1:11).

Kwahiyo maeneo mengine ukikataliwa na kusemwa vibaya, usikasirike sana na kuharibu uhusiano wako na Mungu, kwasababu hata Mwokozi wetu Yesu alifanyiwa hivyo. Mtume Paulo alikataliwa, Daudi alikataliwa, Yusufu alikataliwa n.k

Jambo la muhimu kwako, ni kuendelea kusimama pamoja na Mungu wako na Imani yako. Shetani huwa anatumia watu ili kuharibu uhusiano wako na Mungu wako.

Bwana Yesu akubariki na azidi kukuongoza katika maisha yako,na ninaamini hili somo litakupa hatua mpya.

*ZINGATIA*: Ni vigumu sana ukayaweza mambo yote hayo kwa wakati mmoja,hivyo anza taratibu, jambo moja baada ya jingine. Mtegemee zaidi Roho Mtakatifu ili akusaidie kutembea kwenye hizo kanuni. Tamani sana awe rafiki yako na mshauri wako wa karibu.

🔹Washirikishe watu wengine mafundisho haya.

*Na Mwl M, Mwambeso*
0752 197065, 0784 136 816
Email: mwambeso80@gmail.com

Saturday, February 3, 2018

MEZA YA BWANA

MADA: "MEZA YA BWANA"

A. UTANGULIZI

"Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.

Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake." (Yohana 6:54,55&56)

B.LENGO/MAANA YA MEZA YA BWANA

Meza ya BWANA siyo msosi ama kinywaji tu; inayo maana na tafsiri ya kiroho:-

(i) Kuthibitisha USHIRIKA naye; yuko ndani yako nawe uko ndani Yake
(ii) Kutangaza mauti yake na kufufuka kwake, yeye ni UFUFUO
(iii) Kukiri kwamba WOKOVU unapatikana Kwake; yeye ni Njia,Kweli&Uzima

TAHADHARI: "Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana." (1 Wakorintho 11:27)


MTU AFANYEJE: "Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe." (1 Wakorintho 11:28)

USHIRIKI: Kula na kunywa tu kusikoendana na TAFAKARI ama MUKTADHA huo wa a MAANA ama LENGO la "Meza ya Bwana", huko ni sawa na kula na kunywa MKATE NA MVINYO kama viburudisho; ukifanya hivyo Kanisani unakuwa UNAKOSEA, wajitwalia HATIA, nenda ukafanyie KWENU ama MNAKOKUSANYIKIA kunywea na stori za hapa na pale

Paulo akahoji:
"Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya hili? La, hasha." (Wakorintho 11:22)

NB: Kuhusu kiwango mtu anywe ama kula, aina ya kinywaji ama mkate ubora wake, makanisa mengi yamedhibiti leo(mkate umachovywa tu ama kakipande kadogo na kamvinyo kadogo- wenzetu Wakorintho walilifanya KIHOLELA sana hadi hadi "MATABAKA" yalijidhihirisha,Paulo akahoji hivyo.

C. HITIMISHO

"Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu." (Luka 22:19&20)

Aliposema hayo hakumfukuza YUDA ingawaje aliijua nia yake baada ya kuingiwa na Shetani, akashiriki naye "meza ya BWANA".

Martin Kidenya (mwandishi)

Monday, July 24, 2017

AMINI NDIPO UONE
(Mch. Remmy Kyaruzi, Pentecostal Salvation Assemblies of God-Kitunda, Jumapili 23 July 2017)
Mungu amekuwa akinifunulia juu ya uhusiano uliopo kati ya Kuamini na Kuona kile unachokiamini. Na iwapo hautaamini, itakugharimu sana kupokea. Asubui ya leo tumejifunza somo la Mch. Jackson juu ya Abramu, na nimejiuliza kwanini Abramu aliadhibiwa kwa uzao wake kupelekwa utumwani Misri, lakini kwa hakika ni kutokana na Abramu kutaka kuona badala ya kuamini tu.

Nachelea kukwambia iwapo hautaamini itakugharimu sana kupokea. Na inawezekana hata ukapata madhara.

Habari katika Yohana 20: 24 – 29, inahusu kutokuwamini kwa Tomaso baada ya kuambiwa na wenzake kuwa “Tumemwona Bwana”. Jambo la kujiulize ni kwanini Tomaso hakuwepo ktk kusanyiko Yesu alipowatokea.

