Friday, May 18, 2018

*JE   NI  HALALI  KI-BIBLIA MWANAMKE  KUHUBIRI KANISANI*

                  *AU*

*KUWA  MCHUNGAJI  ❓*

      ( Sehemu ya kwanza )
<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>

Mistari muhimu ya kukumbuka:-

 *1 WAKORINTHO 14:34-36:-*

*34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.*

*35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.*

36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?


*1 TIMOTHEO 2:11-12:-*

11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

*12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.*

πŸ“–πŸ“–πŸ“–πŸ“–πŸ“–πŸ“–πŸ“–πŸ“–πŸ“–

HII NI MADA YENYE UBISHI MKUBWA miongoni mwa vichwa vya watu wengi . Na maandiko hayo kwa kueleweka isivyo sahihi hutumiwa na baadhi  ya watu wengi  kujaribu kujenga hoja zao za kupinga kwamba mwanamke hana haki yoyote ya kuwa Mchungaji wala kusimama madhabahuni  kuwahubiria watu kanisani.

Jambo hili limeleta mzozano mkubwa na mpasuko ndani ya makanisa mengi ya Mungu, kuhusu uhalali wa mwanamke kuhubiri madhabahuni na kuwa Mchungaji. Kuna mawazo ya positive na Negative,  kuna wengine wanaona ni  sahihi na kuna wengine kwao siyo sahihi kabisa .

Sasa basi ukweli na usahihi  wa maandiko hayo ni upi  basi?  Je, ni sahihi kwamba  mwanamke hatakiwi  kuhubiri madhabahuni kanisani au kuwa Mchungaji ?     Tatizo ni kwamba Maandiko hayo hayaeleweki  vizuri  kwa kwa wakristo wengi  na hata baadhi  ya wachungaji  na Maaskofu, wanalifafanua hilo Andiko kwa maana potofu kabisa .

*NB:-*

Kuitwa Mtume, Nabii  Askofu au Mchungaji n.k. Siyo kigezo kikubwa  cha kwamba wewe unaielewa sana Biblia kwa usahihi wake. La asha ! Ndiomaana wako hata wachungaji wengine tena wengi tu ambao huyatafsiri maandiko isivyo na kuyapotosha kwa tamaa zao wenyewe.

MWALIMU MKUU WA BIBLIA NI ROHO MTAKATIFU; yeye ndiye aliyeyaleta maandiko hayo kwetu. Na hatuwezi sisi  kuamua  kuyatafsiri  maandiko hayo  vyovyote tu  kama apendavyo mtu fulani  kutafsiri.  La Asha
*[ 2 PETRO 1:19-20 ]*.
Bali katika kanuni za kuyatafsiri maandiko, tunahitaji sana maongozi ya msaada wa Roho Mtakatifu mwenyewe  katika kuyasoma na kuyaelewa maandiko vizuri  na kuyatafsiri kwa usahihi wake. Neno la Biblia.  Tunaweza kulifaham kwa kufunuliwa na Roho Mtakatifu pekee yake. Ndiomaana  Yesu alisema *uliwaficha wenye hekima na Akili (Wasomi), ukawafunulia  watoto wachanga (Watu wasio na elimu)*. Naam,  Baba,  kwa  kuwa ndivyo ilivyokupendeza mbele zako [ MATHAYO 11:25-26].   *"Lakini  Mungu  ametufunulia  sisi  kwa  Roho Mtakatifu*.  Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo  ya Mungu.  Lakini  sisi  hatukuipokea  roho  ya  dunia,  *bali  Roho atokaye  kwa Mungu makusudi  tupate kuyajua  tuliyokirimiwa  na Mungu "*.
[1 WAKORINTHO  2:10-15].

