INUKA UENDELEE NA SAFARI
1 Wafalme 19: 1-18
Maisha yetu hapa duniani ni safari. Ni safari ya ki roho na
kimwili. Katika safari hii, wakati mwingine tunachoka, tunakata tamaa kwa
sababu ya vikwazo mbalimbali. Inafikia hatua tunashindwa kuendelea na tunakaa
chini, kuzila, kunyanyua mikono au kuacha kile tulichokusudia kufanya.
Ujumbe unatutia ujasiri na nguvu mpya katika safari yetu. Mungu
anatukumbusha kuwa yuko pamoja nasi, na lile kusudi alilokuumbia, lazima
utalitimiza (Yer1:4-5).
Eliya alikumbana na hofu kubwa na mashaka kwa vitisho vya
Yezebel (1Fal 19:1-3). Pamoja na ushindi mkubwa wa kumdhibitisha Mungu wa kweli
na uwezo wake (1Fal 18:36-40), Eliya alioenda kujificha na kuacha mpango wa
Mungu.
Wengi wetu tuna ushuhuda mwingi katika maisha yetu juu ya
matendo makuu ya Mungu, lakini shida kidogo ikitukumba hofu na mashaka uinuka
na kutukatisha tamaa. Inawezekana unatamani, kujificha, kupotea, ua kuacha
kazi. Unatamani ujiue, ufe kabisa. Lakini ashukuriwe Mungu kwani anakuona pale
ulipoketi chini ya mretemu.
Ujumbe huu ni kwa ajili ya kukutia moyo wa kuinuka ili
uendelee na lile kusudi la maisha yako kwa Imani dhabiti.
Ni maombi yetu kwa Mungu aseme nasi leo kwani safari bado inaendelea.
Lile kusudi la maisha yako alijatimia, usikate tamaa. Mungu kutie nguvu ya kuendelea
mbele zaidi. Sauti ya Mungu inakuita kwa upole hapo ulipo “Inuka, ule; maana
safari hii ni kubwa mno kwako” (1Fal 19:7).
Rev. Remi, R.K,
Agape Christian Fellowship
Kitunda – Dar es Salaam.
+255 713 386 315