Tomaso alikaa na Yesu, alimwona Yesu akifanya miunjiza na ishara nyingi za kufufua wafu, kuponya magonjwa na kufungua waliofungwa. Naamini Tomaso alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kumuamini Yesu zaidi yako. Inawezekana Tomaso baada ya Yesu kukamatwa alikimbia moja kwa moja na alirudi baada ya kusikia habari za ufufuko. Akaja anachungulia na pasipo Imani akaanza mabishano yanayodhihirisha kule kutokuamini kwake.

Shida ya Imani ya Tomaso haikuwa kutokumuona Yesu, bali hata akimuona bado hataamini mpaka aguse kovu za misumari na bado hata hakiona kwa macho hizo kovu hataamini mpaka atie mkono wake katika ubavu (vv 25).

Wokovu wetu tulionao siyo kwa sababu tulimwona Yesu au kumgusa, bali ni kwa sababu tuliamini tu neno lake. Yesus anasema tu heri. Iwapo Imani yako ipo kwenye kuona, kuoja, kunusa, basi wewe hauna Imani. Na asubui ya leo, mwombe Mungu akupe uwezo wa kuamini moyoni mwako ahadi zake.

Sharti la Tomaso linaleta maswali mengi ya kufikirika katika Imani yetu. Madharani, Mungu angemfufua Yesu bila kuwa na KOVU lolote katika mwili wake. Tomaso hata baada ya kumuona Yesu asingeamini. Ina maana Tomaso alikaa zaidi ya siku 8 baada ya Yesu kufufuka bila Tomaso kuamini bila Ufufuko wa Yesu. Inaoneka kama vile Yesu alikuwa na huruma sana kuangaika na Tomaso mpaka aamini. Ikambidi arudi tena safari hii, vinginevyo agefukuziwa mbali kama Yuda msaliti.

Usijiwekee Mipaka katika kumuamini Mungu. Mungu anasema, wanitafutao kwa Bidii wataniona. Endelea kufanya bidii kumtafuta ili uweze kumwona Mungu. Yesu anatafuta jidhirishe kwako kwam alivyoshughurika na Tomaso tu mpaka aakamini. Vinginevyo roho ya kutukuamini ingewapata mitume wengine.

Ukimkuta mtu anajenga, tambua nyuma yake anaomchoro wa nyumba, ambao ulitokana na mchoraji anayeitwa Architecture. Architecture pia anakuwa anachora kulingana na mawazo unayomweleza. Mungu kabla hajaumba, aliwaza kwanza, baada ya hapo akaumba.

Mara zote nimekuwa nikikufundisha kuwa endapo unataka kuendelea lazima uwe na wazo unalotaka kulifanyia kazi. Watu wanaosubiri kuona huwa hawafanikiwi, ama wakifanikiwa ni kwa kuchelewa sana.

Baadhi ya mitazamo katika kuamini jambo:
Jambo la Msingi1: Mtazamo wa kutilia shaka kile ambacho Mungu ameaidi katika maisha yao. Yesu alikuwa amewaambia wanafunzi wake kuwa atafufuka siku ya 3. Wanafunzi walitilia shaka. Baada ya kufufuka waliendelea kumtafuta makaburini (Lk 24:5-13). Hata leo bado kuna watu wanaenda Israel kuliangalia kaburi la Yesu.

Jambo la Msingi1: Mtazamo wa kuondoa thamani ya Shuhuda za watu wengine.Tomaso hakuwa tayari kuamini maelezo ya wanafunzi. Mtu akija akakushuhudia jambo zuri la mafanikio, nachofanya ni kulitilia shaka. Tunaishi kwa mashaka katika kila jambo linalotujia mbele yetu. Mambo ya imani hata lisilo la Imani na matokeo yake hatuendelei.

Jambo la Msingi3: Mtazamo wa kulazimisha kuona ndipo uamini. Iwapo unayo mashaka Mungu atakuadhibu. Jamii ya Nuhu haikuamini juu ya gharika kwani walitaka waone kwanza mvua ndipo waingie katika safina (Ebr 11:6-7).