Si  hilo  tu. Nikodemo  alikuwa  ni  mwalimu mkuu  wa  chuo  cha  Torati.  Na  watu  walimwamini  sana  katika  Taifa  la  Israeli.  Lakini  Nikodemo  alipoambiwa na  Yesu  maneno  mepesi  tu ya Mungu , na  usomi  wake wote,  alishindwa  kuyaelewa  maana  yake nini  !!  Sasa  Yesu ambaye  hakupita  chuo  chochote  cha  Theolojia, ikambidi amfundishe Nikodemo,  mwalimu  mkuu  wa  chuo  cha  Theolojia  ya Torati.
[ YOHANA 3:1- 10 ]

Sisemi  wala kupinga kwamba kusoma chuo  cha  Biblia ni  kosa au  ni vibaya, au ni  dhambi.  Hapana. Ni nini  maana  ya kuanza kukwambia  hayo. Maana  yangu  ni  hii kwamba :- Ondoa  dhana  potofu ukafikili kila  mtu anayeitwa  Mchungaji,  Askofu au  Mwanatheolojia fulani msomi  anaielewa  sana  Biblia ki-maana. Ukiwa  na  mawazo  hayo tu,  utapotezwa  na  kudanganyika  sana Mpendwa . Na Mungu huwa  hatendi  kazi  kwa  misingi  hiyo. Mchungaji /Ev/ Mwanatheolojia huyo  *Anaweza kuielewa Biblia kwa namna fulani tu ya  akili hivi ,  lakini asiweze kabisa  kuielewa Biblia kwa jinsi  ya  rohoni  zaidi kwa ufunuo  wa Roho Mtakatifu*. Na  maana  ya  kweli  ya  maneno  ya  Biblia hutumbalikana  kwa  jinsi  ya  rohoni zaidi  na  sio  kwa  jinsi  ya  mwilini.
[ WAGALATIA 1:11-12 ; WAEFESO  1:17-19].

Hivyo  ni  vema  zaidi  tusiweke vipimo  vyetu  vya  usomi kama  kigezo  cha  kuitafsiri  Biblia; bali tumuhitaji  sana Roho wa Mungu ndio  atuongoze katika kulitafsiri  Neno lake  Mungu.

*Je,  ni  halali Mwanamke  kuhubiri  au kuwa  Mchungaji?*

Jibu :- Ni  ndiyo  kwa  herufi  kubwa.

Tutajifunza  somo  hili kwa  kuligawa  katika  vipengele  vinne.  Ambavyo  ni :-

*(1) HOJA POTOFU KUHUSU  MWANAMKE KUTOKUWA  MCHUNGAJI / MUHUBIRI.*


*(2) UHALALI WA MWANAMKE KUHUBIRI / KUFUNDISHA KANISANI*.


*(3) UHALALI  WA  MWANAMKE KUWA  MCHUNGAJI*


*(4) UFAFANUZI  WA  ANDIKO  LA  1 WAKORINTHO 14:34-35 NA  1 TIMOHEO 2:12*.


KIPENGELE NO:1

*HOJA POTOFU KUHUSU MWANAMKE KUTOKUWA MCHUNGAJI/ MUHUBILI*.

Ukiwasikia watu wengi  wanaopinga mwanamke kuhubiri au kuwa Mchungaji.  Mbali na kutumia Andiko  la 1 Wakorintho 14:34-35 na  1 Timoheo  2:12-15 katika ufafanuzi wao .

Pia watajenga  hoja  yao  nyingine  ni kwamba *MWANAMKE  NI  KIUMBE DHAIFU* na hivyo wataeleza mengi  tu  katika kufafanua hoja yao hii.

Lakini mbele za Mungu, hoja ya mwanamke kutokuhubiri au kuwa Mchungaji kwa sababu  eti  ni  kiumbe dhaifu. Hoja kama hii haikubaliki na wala haina maana yoyote.  Kwa sababu Biblia inasema kwamba *Hao  hao  watu  walio dhaifu machoni petu ndio Mungu anayewachagua kuwa watumishi wake*. Neno la Mungu linasema katika

 *1WAKORINTHO 1: 26-29:-" Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; TENA MUNGU ALIVICHAGUA VITU VINYONGE VYA DUNIA NA  VILIVYODHARAULIWA (WANAWAKE), naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu."*

