Friday, June 10, 2016



 KUUKOMBOA WAKATI

Ef 5:15-16 "Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu"!

WEWE NI NANI ?
Umeshawahi kujiuliza wewe ninani?
Je unafaham umetoka wapi?
Na je' unajua unaenda wapi?...
Je umewahi kuwaza au kujiuliza kama hapo ulipo ndipo unapotakiwa kuwepo?
Je' toka upewe nafasi yakuwepo ulipo umeshafanya unacho takiwakufanya?
Je' ulishawahi kujiuliza kwanini haikua jana? Kwanini imekua leo?
Je' unafaham kua umeaminiwa kuwepo ulipo? Kama bado ulikuahujafaham, basi lifaham hilo, ili usimame kwenye nafasi uliyopewa. Acha manung'uniko unapoteza nguvukazi, chamsingi komboa wakati jitahidi kumaliza sehemuyako vyema kwa umakini mkubwa na ubunifu mkubwa.
UMEAMINIWA-Miriam Mauki

Thursday, June 9, 2016




Kanisa la Agape Christian Fellowship, Kimuli Karagwe! Kanisa hili linaongozwa na Mch Paul Maulid na lina waumini wanaozidi 250! Bwana anazidi kuonekana. Kila kazi itapimwa!

Kazi Yako Itapimwa
1 Kor 3:10
"Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake".
Kazi yako mpendwa ni ya muhimu iwe kwa kanisa au huduma uliyopewa na Mungu popote. Itapimwa na utalipwa. Hakikisha unalijua kusudi la Mungu kukuweka mahali ulipo na unalitimiza, ndipo uingoje taji yako!
Mungu akubariki na kukulinda

Tuesday, June 7, 2016

 Mama Judy Lamborn alikuwa ni Mmishenari aliyeipigania Injili toka New Zealand !
Alifika kanisani kwetu Agape Christian Fellowship na akatuasa sana juu ya kumtumikia Mungu bila kuzitelekeza familia zetu. Hii ilikuwa 07 Juni 2015.

Hata hivyo, ilikuwa safari yake ya mwisho na alifika Tanzania, akiwa Karagwe na alizikwa Karagwe Kayanga kwa kadiri ya wosia wake kwamba azikwe popote atakapoitiwa na Bwana.
Leo nikikumbuka mwaka mmoja tangu amekuja kutuhudumia, nafarijika na neno  1Thesolonike 4:13-18 " Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.."
Tunalo tumaini katika Kristo, atamfufua siku ile!


 Mbeba maono, Mwanzilishi wa makanisa ya Agape Christian Fellowship, C.N. Lucas akihudumu kama mkalimani, wakati Mmishenari Tony Lamborn toka New Zealand akitufundisha. Ujumbe wake ulikuwa THE POWER OF VISION (NGUVU YA MAONO). Neno katika Mithali 29:18 "Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria"
Maono hutupa sababu ya kuendelea kuishi, hutupa sababu ya kusonga mbele kwa sababu tunayo dira ya tunakoelekea.

Jifunze kuandika njozi / maono yako, omba Mungu ayatimize. Kama kuna kosa kubwa maishani ni kuishi bila maono na kutojua kusudi la maisha yako!




Kutoka kulia: Mch C.N. Lucas, Mzee Lamborn, aliyetwaliwa Mama Judy na pastor Remigius Kyaruzi wakiwa kanisani Agape Christian Fellowship, Kitunda Kibeberu, Dar es salaam. Hapo ni 07 June 2015

Maneno Ya kutafakari

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako Nisije nikakutenda dhambi. Zaburi 119:11

Mwanangu Sikiliza na kuzipokea kauli zangu na Miaka ya maisha yako itakuwa mingi. Mithali 4:10

Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia zangu. Zaburi 119:105

Neno lako limesifika sana kwa hiyo mtumishi wako amelipenda. Zaburi 119:140

Ezekieli 3:1-3
 Akaniambia mwanadamu lisha tumbo lako ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo, Ndipo nikalila nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu kama utamu wa asali.

Maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Waebrania 4:12

Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na tenzi za rohoni huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Wakolosai 3:16

Yafahamu sana haya nisemayo kwamaana Bwana atakupa akili katika mambo yote. 2Timo¬theo 2:7

Thursday, June 2, 2016

Mpingeni Shetani


1 Pet. 5:8-9
“Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.”

YAK. 4:7
“Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.”
--------
Mpinge Shetani, unaambiwa, na atakukimbia! Ni vizuri akukimbie, awe mbali nawe. Na hii ndio namna ya kumpinga;
1. Uwe na kiasi (self control). Hii ni moja ya silaha nzuri sana itakukuzuwia kutumbukia ktk mitego mingi ya Ibilisi anayekuzungukia kila wakati ili akunase.
2. Kesha. Usisinzie, kuwa makini, kuwa macho, dumu ktk Bwana, dumu ktk neno, dumu ktk imani! Huwezi kumpinga wakati upo legelege kiimani, haiwezekani. Imani hutupa ushindi.
3. Mtii Mungu. Ishi anavyotaka uishi, kamata anachotaka ukamate, acha asichokitaka!

Fanyia kazi maisha yako ya kiroho, tengeneza UTII, KIASI na KUKESHA ktk maisha yako.
BARIKIWA NA BWANA!!!!
By pastor Chikojo

Tuesday, May 17, 2016

Mwanzilishi na mbeba maona ya Agape Christian Fellowship, Mtumishi wa Mungu C. N. Lucas.
Mungu amekuwa akimtumia kama muhubiri wa kimataifa , akiifanya kazi ya Mungu kwa zaidi ya miaka 40!
Amewezesha kueneza Injili hasa vijijini ambako wengi hawafiki, na hakika Mungu anaonekana.

Tunamwombea Mungu azidi kumlinda na kumpigania, afikie mwisho mzuri wa utume wake

2 Timotheo 4 : 7-8 "Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, baili na wote pia waliopenda kufunuliwa kwake"


Monday, May 16, 2016

Mtumishi wa Mungu dada Anna Kiyungu akifundisha akina mama wa Agape Christian Fellowship Kitunda Dsm.
Semina yetu ilihusu MWANAMKE KAMA NGUZO YA KANISA NA FAMILIA.
Semina itakoyofuatia ni Ujasiriamali!