Kuhani mkuu, Zakaria pamoja na kuingia patakatifu pa patakatifu, akiwa na maombi yake kwa Mungu, bado alikuwa na mashaka alipoletewa majibu wa maombi yake (Lk 1:11-18. Alendelea kusisitiza nitajuaje jambo hili (vv 18).

Endapo ahadi za neno la Mungu ni kuwa Mungu atakulinda, atakuponya, atabariki kazi za mikono yako, wewe amini tu. Sema kama Bikira Mariam, “na iwe kwangu kama ulivyosema” (Lk 1: 38).

Tuna jambo la kujifunza kupitia Teknolojia ya mawasilano ya simu na TV. Tunaweza kupewa maelekezo na tukayaamini tu na hata kuchukua tahadhari katika madhara yake. Tambua mara zote kuwa Imani ikiisha kuonekana na kuwa dhahiri kwano, siyo Imani tena.

Mtume Paulo katika 1Kor 2:6-9, atuonya juu ya Imani yetu. Na inawezekana kutumia Elimu na Uzoefu, kukakupelekea kutokuwa na Imani. Imani ni Mambo ambayo hayakuyaona. Imani ni juu ya mambo ambayo Masikio hayakuyasikia. Kwenye Imani, Macho hayaoni kwani yamefundishwa kuona mambo yaliyodhahiri na Masikio hayasikii kwani yamefundishwa Kusikia vitu vinavyotoa mlio. Sasa kwenye Imano, tofauti ni kuwa Moyo tu ndio unaoona na kusikia visivyoonekana kwa macho na masikio ya mwili. Ni kwambia kitu, ukichukua hatua ya Imani, n kuanza kujishughurisha na jambo lolote, ndo unaanza kuona. Kama unatafuta kiwanja unaanza kuulizia madalali na wanaanza kukuonyesha. Kama ni kujenga, unaanza kuangalia nyumba zilivyo jengwa au kuezekwa, kama ni kununua gari, inaanza kuona aina tofauti za magari, unaanza kuulizia bei, unaanza kuulizia mikopo, nk, nk.

Ukifiria juu ya kutafuta baraka za Mungu, anza kuinua Imani yako>

Habari ya Elisha na Mtumishi wake katika 2Falm 6:15-17, inatupa mwanga juu ya kuwa na macho ya roho na kujua mambo ya sirini. Lakini inatuonyesha juu ya hadhari za kuwa na macho ya mwilini tu. Wakati wetu huu, hatuombi ili Mungu atufungue macho yetu kuona kama mtumishi wa Elisha, bali tuweze kutembea katika Imani.

Ni maombi yetu kwa Mungu, kama wanafunzi wa Bwana Yesu, “Tuungezee Imani” (Lk 17:5). Mungu akuzidishie Imani yako ili usiwe kama Tomaso katika maisha yako ya kiroho na mwili.

Amini Ndipo Uone. Shalom.