Kwa maana hiyo ni muhimu kuzidi kuelewa na kufaham vizuri kwamba siku zote Mungu huwa hamchagui mtu yoyote kuwa mtumishi wake katika ngazi  yoyote ya utumishi wa kihuduma kwa sababu tu  ya  kigezo cha jinsia  yake kwamba  ni  kike  au  kiume. Hapana. Mungu hachagui mtu yoyote kwa kigezo cha sifa, umri,  cheo au  jinsia  yake. Mungu huwa hatumikiwi wala kutenda kazi kwa misingi hiyo. Biblia inatuambia katika

*1 SAMWELI 16:7-10*:-

*7. Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA HAANGALII KAMA BINADAMU AANGALIAVYO; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.*

8. Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye *akasema, BWANA hakumchagua huyu*.

9. Ndipo Yese akampitisha Shama. *Naye akasema, wala BWANA hakumchagua huyu*.

10. Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. *Samweli akamwambia Yese, BWANA hakuwachagua hawa*.


*WAFILIPI  3:3-4:-"Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, WALA HATUUTUMAINI MWILI. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi."*

Kwa sababu hiyo. Mungu katika mpango wake anaweza kumchagua  mtu  yoyote  yule bila kujali  sifa  yake,  umri  wake au  jinsia  yake kwamba ni  *mwanamke* au mwanaume , Mungu anaweza kumchagua awe mtumishi  wake katika  ngazi  yoyote ya  utumishi na tena  akamtumia kwa viwango visivyo vya kawaida. Kwa hiyo sisi wanadamu hatupaswi  kuamua  kumpangia Mungu kwamba mwanamke hawezi  kuwa Mchungaji au muhubiri. Kivipi !? *TUSILETE MFUMO-DUME NDANI YA KANISA LA MUNGU*. Hilo ni chaguo la Mungu sio  la  kwako  wewe mwanadamu. Na kwa maana hiyo Mungu akiamua kumchagua mwanamke kuwa Mchungaji, Askofu,  Mwinjilisti,  mtume,  Nabii n. k. Atakuwa hivyo  Mchungaji, mtume, Nabii  na kadhalika. Biblia inasema katika

*WARUMI 9:11-16*:-"
 (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, *ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye)*, aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia. Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!
Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. *Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu."*


*WAEBRANIA 5:4:-" Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ILA YEYE AITWAYE NA MUNGU*, kama vile Haruni ".

Na kwa maana hiyo.  Ngazi yoyote ya utumishi katika huduma mtu huwekwa na Mungu . Mungu akiamua kumwita mwanamke awe mchungaji, atakuwa ni Mchungaji tu na Mungu atajidhihirisha kwake kwa kumthibitisha kwamba yeye ndiye aliyemuita. *Wako wachungaji  wanawake na  wahubiri duniani ambao Mungu anawatumia kwa viwango vya juu sana katika huduma zao*.  Hatuwezi kukanusha na kupinga  utumishi wao kwa sababu tu ya kijinsia. *Yesu alisema kama hamniamini  mimi, ziamini zile kazi  , kwa kuwa kazi zenyewe zanishuhudia ya kwamba Baba Mungu amenituma*.
[ YOHANA 5:36; YOHANA 10:25, 36-38; YOHANA   14:10-12].


*HOJA YAO  YA PILI.*

*Watasema hata maandiko yanamtaja kwamba mwanaume ndiye anayepaswa kuwa Mchungaji (Askofu). Uaskofu ni ngazi ya juu ya madaraka ya kichungaji*.

Na watatumia Andiko lao  hili lifuatalo katika
*1 TIMOHEO 3:1-12:-*

1-7. Ni neno la kuaminiwa; *mtu akitaka kazi ya askofu*, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, *MUME(MWANAUME) wa mke mmoja*, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)
Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.

