MAOMBI YA SHABAHA (Mch. Jackson,PSAG Ijumaa Mkesha, 21/07/2017)
Haya ni Maombi ya Kumaliza mambo yanayosumbua maisha yako. Unakuwa na hasira dhidi ya shetani na Hasira ya ki Mungu inakupa nguvu ya kushinda kupitia Maombi.
Ktk medani za kuvita, Askari ufundishwa kutumia siraha za aina mbali mbali. Ufanyishwa mazoezi ya kulenga Shabaha na kujifunza sehemu ambazo ukimpiga shetani atakufa.
Kwenye uwanda wa vita pia anayetafutwa mara zote ni Kamanda (kingozi wa vita) wa Vita. Kwani yeye ndo anapanga mashambulizi. Ukimuua Kamanda askari wote wanakimbia. Daudi alilijua hilo, alipoenda kwenye uwanda wa Vita alimtafuta kamanda Goliathi. Baada ya kuuwawa, Jeshi lote la Wafilisti lilikimbia na kuuwawa. Ujitaka kukata mti, anzia kwenye mizizi.
Mifano ya Maombi ya Shabaha yenye Manufaa zaidi ya moja:
1. Kufufuliwa kwa Lazaro: Yoh 11:38-45
Kusudio la Maombi ya Maombi ya Yesu ni ili Lazaro afufuke. Na kweli Lazaro alifufuka akawa mzima.
Lakini ni zaidi ya hapo. Kusudio la pili ni Kudhihirisha Utukufu wa Mungu (mst. 41-42).
Mungu anapojibu maombi yake, yale majibu yanamletea kwanza Yeye utukufu kabla yako. Maombi yanapojibiwa ni ili watu wengine wabarikiwe kupitia wewe. Kupitia kazi yako, biashara yako, mafanikio yako, ushindi wako, Mungi anatakiwa atukuzwe kwanza, ufanyike baraka kwa watu wengine, then wewe unufaike.
2. Daniel kutafsiri Ndoto (Dan 2:14-46):
Japo kuwa Daniel alifunuliwa siri ys ndoto ya Mfalme (vv19) kupitia maombi, tunaona faida zake nyingi: Kuijua ndoto na tafsiri yake; Kutouwawa kwa wenye hekima (vv24), Kumtambulisha Mungu wa kweli (vv 47).
Maombi yako yanamtambulisha Mungu wa kweli, wachawi wanakimbia, maadui zako wanatamtukuza Mungu wako.
Siku moja nilikutana na majirani zangu wamembeba binti yao aliyepagawa mapepo, wanaume kama 4 hivi. Nikauliza kulikoni, wakasema binti anapiga ngumi na mateke kama Tyson. Ikabidi nisaidie, na ktk ile purukushani, yule binti akanipiga kibao cha uso. Maumivu yale ya kibao kile, ndipo nikatambua shetani amenipiga, na ulokole wangu, kwa hasira nikasema "acheni nimwombee". Nilipo mwekea mkono kwenye paji la uso na.kuanza kukemea kwa Jina la Yesu, watu wote wakamweka chini na kuniachia peke yangu. Nikapambana naye huku nikikemea kwa nguvu zote. Ghafula yale mapepo yakakubali kumwachia. Mara yule binti ufahamu ukalejea, akaanza kuvaa nguo zake vizuri na kuona aibu. Wale ndugu wakashangaa (japo waliendelea kugangania Imani yao), na Mungu wangu alitukuzwa.
Tunaye Mungu ndani yetu mwenye uwezo, tuna Mungu asiyeshindwa wala kubadilika. Na ni Mungu ambaye ujitukuza kupitia sisi.
Shalom.

No comments:
Post a Comment