Sunday, July 23, 2017

KUTUNZA UTUMISHI WAKO
(Mch. Jackson, PSAG-Kitunda, Jumapili 23 July 2017)
Utumishi ambao Mungu ameweka ndani yako ni wa thamani sana. Mungu amekutoa katik vitu vingi vya ki dunia na kukuleta katika Wokovu kwa neema. Somo ili linalenga kukumbusha kutunza wokovu wako kwa gharama kubwa.
Kitu kikiwa cha thamani lazima kitunzwe vizuri. Mathalani, ukiwa na nguo yako kama Suti, ukiipeleka kweye kazi ya kubeba zege, baadae ukiiva na kuja nayo Kanisa kila mtu atakushangaa ilivyochafuka, hata wewe mwenyewe hautaitamani. Ndivyo ilivyo kwa Wokovu wako uliofanyika kwa Agano la Damu ya Yesu msalabani.
Mwanzo 15:8 – 13, unajifundisha juu ya dhamani ya Sadaka na Madhabahu unayomtolea Mungu Sadaka yako.
Unaposoma habari hii, unakuta moyo wa Imani ya Abramu kwa kumwamini Mungu na kupokea ahadi kwa uzao wake kurithi nchi. Mungu na Abramu wanakubaliana kudhibitisha Agano hili kwa Sadaka yenye dhamani kubwa (vv 8-9). Sadaka hii ilikuwa ni ya dhamini sana.
Kwenye Sadaka hii ndo kulikuwa na Ahadi zote za Mungu kwa Uzao wa Abramu. Abramu akawa mwaminifu katika kutoa hiyo sadaka na kuilinda dhidi ya ndege aina ya Tai wasiiguse. Lakini baadae alichoka na akapitiwa na usingizi (vv 12). Abramu aliingia pia katika hofu ya giza badala ya kuenedelea kumwamini Mungu.
Wewe na mimi wakati mwingine ni kama Abramu, tunazo ahadi za Mungu katika maisha yetu na Mungu ameweka agano lake kwetu, lakini unakubana na changamoto mbali mbali za kukurudisha nyuma na kusahau dhamani ya utumishi wako. Kumbuka Mungu anasubiri aone uvumilivu wako ili aweze kuachilia udhibitisho wa agano la baraka zake.
Je, uko tayari kuendelea kuwa macho na kuwafukuza Tai na hofu ya giza la usiku? Unawa kwa Neema ya Mungu kwa kushinda yafuatayo:-
1. Kuchoka:
Mwili wake ulichoka kama ulivyochoka wewe kuendelea kutunza wokovu na utakatifu wako. Yesu alipoenda kuomba kilichowakuwata ni uchovu. Ninakukumbusha leo kuwa Mwili ni Dhaifu (Mt 26:41). Usiruhusu uchovu wala kupoa kiroho. Usichoke maombi, usichoke kufunga, usichoke Ibada, usichoke uimbaji. Ni vya dhamani sana kukufikasha kwenye ahadi za Mungu.

Neno la Mungu linatuonya kuwa Mwili ushindana na Roho (Gal 5:16 – 17). Uchovu wa Mwili ulipeleka uzao wake utumwani miaka 400. Ukiruhusu Uchovu, sijajua utapelekwa utumwani miaka mingapi, sijajua utatanga tanga kwa kiasi gani, sijajua utashambuliwa na magonjwa mangapi na kwa muda gani. Shinda uchovu wa kiroho
Ndani yako Mungu ameweka Wokovu na Utakatifu. Neno linasema shika sana uilicho nacho, kwani aduai anataka kukipokonya (Ufu 3:11). Mwili wako sikuzidi ujuzi au kukupelekesha. Ukikosa wokovu Mungu anakuwa mbali nawe na hata maombi na ahadi zako kwa Mungu azikufikii tena (Isa 52:2).
2. Usingizi:
Mtu akisinzia anaanza kuota na anapoteza ufahamu. Neno la Mungu linasema Kesheni, si kwamba usilale kabisa bali uwe macho kiroho. Na ukiwa macho kiroho unakuwa makini na kupima athari zinazoweza kukupata. Yesu alionya juu ya kulala usingizi alafu adui akapanda magugu (Mt 13:24-25).
Mbegu wa Wokovu wako ilipandwa kwa Neno la Mungu na halibunguliwi. Adui yako, shetani au Ibilisi ukilala anapanda mbegu ya magugu. Unapookoka unapokea  nguvu ya kiroho na kufunuliwa mambo ya rohoni.
Kanisani kuna watu wa aina 3:
a. Wanaokua: Kundi ili linapigana kuendelea na wokovu na kumjua Mungu zaidi. Mungu anawatumia na kuachilia baraka zake kwao.
b. Wanaodumaa: Kundi ili ni wajuaji au wasikilizaji tu wa neno. Hawachukui hatua na kulitii neno wala kulisikiliza ili walitendee kazi. Kila kitu ni kawaida kwao, hawafungi, hawaombi, hawaji au kuwai kuwai Ibada. Wanazoelea Neno la Mungu na wokovu.
c. Wanauorudi nyuma: Wakuwa na bidii ya muda alafu baada ya muda wanarudi nyuma na kuacha vitu vya msingi.
Adui anachotafuta ni kupanda magugu. Usikubali adui akushinde akutege. Usikubali kupote tiketi yako. Mshitaki wako Ibilisi anakutafuta (1Petro 5:8-9). Lakini ashukuruiwe Mungu maana anatuonya kulinda mioyo yetu (Mithali 4:23). Mwimbaji wa nyimbo za Injili, King Victor anasema “Wokovu moyoni, Akili Kichwani, na Pesa Mfuko”.