8-12. *Vivyo hivyo mashemasi* na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu; wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
*Mashemasi na wawe WAUME wa mke mmoja*, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu. "

Ni muhimu kuelewa vizuri Andiko hilo kwa kusema *mwanaume hapo ndiwe Askofu*. Haimanishi kwamba basi  limemkataza Mwanamke asiwe mchungaji au  Askofu. Hapana. Kwa sababu ukitazama mukadha mzima wa maelezo  yote ya Andiko nzima, yameendelea  kusema pia *" MASHEMASI NA WAWE WAUME wa mke mmoja "*. Sasa Je,  kwa kusema hivyo tuseme Paulo Mtume hapo hakuwaruhusu pia  wanawake wasiwe  washemasi kwa sababu tu amewataja wanaume? Jibu ni  hapana.

Tunaona pia walikuwepo *MASHEMASI WANAWAKE* ambao pia Paulo mtume aliwachagua katika kanisa. Ukisoma katika *WARUMI 16:1*, Biblia inasema:- *" Namkabidhi kwenu Fibi, Ndugu yetu, aliye muhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea"*.  Mstari  huo katika Biblia ya kingereza ya *New International Version*, unasomeka hivi,  *Romans 16:1:-" I commend  to  you  our Sister Phoebe,  a Servant (deaconess) of the church in Cenchrea"*.

Kwa hiyo tunaona hapo  juu ya Shemasi Mwanamke ingawa katika Waraka wa Timotheo wanatajwa tu kuwa mashemasi wanaume tu. Kwa maana hiyo tunapata kuelewa kwamba Andiko la *1 TIMOTHEO 3:1-12*, Ingawa liliwataja maaskofu na mashemasi kuwa wanaume hapo , lakini hakumaishi kwa wanaume tu pekee yao , bali hata wanawake pia  wanaweza kuwa mashemasi,  na vilevile  wachungaji (maaskofu) pia kwa msingi huo.

Ni muhimu kuyaelewa maandiko  ya Biblia vizuri sio  kila mahali andiko linapotaja jambo  kwa  upande mmoja linamainisha  tu  kwa upande mmoja pekee  yake . Hapana. *Linaweza kutajwa  kwa upande mmoja, lakini  halikumainishi kuishia  tu  kwa  upande mmoja, bali  kwa pande zote mbili*. Kwa  mfano , Yesu alisema, kila  mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani  amekwisha kuzini  naye  moyoni  mwake [ MATHAYO 5:27-28].

Sasa Swali la ufaham :- *Andiko  hilo hapo linamgusa tu  mwanaume kumtamani  mwanamke ndio  dhambi. Lakini Je, tuseme  mwanamke naye akimtamani mwanaume kiuasherati, itakuwa siyo dhambi?*  Kwa sababu tu eti  Andiko hilo limemtaja tu mwanaume hapo?  Jibu ni la!

Na kwa msingi  huo  huo hata  kama Biblia imewataja wanaume kuwa ndio  wawe  maaskofu  na mashemasi.  Neno  hilo  halikuishia  kumainisha  tu kwa  wanaume pekee  yao  bali  hata  kwa  wanawake  pia wanaweza kuwa wachungaji  au  maaskofu,  mashemasi,  mitume,  manabii n.k.

Ni muhimu kufaham Biblia  inasema katika  *MATENDO  10:34-35:-*

*" Petro akafumbua  kinywa  chake, akasema, HAKIKA NATAMBUA  YA  KUWA  MUNGU HANA UPENDELEO; bali  katika  kila taifa mtu  amchaye  na  kutenda  haki hukubaliwa  na  yeye. "*

Kusema kwamba mwanaume tu  ndio  anayepasa  kuhubiri  na  kuwa  Mchungaji lakini  mwanamke  hafai kwa lolote. Huo ni  upendeleo.  Mungu  wetu  hana  upendeleo  wa  aina  yoyote ile , kila  mtu  awe  ni  mwanaume  au  mwanamke bado Mungu anaweza  kuwatumia  wote sawasawa  katika  nafasi  yoyote ile  ya  utumishi iwe  ni  uchungaji na  kadhalika.

