Kati ya vitu ambavyo Mungu alimpa mwanadamu ni pamoja na KUCHAGUA! Kila kinachotokea kwako mara nyingi ni jinsi ulivyoamua kuchagua. Kuchagua kufaulu au kufeli, kuwa mtakatifu au mdhambi, kujiongoza au kuongozwa. Watu wengi tunashindwa kuchagua. Nimeamua kuchagua! Amua, anza!
*Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;*
KUM. 30:19.
✅Enzi na enzi maisha ya mwanadamu yaliongozwa na kuchagua; Adam na Hawa walichagua kutoisikia sauti ya Mungu wakamsikiliza nyoka *walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.*
MWA. 2:17
✅Esau alichagua kuitii njaa akauacha mbaraka wa mzaliwa wa kwanza *Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.*
MWA. 25:34
✅Samson alichagua kumwambia siri Delila akapoteza agano lake kwa kumwambia adui siri za nguvu zake *Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu*
AMU. 16:17.
✅Mtume Paulo aliyaacha mambo ya faida kumfuata Kristo *Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.*
FLP. 3:7
✅Wanafunzi wa Yesu wanasema waliacha vyote *Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe.*
MK. 10:28 🏹Uchaguzi katika maisha yako unatengeneza kila kitu. Amua kuanza, amua kumtii Mungu, chagua ushindi. Jifunze kufanya maamuzi sahihi wakati wote.
*√Salamu kutoka makanisa ya PSAG ( Pentecostal Salvation Assemblies of God)!*Pastor Kyaruzi

No comments:
Post a Comment