Kutunza Utumishi Wako. Shalom.

Friday, July 21, 2017

MAOMBI YA SHABAHA (Mch. Jackson,PSAG Ijumaa Mkesha, 21/07/2017)

Haya ni Maombi ya Kumaliza mambo yanayosumbua maisha yako. Unakuwa na hasira dhidi ya shetani na Hasira ya ki Mungu inakupa nguvu ya kushinda kupitia Maombi.

Ktk medani za kuvita, Askari ufundishwa kutumia siraha za aina mbali mbali. Ufanyishwa mazoezi ya kulenga Shabaha na kujifunza sehemu ambazo ukimpiga shetani atakufa.

Kwenye uwanda wa vita pia anayetafutwa mara zote ni Kamanda (kingozi wa vita) wa Vita. Kwani yeye ndo anapanga mashambulizi. Ukimuua Kamanda askari wote wanakimbia. Daudi alilijua hilo, alipoenda kwenye uwanda wa Vita alimtafuta kamanda Goliathi. Baada ya kuuwawa, Jeshi lote la Wafilisti lilikimbia na kuuwawa. Ujitaka kukata mti, anzia kwenye mizizi.

Mifano ya Maombi ya Shabaha yenye Manufaa zaidi ya moja:
1. Kufufuliwa kwa Lazaro: Yoh 11:38-45
Kusudio la Maombi ya Maombi ya Yesu ni ili Lazaro afufuke. Na kweli Lazaro alifufuka akawa mzima.
Lakini ni zaidi ya hapo.  Kusudio la pili ni Kudhihirisha Utukufu wa Mungu (mst. 41-42).

Mungu anapojibu maombi yake, yale majibu yanamletea kwanza Yeye utukufu kabla yako. Maombi yanapojibiwa ni ili watu wengine wabarikiwe kupitia wewe. Kupitia kazi yako, biashara yako, mafanikio yako, ushindi wako, Mungi anatakiwa atukuzwe kwanza, ufanyike baraka kwa watu wengine, then wewe unufaike.

2. Daniel kutafsiri Ndoto (Dan 2:14-46):
Japo kuwa Daniel alifunuliwa siri ys  ndoto ya Mfalme (vv19) kupitia maombi, tunaona faida zake nyingi: Kuijua ndoto na tafsiri yake; Kutouwawa kwa wenye hekima (vv24), Kumtambulisha Mungu wa kweli (vv 47).
Maombi yako yanamtambulisha Mungu wa kweli, wachawi wanakimbia, maadui zako wanatamtukuza Mungu wako.

Siku moja nilikutana na majirani zangu wamembeba binti yao aliyepagawa mapepo, wanaume kama 4 hivi. Nikauliza kulikoni, wakasema binti anapiga ngumi na mateke kama Tyson. Ikabidi nisaidie, na ktk ile purukushani, yule binti akanipiga kibao cha uso. Maumivu yale ya kibao kile, ndipo nikatambua shetani amenipiga, na ulokole wangu, kwa hasira nikasema "acheni nimwombee". Nilipo mwekea mkono kwenye paji la uso na.kuanza kukemea kwa Jina la Yesu, watu wote wakamweka chini na kuniachia peke yangu. Nikapambana naye huku nikikemea kwa nguvu zote. Ghafula yale mapepo yakakubali kumwachia. Mara yule binti ufahamu ukalejea, akaanza kuvaa nguo zake vizuri na kuona aibu. Wale ndugu wakashangaa (japo waliendelea kugangania Imani yao), na Mungu wangu alitukuzwa.

Tunaye Mungu ndani yetu mwenye uwezo, tuna Mungu asiyeshindwa wala kubadilika. Na ni Mungu ambaye ujitukuza kupitia sisi.

Shalom.

Tuesday, July 18, 2017

USIOGOPE VITA (Mch. Remmy, PSAG The House of Vision, DSM 09/07/2017)

Ushujaa baada kupambana na kushinda. Ni bahati mbaya, mfumo wa Elimu ulitufanya kufikiria kushindwa na kuona ukosefu au upungufu wa vitu ktk maisha yetu, hivyo kukosa ujasiri na uhodari wa Kupambana.