Ni  muhimu  kufaham  katika  suala  la  utumishi  wowote  mbele  za  Mungu. Mwanaume  hawezi  kujivuna  na  kujiinua kwamba  yeye  anastahili sana  zaidi  ya  mwanamke. Katika imani  ya  wokovu  iliyobeba utumishi ndani yake, sisi wote ni sawasawa mbele  za Mungu.  Hakuna mmoja aliye bora wa kujiinua  juu zaidi  ya  mwingine. Biblia inasema katika

*1 WAKORINTHO 12:17-27:-*

*" BALI MUNGU AMEVITIA VIUNGO KILA KIMOJA KATIKA MWILI KAMA ALIVYOTAKA*. Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi. *Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana*. Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na *kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa;* ili kusiwe na faraka katika mwili, *bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe*. Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, *na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho*. Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza.............."


*YOHANA 6: 28-29:-*
*"Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate KUZITENDA KAZI ZA MUNGU ? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye."*

*WAGALATIA 3:26-29:-*

*"Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. HAPANA MTU MUME WALA MTU MKE. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu."*.

Maandiko  hayo kwa ujumla wake yanatufundisha Mungu ndiye anaweza  kuamua kumuweka mtu yoyote katika nafasi  yoyote  ya  utumishi wa kazi ya huduma ya Mungu , huyu hivi  na  yule vile. Na kwa Mungu hakuna kigezo  cha  ubaguzi  wowote wa jinsia katika nafasi yoyote ya kumtumikia .Na kwa maana hiyo *WANAUME NA WANAWAKE WOTE KWA PAMOJA  WANAWEZA KUWA WAHUBIRI,  WACHUNGAJI,  MITUME N. k.*

Mwanaume huyu Akila na Mwanamke huyu Priska, mke  na mume.  Kwa pamoja wote wanatajwa kila mmoja wao katika  kuhusika kuifanya kazi  ya Mungu ya  uchungaji waliokuwa nayo juu ya kanisa.
*[ WARUMI 16:3-4. ]*


Somo hili litaendelea sehemu  ya pili........


🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺

Unakaribishwa pia kujiunga  na group letu.

Mtumishi wa Mungu aliye hai.

*MWL,  REV:- ODRICK BRYSON*

*SIMU (0759 386 988; 0717 591 466)*.

Whatsap group.

Email :- Odrick 16@gmail. Com.

*" KWELI YOTE YA NENO LA MUNGU ISIYOGOSHIWA"*.

[  2 WAKORINTO 2:17   ]

🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺

Monday, April 2, 2018

SOMO:JINSI YA KUIFAHAMU MIUJIZA YA MUNGU NA ISHARA ZA UONGO ZA MANABII WA UONGO (PART 1)

NENO LA MSINGI:
2 WATHESALONIKE 2:9:
"Yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa KUTENDA KWAKE SHETANI, KWA UWEZO WOTE, NA ISHARA NA AJABU ZA UONGO."

Katika somo la leo la Kanisa la Nyumbani, tunajifunza somo muhimu linaloambatana na majira tuliyo nayo ya nyakati za mwisho.  Siku hizi, mahali pengi duniani ikiwamo Tanzania, kumezuka watu wa kila namna wakisema ni watumishi wa Mungu na kwamba wamepewa karama ya kutenda miujiza kwa ajili ya kuwasaidia watu.  Kwa sababu hii, watu kila mahali wanamiminika kuwafuata, wakihitaji watoto au uponyaji mbalimbali wa mwili.  Sehemu nyingine watu hao wanaodaiwa kuwa ni watumishi wa Mungu, wanatumia maji ya baraka kuponya; wengine wanatumia sanamu ya Bikira Maria; wengine wanawapeleka watu makaburini; wengine wanakwenda kupewa maji mahali inaposemekana alitokea Bikira Maria; wengine wanapewa madaftari ambamo humo wameandikiwa kwamba "Mungu" amesema watazaa mtoto wa kiume na wameandikiwa jina la kumwita, au mtoto wa kike na jina ambalo "Mungu" amemchagulia, na kupeleka madaftari hayo kila mara kuombewa na kukatazwa kwenda kliniki n.k.  Wengine wamebeba "mimba" zilizotokana na maombezi ya watu hawa kwa miaka miwili bila kujifungua na kupata mateso makali mno.  Wengine wameshuhudia kwamba wamepona kabisa baada ya kuhudumiwa na watu wa jinsi hiyo.  Hapa ndipo penye mtego.  Ili tusinaswe na mitego ya namna hii, Kanisa la Mungu linapaswa kufahamu Biblia inasema nini kuhusu Miujiza, Ishara na Ajabu za Mungu na zile za Shetani.

SHETANI ANA UWEZO WA KUFANYA MIUJIZA, ISHARA NA AJABU ZA UONGO

Miujiza kadhaa kwa kipimo kidogo cha uwezo ulio na mpaka.  Wakati wana wa Israeli walipokuwa hawajatoka Misri, waganga na wachawi wa Farao, walifanya miujiza kwa uwezo wa shetani:
(a) Wachawi hawa walipozibwaga fimbo zao chini, ziligeuka kuwa nyoka kwa mfano wa muujiza alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na Haruni [SOMA KUTOKA 7:8-12]

(b) Wachawi hawa walifanya muujiza wa kubadilisha maji kuwa damu kwa mfano wa muujiza alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na Haruni [SOMA KUTOKA 7:19-22].

Unaona!  Shetani ana uwezo wa kufanya miujiza na ishara.  Biblia inasema katika:
UFUNUO WA YOHANA 16:14:
"Hizo ndizo roho za MASHETANI, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi."
Wakati wa dhiki Kuu, roho za Mashetani zitafanya ishara kubwa, hata kufanya moto kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.  [SOMA UFUNUO 13:11-13].
Lakini pamoja na ufahamu huu ulio nao sasa kwamba Shetani ana uwezo wa kufanya ishara na miujiza, bado inakupasa kufahamu jambo moja.  Shetani ana mpaka katika uwezo wake wa kufanya miujiza.  Hana uwezo wa Mungu wa KUTENDA MAMBO YOTE.  Shetani hawezi kutenda mambo yote.  Wachawi na waganga wa Farao ingawa walifanya miujiza tuliyoiona, hata hivyo walishindwa kufanya muujiza alioufanya Mungu kwa kuwatumia Musa na Haruni; pale walipoyabadilisha mavumbi ya nchi kuwa chawa.  Wachawi hao waliposhindwa walikiri mbele ya Farao kwamba uwezo wa Mungu uko juu mno kuliko uwezo wao.  [SOMA KUTOKA 8:16-19].  Wachawi na waganga wa Farao pia walishindwa kuzuia majipu yenye kufura yaliyotumbuka juu ya wanadamu wote wa Misri kutokana na mavumbi aliyoyarusha Musa hewani.  Wachawi hao nao walipigwa majipu hayo [SOMA KUTOKA 9:8-11].  Fimbo ya Haruni ilizimeza fimbo za wachawi kudhihirisha uwezo wa Mungu ulivyo mkubwa mno kuliko wa majeshi yote ya shetani [SOMA KUTOKA 7:11-12].

ISHARA, AJABU NA MIUJIZA YA SHETANI WAKATI WOTE INA  LENGO LA KUWAPOTEZA WANADAMU ILI WAANGAMIZWE

MATHAYO 24:24:
"Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu WAPATE KUWAPOTEZA, kama yamkini, hata walio wateule."
Ishara, ajabu na Miujiza ya Shetani ndiyo maana inaitwa pia "NGUVU YA UPOTEVU" kwa jinsi ambavyo miujiza hiyo ilivyo madanganyo ya udhalimu kwa hao wanaopotea ambao hawataki kuiamini kweli ya Mungu na kuokolewa na hatimaye kuzidi kuipenda kweli katika wokovu.  Nguvu hiyo ya upotevu juu ya wanadamu, hatimaye inawafanya wanadamu hao kuhukumiwa na kwenda Jehanum ya moto.  [SOMA 2 WATHESALONIKE 2:7-12].  Kwa sababu hii, Kanisa la Mungu lazima liwe macho na kufahamu waziwazi jinsi ya kuzifahamu ishara, ajabu na miujiza ya Shetani na kutofautisha na ile itokanayo na Mungu.  Kwa maarifa haya, ni rahisi kuziepuka kazi zote za Shetani na manabii wake; na pia kuwasaidia wengine waliokwisha kunaswa.
ALAMA TISA ZINAZOAMBATANA NA ISHARA, AJABU NA MIUJIZA
 INAYOTOKANA NA MUNGU