Kwa bahati mbaya hata kwenye mambo ya ki Kiroho tumeambukizwa mwelekeo huo huo.
Ni maombi yangu kwa Mungu abadili fikiri za kizazi chetu na Kanisa kutoogopga Vita.

Hotuba ya marehemu Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere akitangaza vita kati ya nchi yetu na Uganda, baada ya Uvamizi wa Iddi Amina, alisema, namnukuu "Sababu tunayo, Nia tunayo, na Uwezo tunao". Hii ilikuwa ni kauli ya Jemedali Mkuu asiyeogopa Vita.

Wewe na mimi ni Majemedali na tunao Ujasiri wa kupambana na kila adui anayekuja ktk maisha yetu ya kila siku. Upo vitani, na Roho Mtakatifu abakukumbusha kupigana Vita ya Imani. Hii ni kwa sababu changamoto tulizonazo kwenye maisha yetu zinatokana na Shetani.

Katika Waamuzi 3:1-11, tunasoma habari ya kusudio la Mungu kwa Israel KUJIFUNZA VITA.

Ili kuwafundisha vita, Wana wa Israel hambao "hawakujua vita", Mungu aliwawekea mataifa 5 jirani ili wawe MAADUI.

Mpendwa, kuna vitu vinaachwa ktk maisha yako ili kukufundisha VITA. Ili uweze kuomba, kufunga, kusoma neno, ni sharti uingie ktk ugumu ili kukuchochea "kutitiliza" ili UPIGANE na Adui shetani.

Nataka ujue mataifa mengi ulimwenguni yameendelea kutokana na kupigana Vita ya Maadui wa Ndani au Nje (majirani zetu Rwanda na Uganda mfano).

Hivyo ktk suala la vita ya kiroho na ki mwili Mungu anakusudia:
1. Kukufundisha Vita: Jifunze mbinu mbalimbali za kupigana (vita ya ki roho na mwili). Tumia akili na nguvu zako zote. Vita siyo lele mama.
2. Kukujaribu kama Utatii. Askari ujiandaa ukakamavu na medani za vita wakati wa Amani. Unajenga misuli yako na Ukakamavu  wa Imani ktk maisha ya Utii kwa maisha ya Maombi, kufunga, na Neno.

Wana Israel walishindwa kujifunza Vita. Badala yake wakajiunga na Adui.

Mungu akuweka ktk ya Watu ili uwasadie (Mt 5:13-14). Tunapoza ukali na kuwa butu tunapoiga mifumo ya maisha ya dhambi ya Jamii iliyotuzunguka (kuozeana). Tunakosa kuwa chachu. Hautakiwi kulalamika kwa kukaa jirani na wachawi, walevi, na wazinzi. Ni ili tuweze kujifunza vita. Tunajifunza mbinu za ki vita za kupambana nao.

Usiache kazi kwasababu kuna watu wanakusema. Usikubali kukatishwa tamaa. Endelea na ulichokusudia kufanya. Waliokudharau watakuona juu.

Musa kuna vitu alichelewa kutambua ktk kufundishwa vita. Mungu alimpeleka kwa Farao ili afanye mazoezi ya kupambana (kiroho, kimwili). Mungu akikupelekwa mbele ya adui zako usiogope kwa amesema "nitaandaa kalamu" mbele yao.

Usikubali kushindwa. Ukisema, Ndoa yangu itavunjika, itavunjika kweli! Lakini ukiamua kupigana, hata hiyo "Nyumba ndogo" itaachia. Pigana vita "Agani na Ardhini", usitumue mbinu mmoja.

Narudia, kamwe usitumie mbinu wala Siraha aina mmoja. Hata Musa alipotumwa kwa Farao hakutumia siraha moja. Ilichukua muda Farao kuwaruhusu waondoke.

Ukisoma kitabu cha  Kutoka sura 4, Maongezi ya Mungu na Musa, yanaweza kukusaidia kujiandaa kisaikoligia, na yalimsaidia kutambua yafuatayo:
1. Tambua Fimbo uliyonayo: Musa hakutambua kama hiyo fimbo inaweza kutumika kwa Uweza wa Mungu kama siraha ya ukombozi. Kumbuka Musa alitumia Fimbo hii siku zote kuchunga Kondoo.