Kwa kuangalia alama hizi tisa zifuatazo, na kuhakikisha kwamba ZOTE ZINAKUWEPO; ndipo tunapoweza kuzitambua ishara, ajabu na miujiza inayotokana na Mungu na kuifahamu na kukwepa miujiza ya Shetani na manabii wake:

(1) Mtu anayetumiwa kufanya ishara, ajabu au miujiza na Mungu, inabidi awe ameamini au kuokolewa;  akikiri mwenyewe wokovu ulio katika Kristo Yesu na kuushuhudia.
 MARKO 16:17;  "Na ishara hizi zitafuatana na hao WAAMINIO .....".
Mtu yeyote asiyeokolewa na kukiri wokovu na kuushuhudia, hawezi kufanya miujiza itokanayo na Mungu.  Miujiza hiyo hutokana na Shetani.

(2) Huduma ya Uponyaji au Ishara yoyote inayotokana na Mungu lazima iambatane na Biblia au Neno la Mungu kwa kuwa Neno la Mungu ndiyo dawa ya Ugonjwa na tena ndilo linalofanya
miujiza.  Huduma yoyote ya uponyaji wa miujiza isiyoambatana na Biblia au Neno la Mungu, inatokana na Shetani.
 ZABURI 107:20: "HULITUMIA NENO LAKE, HUWAPONYA, huwatoa katika  maangamizo yao."
 MITHALI 4:20-22: "Mwanangu, SIKILIZA MANENO YANGU; ....UZISIKIE KAULI  ZANGU .....MAANA NI UHAI kwa wale wazipatao, na AFYA YA  MWILI WAO WOTE."
 YOHANA 6:63: ".....MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA niroho tena NI  UZIMA."

(3) Huduma yoyote ya Uponyaji wa Miujiza inayotokana na Mungu, LAZIMA iambatane na kuhubiri Injili na kufundisha Neno la Mungu, Angalia maandiko:
(a) HUDUMA YA YESU:
(i) Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena, KULIAMBATANA na kuwahubiri maskini habari njema [SOMA LUKA 4:18].
(ii) Yesu alipokuwa akifundisha Neno la Mungu ndipo uweza wa Bwana ulipokuwapo kuponya:

LUKA 4:17:
"Ikawa siku zile mojawapo ALIKUWA AKIFUNDISHA .... NA UWEZA WA BWANA ULIKUWAPO APATE KUPONYA."

(4) YESU ALIPOWATUMA WANAFUNZI KUFANYA HUDUMA YA UPONYAJI
Wakati wote Yesu Kristo alipowatuma wanafunzi wake na kuwapa uwezo wa kuponya maradhi, au kuwaambia wapoze wagonjwa kwa miujiza; jambo hilo LILIAMBATANA na kutumwa kuhubiri au kuutangaza ufalme wa Mungu.  Mambo haya mawili lazima yaende pamoja.
LUKA 9:1-2: "Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.  Akawatuma WAUTANGAZE UFALME WA MUNGU NA KUPOZAWAGONJWA."
LUKA 10:1-2, 9:  "Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine,sabini, akawatuma wawili wawili .... Akawaambia ... WAPOZENI WAGONJWA waliomo, WAAMBIENI, UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA."
MATHAYO 10:7-8:  "Na katika kuenenda kwenu, HUBIRINI,mkisema, Ufalme wa Mbinguni umekaribia.  POZENI WAGONJWA, FUFUENI WAFU, TAKASENI WENYE UKOMA, TOENI PEPO; mmepata bure, toeni bure."