Mpendwa, nikukumbushe Mungu anaweza kukutumia hivyo hivyo, usijidharau. Tambua ndani yako ipo karama na uwezo wa ajabu kushinda vita!!

2. Tambua uwezo wako:
Kushinda vita kuna kunataka kutambua uwezo wako. Usisubiri watu wakuambie au kukutia moyo. Endapo hautapa mtu wa kukutia moyo utabakia hivyo.

Ongeza uweka wako,  fanyia mazoezi mambo unayoyajua. Tumia muda wako kujifunza kuimba, kupiga vyombo, ujasiriamali. Tafuta maarifa mapya ya kukukwamua kimaisha.
3. Tambua Nyakati (Timing):
Kutambua mapema adui zako, wabaya wako, wanaokuloga, upinzani, nk, ni muhimu sana. Vita huitaji kuwai au kushutukiza ili uweze kupata ushindi wa mapema.

Pia tambuacKuna vitu una uwezo wa kufanya vizuri zaidi ktk umri fulani, vinginevyo utakabiliwa na changamoto kubwa.

4. Tambua kuvaa na kuzitumia siraha za vita:
Bila siraha za kumtishia au kumpigia hauwezi shinda. Biblia imeweka wazi kuwa Nyoka na Nge havitatudhuru (Lk 10:19). Na hivyo unahitaji kutumia Mamlaka ya ki Mungu (Mk 16:17). Wakati mwingine Tumekuwa waoga muno kukemea mapepo.

Somo la kujifunza kwa tabia za ndege anayeitwa Tai:
i. Tai Uruka peke yake juu sana: Kushinda vita yako, usikubali kujiweka au kujishusha chini. Nenda sehemu ya juu

Kwa ndege, Eneo la chini lina hatari nyingi (juu sana kuna usalama na uhakika). Usikubali na watu wasiokuwa na mchango hasi kwako kimaendeleo au kimawazo.
ii. Jicho la Tai Ulenga Maono ya Uhakika:
Jicho la Tai anaporuka juu ulenga maono sahihi na akishuka uyajia hayo maono kwa kasi na nguvu. Kushinda Vita lazima uwe na Maono sawa na Mith 29 ili usije kushindwa vita au adui jukupotezea lengo.
iii. Tai hali Mizoga:
Tai utafuta mawindo yaliyo mapya (fresh). Usipigane kwa Vita kwa ajiri ya vitu dhaifu. Angaukia Vita yenye manufaa kwako au jamii yako.

iv. Tai Ufuraia Mawindo yake:
Tai yupo tayari kukabiliana na changamoto ili mwisho afuraie mawindo yake. Kwente maisha ya Vita, unachosemwa au kugombezewa kikusaidie kuboresha maisha yako na kupata mwelekeo mzuri zaidi.

v. Tai Jike upima Uwezo wa Tai Dume:
Ili uweze kushinda ktk vita, ni vizuri kupima uwezo wa kujitoa wa Marafiki zako, Mchumba,  au mdau yeyote unayeshirikiana naye iwe biashara kazi, hata huduma.

vii. Tai Ujiandaa kwa Mafunzo:
Tai kama ndege wenhine ujenga uwezo wa vifaranga kwa kuviachia toka juu ili kuvifundisha kuruka kwa mbawa zao wenyewe.
Unahitaji kuwafundisha/kuwajengea uwezo Watoto wako ( kuwinda, kuruka, kutafuna) kujitegemea. Waondoe kwenye kujiona huru (confort zone).
vii. Tai akikua ujijerui ili kujiuisha:
Tai kama vile Nyoka anavyojivua gamba, akifikia Umri fulani makali ya Mdomo na Kucha zake uisha na Manyoya yake upungua. Utumia nguvu nyingi na Maumivu makali kuondoa mdomo, kucha na manyoya ya zamani.
Kadiri maisha yako ya ki Roho na mwili  unaweza kupungua nguvu, kupata maradhi na udhaifu tofauti tofauti. Unaihitaji kujijerui ili kujijenga upya.

Shalom.
Kyaruzi