Katika kujifunza juu ya Huduma ya Yesu ya miujiza na uponyaji, na ile ambayo aliwapa wanafunzi wake; umeona kwamba kuponya wagonjwa kwa miujiza na kufanya ishara na ajabu zinazotokana na Mungu, LAZIMA kuambatane na kuhubiri Injili, na kuwaambia watu watubu dhambi zao na kuokolewa maana ufalme wa Mungu umekaribia.  Ukimwona mtu anasema ni mtumishi wa Mungu na kwamba eti amepewa karama na Mungu kuponya wagonjwa, halafu akawa nyumbani kwake tu au ofisini kwake na watu wanamwijia kuponywa bila kuelezwa habari za kutubu na kuokolewa, ufahamu huyo ni nabii wa uongo, na anatumia NGUVU YA UPOTEVU ya Shetani kufanya ishara za uongo.  Uponyaji wa Miujiza wa Mungu hauwi kama hospitali ambapo watu wanaenda kupewa vidonge tu bila kuhubiriwa Injili.  Miujiza lazima iambatane na kuhubiri Injili.  Mtu ukimsikia anasema yeye amepewa karama na Mungu kuponya wagonjwa tu, lakini hakupewa karama ya kuhubiri; hivyo kuhubiri amewaachia wengine, ujue huyo ni nabii wa uongo.  Yeyote aliyepewa kufanya miujiza na Mungu, pia huyohuyo atahubiri Injili.  Yesu, Petro, Paulo, Filipo na yeyote katika Biblia walifanya miujiza PAMOJA NA kuhubiri Injili.

Uponyaji wowote, muujiza wowote, au ishara yoyote inayofanywa kutokana na Mungu LAZIMA IFANYWE KWA JINA LA YESU SOMA:  LUKA 10:17; MATENDO 4:30; MARKO 16:17; MATENDO 3:6;  MATENDO 4:10; MATENDO 3:13, 16; MATENDO 16:18. Jina la Yesu, ndilo linalomtia mtu dhaifu, nguvu.  Imani katika Yesu ndiyo inayoleta uzima [MATENDO 3:16].  Ukimwona mtu anayejiita mtumishi wa Mungu na kwamba anaombea wagonjwa, lakini halitumii Jina la Yesu ila anamtaja "Mungu" tu; ujue mtu huyo ni nabii wa uongo.  Hakuna muujiza wowote wa Mungu pasipo kulitaja jina la Yesu!  "PEPO WANATUTII KWA JINA LAKO", "KWA JINA LANGU WATATOA PEPO."  Siyo kwa jina la Mungu au kwa kumtaja Mungu ila kwa jina la Yesu.  LAZIMA Yesu atajwe katika kuufanya muujiza unaotokana na Mungu.

(5) Mtu anayetumiwa kufanya miujiza, ishara au ajabu na Mungu, hukusanya pamoja na Yesu, na kutumia miujiza kuliongeza Kanisa la Mungu kwa wale waaminio au wanaookolewa.  Lengo la Mungu kutoa uwezo wa kufanya miujiza kwa watumishi wake, ni kuwafanya wasioamini waweze kuamini kwa kuziona nguvu za Mungu.  Huduma yoyote ya miujiza isiyokuwa na lengo la kuwaongeza walioamini kwa Bwana Yesu au katika Kanisa la Mungu siyo huduma ya Mungu.

 MATENDO 5:12,14:
"Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; ....walioamini wakazidi kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake".

Miujiza hutumika kukusanya watu na kuwaleta katika Kanisa ambalo kiongozi wake ni Yesu [SOMA PIA LUKA 11:23; MATHAYO 23:37; ZABURI 50:5].

INAENDELEA.................

KWA MAWASILIANO NAMI
SHUJAA  Charles Mwaisemba
0712-054498/0759-420202
Limefundishwa na ASKOFU ZACHARY KAKOBE